Thursday, April 25, 2013

Wazayuni kuidhinisha mauaji ya Wapalestina

Bunge la utawala haramu wa Kizayuni (Knesset), limeazimia kupasisha muswada utakaotoa  ruhusa kwa walowezi wa Kizayuni kuwashambulia Wapalestina. Mbunge wa mrengo wenye kufurutu mipaka katika bunge la utawala huo OritStruk, ametaka kupitishwa sheria iliyopewa jina la Drumi katika vitongoji vilivyoko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Ikiwa sheria hiyo itapitishwa, basi itaambatana na kutolewa idhini ya mashambulizi ya walowezi hao dhidi ya Wapalestina na kuongeza vitendo vya dhuluma na ukandamizaji wa Wazayuni dhidi ya raia hao wa Palestina. Aidha sheria hiyo inatoa ruhusa kwa mlowezi kutekeleza mauaji dhidi ya Mpalestina kwa sababu yoyote iwayo. Hii ni katika hali ambayo kwa mara kadhaa walowezi wa Kiyahudi wamekuwa wakiyashambulia maeneo ya Wapalestina kwa msaada wa askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

No comments: