Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo ambaye alisema hakuna shida
vijana kutoka Kenya kufanya kazi Tanzania katika sekta mbalimbali.
Mulugo alisema kuwa ushirikiano wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki unatoa nafasi ya watu kutoka nchi moja na kwenda nchi
nyingine na kufanya kazi wakiwamo Watanzania kuwapokea wageni kutoka nje
na Vijana wa Tanzania kwenda nchi nyingine.
Alikuwa akijibu swali la Christowaja Mtinda (Viti
Maalumu-Chadema), ambaye alitaka kujua Tanzania ina mkakati gani wa
makusudi katika kuwaandaa Vijana wake kielimu ili waweze kushindana
katika soko la ajira la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbunge huyo pia alihoji ni kwa nini Serikali
inatoa kipaumbele kwa Vijana wanaosoma masomo ya Sayansi pekee na
kuyasahau masomo mengine yakiwamo ya masuala ya uhasibu.
Naibu Waziri alisema kuwa Serikali inatekeleza
mikakati katika ngazi zote za kielimu ya kuwaandaa vijana wa kitanzania
ili waweze kushindana katika soko la ajira la Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Alitaja baadhi ya mikakati ni kuvijengea uwezo
Vyuo vya Ufundi ili viweze kuzalisha wataalamu ambao watakuwa na uwezo
wa kitaaluma na kitaalamu wa kuingia kwenye soko la ajira ndani na nje
ya nchi.
Mulugo aliwashukuru wabunge wanaofuatilia mambo bungeni.
Aliwasihi wabunge kushirikiana na Serikali katika
mipango yake ya kuboresha vyuo vya ufundi na kwamba lengo ni kuhakikisha
vijana wengi wanakuwa na elimu hiyo na kuweza kujiajiri.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment