MICHEZO

YANGA YABADILI MSEMAJI

KAMA alivyopokea ofisi kwa mbwembwe kutoka kwa Lous Sendeu, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, amechomolewa kwenye nafasi hiyo na nafasi akapewa Jerry Muro mtangazaji wa zamani wa ITV na TBC1.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa uamuzi huo wa Yanga ulitolewa katika kikao kilichofanyika jana Jumapili ambapo sasa Kizuguto atakuwa Meneja wa timu. 

Mwanaspoti linajua ni katika hali ya kutekeleza maagizo ya Uongozi wa juu ambao unataka timu ijiendeshe kiumakini zaidi.

“Mkataba wake pia ulikuwa unakwenda ukingoni, huenda ameamua kutomwongeza mkataba mpya,” kilisema chanzo chetu ambacho kimesisitiza kwamba sasa Yanga inajiendesha kibiashara zaidi hivyo inaajiri watu kwa malengo maalum ndiyo kusudio pia la kumleta kocha Marcio Maximo kwa gharama kubwa.

CHANZO: Mwanaspoti

 SIMBA YAISHUSHA KAGERA SUGAR LIGI KUU BARA

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, jana waliwapigisha kwata maafande wa Ruvu Shooting baada ya kuwachapa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 42 na kuwashusha Kagera Sugar yenye pointi 40 kwenye nafasi ya tatu.
Katika mchezo huo, Simba ilianza kwa kasi ikionyesha uchu wa kuibuka na ushindi, ambapo dakika ya 14 Amri Kiemba alianza kutingisha nyavu za maafande hao.
Dakika ya 21, Felix Sunzu aliunganisha krosi ya Kiemba kwa kichwa lakini mpira uligonga mwamba.
Hadi mwamuzi Athuman Lazi wa Morogoro akiashiria mapumziko, Simba ilikuwa mbele kwa bao moja.
Kipindi cha pili, Ruvu walifanikiwa kuchomoa dakika ya 52 kwa bao la Abdulrahman Musa baada ya kuuwahi mpira uliozembewa na kuokolewa na Masudi Cholo na Musa Mude.
Dakika ya 86, Edward Christopher aliyeingia kuchukua nafasi ya Messi, aliwanyanyua mashabiki wa Simba vitini kwa kupachika bao la pili, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Shooting.
Kama haitoshi, Ismail Mkoko aliyeingia kuchukua nafasi ya Haruna Chanongo, aliiandikia Simba bao la tatu, akimalizia krosi ya Kiemba.
Hadi dakika 90 zinakamilika, Simba iliibuka na ushindi huo wa 3-1.
Simba: Abel Dhaira, Nasoro Masoud ‘Cholo’, Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mude, William Lucian, Haruna Chanongo, Abdallah Seseme, Felix Sunzu, Amri Kiemba na Ramadhan Singano ‘Messi’.
Ruvu Shooting: Benjamin Haule, Michael Pius, Baraka Myakamande, Nyambiso Athumani, Shabani Susan, Ernest Ernest, Saidi Madega, Hassan Dilunga, Abdulraman Musa, Saidi Musa, Saidi Dilunga,

                  RCL kuanza Mei 12, Ratiba kupangwa j'nne

RATIBA RCL KUPANGWA J'NNE, LIGI KUANZA MEI 12
Upangaji ratiba (draw) ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) uliokuwa ufanyike juzi (Mei 3 mwaka huu), sasa utafanyika Jumanne (Mei 7 mwaka huu) na ligi hiyo itaanza Mei 12 mwaka huu kama ilivyopangwa.
Uamuzi huo umefanya na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Mei 5 mwaka huu) kujadili maandalizi ya ligi hiyo, yakiwemo maombi ya baadhi ya mikoa ambayo haijamaliza yao kutaka RCL isogezwe mbele.

Kamati ya Mashindano chini ya Uenyekiti wa Blassy Kiondo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ilipitia maombi hayo na kuangalia athari ambazo zinaweza kujitokeza huko mbele iwapo RCL itasogezwa mbele.
Baadhi ya athari iwapo RCL itasogezwa mbele ni timu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutopata muda wa kufanya usajili wa wachezaji kwa msimu mpya.
Hivyo draw hiyo itakayofanyika saa 6 mchana itahusisha mikoa ambayo tayari imemaliza ligi na kuwasilisha majina ya mabingwa wao. Mabingwa ambao wamewasilishwa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC (Dar es Salaam 2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends Rangers (Dar es Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United (Pwani), Kimondo FC (Mbeya) na Machava FC (Kilimanjaro).
Mingine ni Magic Pressure FC (Singida), Mbinga United (Ruvuma), Mji Njombe (Njombe), Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast FC (Dar es Salaam 1), Rukwa United (Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya Kilombero ambayo ni Shule ya Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).
Ada ya ushiriki ni sh. 100,000 wakati usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika Ligi ya Mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.
Mikoa iliyoshindwa kuwasilisha mabingwa wake ni Dodoma, Geita, Iringa, Lindi, Manyara, Mtwara, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Tanga.
TAIFA STARS KUANZA COSAFA JULAI 6
Taifa Stars imepangwa kundi A la michuano ya Kombe la COSAFA ambapo itacheza mechi yake ya kwanza Julai 6 mwaka huu jijini Lusaka, Zambia dhidi ya Shelisheli.
Upangaji ratiba (draw) wa mashindano hayo ulifanyika juzi (Mei 3 mwaka huu) jijini Lusaka ambapo timu nyingine zilizo na Taifa Stars katika kundi hilo ni Namibia na Mauritius. Kundi la Taifa Stars litachezea mechi zake jijini Lusaka.
Mechi ya pili ya Taifa Stars katika hatua ya makundi itakuwa Julai 8 mwaka huu dhidi ya Mauritius. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo itakuwa Julai 10 mwaka huu dhidi ya Namibia.
Kundi B lina timu za Kenya (Harambee Stars), Botswana (Zebras), Lesotho na Swaziland. Hatua itakayofuata baada ya hapo ni ya mtoano (knockout) na kila kundi litatoa timu moja tu.
Iwapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itafuzu kwa hatua itakayofuata itacheza Julai 13 mwaka huu na Afrika Kusini (Bafana Bafana) ambayo pamoja na timu nyingine tano zimekwenda moja kwa moja katika hatua ya mtoano.
Nyingine zilizokwenda moja kwa moja hatua ya mtoano ni wenyeji Zambia, Angola, Zimbabwe, Msumbiji na Malawi ambazo kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ziko juu ya zile zilizoanzia hatua ya makundi.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, fainali ya michuano ya Kombe la COSAFA itafanyika Julai 20 mwaka huu.
AZAM FC KUREJEA NYUMBANI KESHO
Timu ya Azam inatarajiwa kurejea nchini kesho (Mei 6 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Emirates kutoka Morocco ambapo jana (Mei 5 mwaka huu) ilicheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya huko.
Azam ilipoteza mechi hiyo kwa mabao 2-1, hivyo kutolewa katika raundi ya pili ya mashindano hayo. Mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka suluhu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)RATIBA RCL KUPANGWA J'NNE, LIGI KUANZA MEI 12

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Bayern, dotmund fainali UEFA Wembley

Bayern watinda fainali kwa kishindo baada ya kuitwanga Barcelona 7-0 katika michezo yote miwili, wa kwanza 4-0 na wa pili 3-0.

Arjen Robben (katikati) akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza Nou Camp

Thomas Muller wa Bayern akifunga bao la tatu

Itakuwa fainali ya Wajerumani watupu Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Wembley wiki tatu zijazo Jumamosi, ikiwakutanisha Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Hiyo inafuatia Barcelona iliyomkosa Lionel Messi aliyekuwa benchi kutandikwa mabao 3-0 nyumbani usiku huu, baada ya awali kuchapwa 4-0 Ujerumani, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 7-0.
Barcelona walionekana kabisa kuzidiwa uwezo na mapema tu walionekana hawawezi kupanda mlima huo. Mabao ya Bayern ambao tayari ni mabingwa wa Ujerumani, wakiivua taji Dortmund, yamefungwa na Arjen Robben dakika ya 49, Gerard Pique aliyejifunga dakika ya 72 na Thomas Muller dakika ya 76. Chanzo: Binzubeiry.

                     MIKOA 18 YAPATA MABINGWA WA MIKOA

 Mikoa 18 kati ya 27 ya kimpira tayari imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa itakayoanza Mei 12 mwaka huu chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Timu tatu za juu katika Ligi hiyo ya Mabingwa zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014). Ligi ya FDL ina jumla ya timu 24 ambapo tatu katika ligi hiyo zilizoshuka daraja msimu huu ni Moro United ya Dar es Salaam, Small Kids ya Rukwa na Morani FC ya Manyara.

Mabingwa waliopatikana hadi sasa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC (Dar es Salaam 2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends Rangers (Dar es Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United (Pwani), Kimondo FC (Mbeya) na Machava FC (Kilimanjaro).
Wengine ni Magic Pressure FC (Singida), Mbinga United (Ruvuma), Mji Njombe (Njombe), Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast FC (Dar es Salaam 1), Rukwa United (Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya Kilombero ambayo ni Shule ya Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).
Kila klabu inatakiwa kulipa ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000 wakati usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika Ligi ya Mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.
MTANZANIA AOMBEWA ITC ACHEZE NORWAY
Shirikisho la Mpira wa Miguu Norway (NFF) limetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Godfrey Mlowoka ili aweze kucheza mpira nchini humo.
NFF inamuombea hati hiyo Mlowoka ili aweze kujiunga na klabu ya Ekne IL kama mchezaji wa ridhaa ambapo klabu yake ya zamani aliyokuwa akiichezea nchini imetajwa kuwa Sadani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika hati hiyo ya uhamisho itatumwa nchini Norway.
AZAM YAENDELEA KUJINOA MOROCCO
Timu ya Azam ambayo iko jijini Rabat kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabati ya huko inaendelea vizuri na mazoezi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari Msaidizi wa Azam FC, Jaffer Idd maandalizi yanakwenda vizuri kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Mei 4 mwaka huu). Jaffer Idd anapatikana kwa namba +212671146092.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
 
  AZAM YAIPA UBINGWA YANGA BAADA YA KUTOKA SARE 1-1 NA COASTAL UNION

Klabu ya Yanga ya Dar es salaam jana imejitangaziwa ubingwa wake wa 24 wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya wapinzani wake wakubwa kwa muda mrefu klabu YA Azam fc kutoa sare ya kufunga bao 1-1 na Wagosi wa kaya Coastal unioni katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Matokeo hayo yana maanisha, Azam FC waliokuwa washindani wakuu wa Yanga SC waliojikusanyia pointi 56 kibindoni, hawawezi tena kufikisha pointi hizo ambazo wanazo mabingwa hao wapya, kwani hata wakishinda mechi zao nyingine  mbili zilizobaki, watamaliza na pointi 54. 

Shukurani kubwa kwa  nyota wa Coastal union Danny Lyanga, ambaye aliifungia Coastal bao la kusawazisha dakika ya 72 akipokea pande maridhawa kutoka kwa nyota wa zamani wa Yanga Pius Kisambale. Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo wa leo, lililofungwa na beki Aggrey Morris kwa penalti dakika ya 60, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Gaudence Mwaikimba kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari  na beki Yussuf Chuma- na refa Andrew Shamba wa Pwani akaamuru pigo hilo.

Matokeo haya yanakuwa sawa na Coastal kulipa fadhila kwa Yanga, kwani hata wao, ubingwa wao pekee wa Ligi Kuu waliochukua mwaka 1988 ulitokana na ‘msaada’ wa wana Jangwani hao.

Kilichobaki kwa Yanga sasa ni kulinda heshima kutokana na kubakiwa na mechi mbili ambapo watashuka dimbani kuvaana na Coastal union waliowapa ubingwa msimu huu pamoja na mechi ya kufunga dimba dhidi ya Mnyama Simba uwanja wa Taifa Dar es salaam

Lakini licha ya Coastal union kuwapa ubingwa wanajangwani hao, Kocha mkuu wa wagosi Wakaya Hemed Morroco  amesema mchezo wa leo walistahili kushinda na kilichokwamisha ushindi leo ni waamuzi kuchezesha hovyo.

“Unajua Azam walikuwa na Presha kubwa ya kutaka ushindi, lakini tuliwabana na waamuzi wameshindwa kuchezesha vizuri na ndio maana wameambulia sare vinginevyo walikuwa wanafungwa leo”. Alisema Morroco.

Kikosi cha Coastal Union leo kilikuwa; Shaaban Kado, Hamad Khamis, Othman Tamim, Philip Mugenzi, Yussuf Chuma, Abdi Banda, Joseph Mahundi, Razack Khalfan, Pius Kisambale/Mohamed Soud dk85, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Danny Lyanga dk71 na Twaha Shekuwe. 
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris, Jabir Aziz/Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ dk75, Brian Umony/Seif Abdallah Karihe dk68, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk82, Humphrey Mieno na John Bocco ‘Adebayor’

Ruvu Shooting, Simba Sasa Kucheza Mei 5

Release No. 072
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 25, 2013
 
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.

Ligi hiyo inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili (Aprili 28 mwaka huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.
Boniface Wambura
Ofisa Habari, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments: