Friday, March 25, 2016

MUFTI WA TANZANIA AMUOMBEA DUA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM


MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amemuombea dua, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kulitumikia vema taifa na kuliletea maendeleo.

Zubery alimfanyia dua hiyo Makonda Dar es Salaam leo asubuhi alipofika nyumbani kwake kujitambulisha na kumjulia hali pamoja na kumueleza mambo kadhaa ya maendeleo yaliyofanyika.

"Tunakuomba mola wetu kuwapa moyo wa imani na uzalendo na kuwaepusha na mabaya yote  Mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda, Rais wetu Magufuli pamoja na viongozi wote ili waliongoze taifa letu kwa amani" alisema Mufti Zubery"  wakati akiomba dua hiyo.

Makonda akizungumza na Mufti Zubery nyumbani kwake Mikocheni alimwambia kuwa kuna mambo kadhaa ameyafanya kwa kushirikiana na watendaji wenzake kwa kukutana na waendesha boda boda ili kuwawezesha kupata mkopo utakaowasaidia kupata vitendelea kazi zao kama kupata kofia ngumu mbili za kuvaa dereva na abiria wake ili kuwasaidia katika shughuli zao za kusafirisha abiria.

Makonda alitaja mambo mengine kuwa ni suala nzima la kupambana na uhalifu ambao bado unaonesha kupamba moto hasa ujambazi wa kutumia silaha za moto.

Alitaja mambo mengine kuwa ni mkutano alioufanya hivi karibuni wa kukutana na wenyeviti wa mitaa na maofisa watendaji ili kuzungumzia suala la utunzaji wa mazingira na mambo mengine ambapo alisema ameandaa mpango wa kumzawadia mwenyekiti atakayefanya vizuri kwenye mtaa wake.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema jambo alilofanya Makonda la kumtembea Mufti ni jambo zuri na kuwa kumuona mufti ni sawa kama amewaona waislam wote nchini.

Alisema wanamuombea Makonda mungu amzidishie wepesi katika kazi zake kwani ni viongozi wachache wanaopata madaraka ambao uwakumbuka viongozi wa dini kama alivyofanya Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda alifanya ukaguzi wa barabara kadhaa za Manispaa ya Kinondoni ambazo hivi karibuni aliagiza zifanyiwe marekebisho ikiwa ni pamoja na kuchimba mifereji baada ya kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

HISTORIA YA PASAKA

JE NI KWELI PASAKA NI SIKUKUU YA KUFUFUKA KWA YESU?



JE, NI KWELI PASAKA NI SIKUKUUYA  KUFUFUKA KWA YESU?
     Adhuhuri moja wakati nikiwa nyumbani alikuja jamaa yangu mmoja ambaye aliniletea bakuli maalum la kuhifadhia chakula. Ndani ya bakuli lile kulikuwa na wali na nyama ya kuku ambavyo kwa hakika vilinitamanisha sana hasa ukizingatia nilikuwa na njaa kali. Nikaona ule ndiyo wakati haswaa wa kujifaidia kile nilicholetewa.

      Baada ya kuutwanga wali ule ndipo nilipopatwa na shauku ya kujua Yule jamaa yangu alipata wapi ujuzi wa kupika wali mtamu namna ile na kumtayarisha kitaalamu, kuku yule wa kienyeji. Ndipo jamaa yangu aliponiambia kuwa chakula kile amekipika maalum kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya kufufuliwa kwa Yesu Kristo maarufu kwa jina la Pasaka.

       Kwa miaka mingi nimekuwa nikisikia kuhusu siku hiyo na ndipo baada ya kuambiwa vile na jamaa yangu, nilipoamua kuandika makala haya ili kuuelezea umma juu ya historia ya sikukuu hiyo na mwanzilishi wake na lengo la kuwepo kwake.

Historia ya pasaka
    Pasaka ni sikukuu iliyoanza kwa nabii Mussa, kumbuka kuwa wana wa Israel walikuwa utumwani nchini Misri chini ya utawala wa mfalme Firauni(Farao) takribani miaka 400 walikuwa wanateswa na mfalme Farao.

    Baada ya mateso ya muda mrefu mungu akamtoa Mussa na kumfanya kwa Nabii na akaamrishwa kwenda kupambanana na Farao ili awakomboe wana wa Israel na wawe huru.Ndipo Mussa akaenda kwa firauni na akafanikiwa kumshinda Farao.

     Baada ya Mussa kumshinda farao  akaondoka na wana wa Israel (wayahudi) akavuka nao katika bahari ya Shamu,Firauni naye alipojaribu kuvuka pamoja na jeshi lake aliangamizwa baharini.

      Baada ya mussa kuvuka salama na wana wa Israel mungu akawapa amri ya kufurahia kutoka utumwani na ndipo sikuku hiyo ya pasaka ilipoanzia hapo rejea katika kitabu cha kumbukumbu la torati 16:1-6)

“1 Utunzwe mwezi wa Abibu ukamfanyie pasaka Bwana mungu wako kwa kuwa ilikuwa mwezi wa Abibu alipokutoa misri usiku Bwana Mungu wako, 2 Nawe umchinjie pasaka Bwana Mungu wako katika kundi la kondoo na la ng’ombe mahali atakapochagua bwana apakalishe jina lake,3 Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu ,siku saba unakula naye mikate isiyotiwa chachu nayo ni mikate ya mateso kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka ili upate kukumbuka siku iliyotoka nchi ya Misri siku zote za maisha yako, 4 Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni kisilale chochote usiku kucha hata asubuhi,5 Usimchinjie pasaka ndani ya malango yako yote akupayo Bwana Mungu wako ,6 Ila mahali atakapochagua Bwana mungu wako apakalishe jina lake ndipo mtakapomchinjia pasaka jioni katika machweo ya jua kwa wakatika kama uliotoka misri”

    Baada ya kuangalia maandiko kutoka katika kitabu cha kumbukumbu la torati sasa tuangalie tena katika kitabu cha pili cha Nabii Musa kiitwacho “KUTOKA”

    Katika kitabu cha kutoka pia tunaona kuwa asili ya sikukuu ya pasaka ilianza kwa Nabii Mussa baada ya kutoka misri na wana wa Israel rejea Kutoka 12:42-51

“42 Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za Bwana kwasababu ya kawatoka katika nchi ya Misri ,huu ndio usiku wa bwana ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israel wote katika vizazi vyao, 43 Bwana akawaambia Mussa na Haruni Amri ya pasaka ni hii, mtu mgeni asimle 44 Lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha,ukiisha kutahiri ndipo hapo atamla pasaka.45 Akaaye kwenu hali ya ugeni na mtumishi aliyeajiliwa wasimle pasaka, 45 Akaaye kwenu hali ya ugeni na mtumishi aliyeajiliwa wasimle pasaka, 46 Na aliwe ndani ya nyumba moja ,usiichukue nje ya nyumba nyama yake yoyote wala msifunje mfupa wake uwao wote. 47 Na wafanye jambo hili mkutano wa Israel wote. 48 Na mgeni atakapoketi pamoja nawe na kupenda kumfanyia Bwana pasaka waume wake wote na watahiriwe ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka ,naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi lakini mtu yeyote asiyetahiriwa asimle. 49 Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini. 50 Ndivyo walivyofanya wana wa Israel wote kama Bwana alivyowaagiza Mussa na haruni ndivyo walivyofanya. 51 Ilikuwa siku ile ile moja,Bwana akawatoa wana wa Israel katika nchi ya Misri kwa majeshi yao”(KUTOKA 12:42-51)

    Kwa maelekezo hayo hapo juu kutoka katika kitabu cha tano cha Mussa kiitwacho “KUMBUKUMBU LA TORATI” na kitabu cha pili cha Mussa kiitwacho “KUTOKA” moja kwa moja tunaona kuwa pasaka ni sikukuu iliyoanza wakati wa Nabii Mussa baada ya kuamriwa na Mungu wake kusheherekea pasaka pamoja na wana wa Israel kwa kuchinja Kondoo na Ng’ombe baada ya Mussa kufanikiwa kuwatoa wana wa Israel kutoka katika mikono ya mateso ya mfalme Firauni(Farao),Hivyo kwa maneno hayo moja kwa moja tunaona kuwa sikukuu ya pasaka si  kufufuka bwana Yesu kama baadhi ya wakristo wanavyodai 

    Jambo la kushangaza na kustaajabisha ni kuona baadhi ya watu hususani jamii ya Wakristo wakidai kuwa pasaka ni sikukuu ya kufufuka kwa Yesu wakati kwa mujibu wa vitabu vyao wanavyoviamini na kuvitumia kila siku vinakanusha suala la pasaka kuwa ni sikukuu ya kufufuka Bwana yesu.

     Baada ya kuona maandiko hayo hebu tuangalie je kweli bwana yesu alikufa na kufufua na je wanaosheherekea pasaka kuwa ni sikukuu ya kufufuka yesu wako sahihi?

LUKA 2:41-45  “Basi wazee wake huenda yerusalemu kila mwaka wakati wa sikuku ya pasaka.Na alipopata umri wa miaka kumi na miwili walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuuu.Na walipokwisha kutimiza siku wakati wa kurudi kwao,Yule mtoto yesu alibaki nyuma huko yerusalemu na wazee wake walikuwa hawana habari.Na wakadhani ya kuwa yumo katika msafara wakaenenda mwendo wa kutwa wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao.Na walipomkosa wakarejea Yerusalemu huku wakimtafuta”

     Kwa maelezo hayo hapo juu tunaona kuwa hata yeye mwenyewe yesu alikula sikukuu ya pasaka wakati akiwa mdogo na umri wake ulikuwa ni miaka kumi na miwili akiwa na wazee wake ambao walikuwa wakienda Yerusalemu kama ilivyokuwa desturi yao.

     Swali la kujiuliza hapo je ni nani alikufa na kufufuka ikiwa Yesu mwenyewe alikula pasaka akiwa na umri wa miaka kumi na miwili je kusema kuwa sikukuu ya pasaka ni kufufuka kwa Yesu je huyo ni yesu gani?
    Ukweli ni kwamba kusheherekea sikukuu ya pasaka ni kupoteza mwelekeo kwani sikukuu hiyo ya pasaka ni sikukuu ya wayahudi.

    Ushahidi unaothibitisha kuwa pasaka ni sikukuu ya wayahudi ni YOHANA 6:4 “Na pasaka sikuku ya wayahudi ilikuwa karibu”

     Nihitimishe makala hii fupi ya UKWELI KUHUSU PASAKA kwa maneno ya kitabu kitukifi cha QUR’AN pale ambapo ALLAH S W aliposema katika sura ya 4:157-158

    “Na kwaajili ya kusema kwao sisi tumemuua Masihi Isa mwana wa Mariamu mtume wa mungu hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani Nabii Isa) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika hiyo(ya kumuua Isa)wako katika shaka nalo (jambo hilo la kusema kauawa)wao hawana yakini juu ya jambo hili isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumwua. Bali Mwenyezimungu alimnyanyua kwake na Mwenyezimungu ni mwenye nguvu na mwenye hikima.

      Kwa aya hiyo ndipo ambapo tunaona kuwa Nabii ISSA(a.s) au YESU hakufa wala hakusulubiwa ila walifananishiwa tu hao mayahudi waliotaka kumsulubu na kumuua bwana Yesu.

    Hivyo kusheherekea sikukuu ya pasaka ni kufuata mila za wayahudi na watu wasio na dini.

Kwa kifupi huo ndio ukweli kuhusu pasaka na historia yake ambapo tumeona kuwa pasaka ilianza kwa Nabii Mussa pale alipoambia na Mungu wake aende kwa Firauni(Farao) akawaokoe wana wa Israel kutokana na mateso waliyokuwa wanayapata kutoka kwa mfalme Firauni(Farao) lakini pia tumeona kuwa pasaka ni sikukuu ya iliyokuwa inasheherekewa na mayahudi wa kipindi hicho.

     Nakuacha na swali hili; Kusema kuwa pasaka ni siku ya kufufuka kwa Yesu je ni Yesu gani huyo aliyekufa na kufufuka wakati yeye mwenyewe amekula pasaka?

Makala hii imeandaliwa na 
Adinani  H chorobi 0753-733217

Wednesday, December 24, 2014

Historia Ya Krismasi Na Hukumu Ya Kusherehekea Na Kupongezana

 HISTORIA YA KRISMAS

Wakati wa zama za kale, siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za Kusini kulisherehekewa mfano wa usiku ambao mungu wa Mama Watakatifu alijifungua mtoto akijulikana kuwa ni mungu wa Jua. Pia (siku hii) inaitwa Yule, siku ambayo inasherehekewa mno kwa kurushwa pashpashi. Ambapo kila mtu atacheza na kuimba ili kuliamsha jua kutokana na usingizi wake mnono wa majira ya baridi.
Wakati wa Warumi, iliadhimishwa kwa kumsifu Satunusi (mungu wa mavuno) na Mithrasi (mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia jua ambao umekuja ukitokea Syria hadi Urumi. Karne kabla ya madhehebu ya Sol Invictus, ilitangaza ya kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele, na kwamba maisha yanasonga mbele, na ni mualiko wa kubaki kwenye nguvu nzuri.
Siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za mviringo za Kusini ni baina ya siku ya 20 au 22 Disemba. Warumi waliadhimisha Saturnalia baina ya tarehe 17 na 24 Disemba.

Wakristo wa kale
Ili kuepuka kuchunguzwa wakati wa sherehe ambazo ni za wapagani, Wakristo wa kale walikaa majumbani mwao pamoja na mtakatifu Saturnalia. Kwa vile idadi ya Wakristo iliongezeka na mila zao zikaenea, sherehe zikachukua shuruti za Kikristo. Lakini, Makanisa ya kale hakika hayakusherehekea mwezi wa Disemba kwa kuzaliwa Kristo hadi alipokuja Telesforusi Telesphorus, ambaye alikuwa askofu wa pili wa Roma kutoka mwaka 125 hadi 136 M, askofu huyo ndiye aliyetangaza kwamba huduma za Kanisa zifanywe wakati huu ili kuadhimisha “Kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mwokozi”. Hata hivyo, kwa vile hakuna mtu hata mmoja aliye na uhakika wa mwezi ambao amezaliwa Kristo, kawaida ya Uzawa ulikumbukwa Septemba, ambao ulikuwa ni wakati wa Sherehe za Kiyahudi za Trumpetsi (kwa sasa ni Rosh Hashanah). Ukweli ni kuwa, kwa zaidi ya miaka 300, watu walielewa kuzaliwa kwa Yesu katika tarehe tofauti.
Katika mwaka 274 M, kikomo cha jua kiliangukia tarehe 25 Disemba. Mfalme wa Roma aitwaye Aurelian alitangaza tarehe hiyo kama ni “Natalis Solis Invicti”, ‘Sherehe Ya Kuzaliwa Jua Lisiloshindikana’. Katika mwaka 320 M, Papa Julius I aliitangaza tarehe 25 Disemba kama ni tarehe rasmi ya kuzaliwa Yesu Kristo.
Mnamo mwaka 325 M, Krismasi ilitangazwa rasmi, lakini kiujumla haikutiliwa maanani. Mtakatifu Constantine, ambaye ni Mfalme wa mwanzo wa dhehebu la Ukristo la Kirumi, aliitanguliza Krismasi kama ni sherehe isiohamishika kwa tarehe 25 Disemba. Pia aliitanguliza Jumapili kama ni siku kuu ndani ya siku saba za wiki, na aliitanguliza (Pasaka) kama ni sherehe yenye kuhamishika. Mnamo mwaka 354 M, Askofu Liberius wa Rumi, alitoa amri rasmi kwa wafuasi wake kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu ndani ya tarehe 25 Disemba.
Hata hivyo, ingawa Constantine aliifanya rasmi tarehe 25 Disemba kama ni sherehe ya kuzaliwa Kristo, Wakristo wakiitambua kama ni tarehe ya sherehe iliyofanana na mapagani, hawakushiriki katika mambo mazuri (kwa siku hii) iliyopangwa na Askofu. Krismasi ilishindwa kupata utambulisho wa kilimwengu miongoni mwa Wakristo hadi kipindi cha hivi karibuni. Huko Uingereza England, Oliver Cromwell alizipiga marufuku sherehe za Krismasi baina ya miaka 1649 na 1660 kupitia kwa inayoitwa Sheria za Rangi Samawati Blue Laws, akiamini kwamba iwe ni siku ya kumuabudu mungu tu.
Hamu ya kuifurahia sherehe ya Krismasi ilikirimiwa pale Waprotestanto (Wakristo wasiokubali baadhi ya mafundisho ya Kanisa la Kirumi) walipokimbia uchunguzi kwa kutorokea sehemu za makoloni yote duniani. Hata hivyo, Krismasi bado haikuwa ni sikukuu halali hadi miaka ya 1800. Na, weka akilini, hakukuwa na picha ya Baba Krismasi (Santa Claus) kwa wakati huo.

Krismasi inaanza kuwa maarufu
Umaarufu wa Krismasi ulianza ghafla mnamo mwaka 1820 kutokana na kitabu cha Washington Irving The Keeping of Christmas at Bracebridge Hall ‘Kuiadhimisha Krismasi Kwenye Jukwaa La Bracebridge’. Mnamo mwaka 1834, Malkia wa Uingereza aitwaye Victoria, alimkaribisha mumewe wa Kijerumani Prince Albert ndani ya Ngome ya Windso Windsor Castle, akimuonesha tamaduni za mti wa Krismasi Christmas tree na Nyimbo Za Kumsifu Yesu Kristo carols ambazo ziliadhimishwa Uingereza kwa Mfalme wa Uingereza. Mwaka 1834, wiki moja kabla ya Krismasi, Charles Dickens alichapisha Nyimbo za Kumsifu Yesu za Krismasi Christmas Carols (ambapo aliandika kwamba Scrooge alimuamrisha Cratchit kufanya kazi, na kwamba Baraza Kuu la Marekani US Congress lilikutana Siku ya Krismasi). Ilikuja kuwa ni maarufu mno hadi kufikia kwamba sio makanisa wala serikali kukana umuhimu wa sherehe za Krismasi. Mnamo mwaka 1836, Alabama ilikuja kuwa ni taifa la mwanzo ndani ya Marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mnamo mwaka 1860, mfananishi illustrator wa Marekani aitwaye Thomas Nast alichukua kutoka hadithi za Kiingereza kuhusu Mtakatifu Nicholas, muangalizi mtakatifu wa watoto, kumtengeneza Baba Krismasi Father Christmas. Mwaka 1907, Oklahoma ilikuwa ni ya mwisho miongoni mwa mataifa ya Marekani kutangaza Krismasi kama ni sikukuu halali. Mwaka baada ya mwaka, nchi za dunia nzima zilianza kuitambua Krismasi kama ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu.

Nakuombea Krismasi Njema Have a merry Christmas
Leo, mambo mengi yasiyokuwa ya Kikristo yananasibishwa ndani ya Krismasi. Yesu alizaliwa mwezi wa Machi, bado siku yake ya kuzaliwa inasherehekewa Disemba ya 25, wakati wa solstice. Sherehe za Krismasi zinamalizikia siku kumi na mbili za Krismasi (Disemba 25 hadi Januari 6), ni idadi hiyo hiyo ya siku ambazo zilisherehekewa na wapagani wa ki-Rumi wakale kwa kuadhimisha kurudi kwa jua. Hivyo, hakuna mshangano wowote kwamba Wakristo waliosafi puritans – au Wakristo wasiotaka mabadiliko conservative – watahamaki kwa Krismasi kuwa “sio ya kidini kama ilivyotakikana kuwa,” wakisahau kwamba Krismasi haikusherehekewa hata kidogo hadi siku za hivi karibuni.


Yesu Alisemaje Kuhusu Krismasi?


Mazoea ya Krismasi

Mti ulio bora wa Krismasi unanunuliwa. Ukipambwa kwa madoido yenye kung’ara pamoja na kumetameta, unasimamishwa karibu na dirisha. Maduka yanajazana wanunuzi wakisaka zawadi na vile viduchu vinasubiri kwa hamu kubwa ya Baba Krismasi Santa.
Ni mshughuliko na ni homa ya Krismasi Christmas fever, umewahi kufikiri kabla? Je, Biblia au Yesu aliwahipo kusababisha homa ya Krismasi?
Tafakari juu ya mchanganuo ufuatao kuhusu Krismasi, na ukweli utakuja kuwa wazi zaidi na zaidi.

Je, Krismasi Ina Ushahidi wa Biblia?

Neno ‘Krismasi’ halipo ndani ya Biblia. Biblia ilifunga midomo ya sherehe yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kitu kimoja; upambaji wa mti. Biblia wenyewe inashutumu upambaji wa miti (ya Krismasi):
“Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu, wanaugandanisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika” (Jeremia 10-3,4).
Wazungu wa ki-Pagani kabla ya Ukristo, waliamini miujiza kwamba miti ya kijani ina nguvu maalum za ulinzi. Hakika, matumizi ya Miti ya Krismasi imeanza hivi karibuni tu mwa karne ya 17 huko Strasbourg, Ufaransa na kutoka huko ukaenea hadi Ujerumani, Uingereza na baadaye Marekani. “Ibada ya miti ilikuwa ni jambo la kawaida kwa dini miongoni mwa watu wa Tyutoniki Teutonic na Skandinavia Scandinavia wa Ulaya ya kaskazini kabla ya kuingia kwenye Ukristo…Walowezi wa ki-Jerumani walileta mila za Mti wa Krismasi kwenye makoloni ya Kimarekani mnamo karne ya 17. Kufikia karne ya 19, matumizi yake yalienea sehemu tofauti”. (Angalia Encyclopedia ya Compton, Toleo la 1998)

Je, Yesu Alizaliwa Disemba ya 25?
Si tarehe ya Disemba 25 wala tarehe nyengine yoyote iliyotajwa ndani ya Biblia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Ilikuwa ni hivyo hadi kufikia mwaka 530 C.E kwamba mtawa monk aitwaye Dionysus Exigus, aliweka tarehe isiyobadilika ya kuzaliwa kwa Yesu kuwa ni Disemba 25. “Kulingana na taratibu za ki-Roma, alikosea kuipanga tarehe ya kuzaliwa kwa Kristo (yaani, miaka 754 baada ya kupatikana nchi ya Rumi) kama ni Disemba 25, mwaka 753”. (Angalia: Encyclopedia Britannica, toleo la mwaka 1998) Tarehe hii ilichaguliwa ili iendane pamoja na sikukuu ambazo zimeshagandana na imani za kipagani.
Mapagani wa Kirumi walisherehekea Disemba 25 kama ni ya kuzaliwa kwa ‘mungu’ wao wa nuru, aitwaye Mithra.
“Mnamo karne ya pili M, hiyo sherehe ya Mithra ilikuwa ni ya kawaida zaidi ndani ya Ufalme wa Rumi kuliko Ukristo, ambayo ilizaa mifanano iliyo mingi” (The Concise Columbia Encyclopedia, toleo la mwaka 1995).
‘Waungu’ wengine wakipagani waliozaliwa Disemba ya 25 ni: Hercules mtoto wa Zeuz (Wagiriki); Bacchus, ‘mungu’ wa mvinyo (Warumi); Adonis, ‘mungu’ wa Kigiriki, na ‘mungu’ Freyr wa Ugiriki-mapagani wa Roma.


Je, Vipi Kuhusu Baba Krismasi Santa Claus?

Kama viumbe visivyokuwa binaadamu aliens watafika duniani katika wakati wa Krismasi, bila ya shaka wataamini Krismasi kuwa ni sherehe ya kufurahikia kuzaliwa kwa Baba Krismasi Santa. Majina ya ‘Santa Claus’, hayamo popote ndani ya Biblia.
Hata hivyo, Mtakatifu Nikolas Saint Nicholas (Baba Krismasi Santa Claus) alikuwa ni mtu halisi, askofu, ambaye alizaliwa miaka 300 baada ya Yesu. Kwa mujibu wa hekaya za kale, alikuwa ni mtu mwenye huruma mno na alitenga nyakati za usiku kwenda kutoa zawadi kwa mafukara. Baada ya kifo chake mnamo Disemba ya 6, watoto wa shule huko Ulaya walianza kusherehekea siku hiyo kwa karamu kila mwaka.
Baadaye Malkia Victoria aliibadilisha sherehe hiyo kutoka Disemba ya 6 kuwa ni Disemba ya 24 kuamkia Krismasi.


Je, Yesu au Wafuasi Wake Waliwahi Kusherehekea Krismasi?

Kama Yesu alimaanisha kwa wafuasi wake kusherehekea Krismasi, angeliifanyia kazi yeye mwenyewe na kujikusanya pamoja na wafuasi wake. Hakuna sehemu iliyotajwa ndani ya Biblia kwamba kuna mfuasi yeyote aliyewahi kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kama Wakristo wanavyofanya leo.
“Kanisa halikupatapo kuweka sikukuu kwa ajili ya sherehe za tukio la Krismasi hadi ilipofika karne ya 4” (Angalia: Encyclopedia ya Grolier)
Hivyo, tunaona kwamba sio Biblia wala Yesu na wafuasi wake waliosema kitu kuhusu sherehe za Krismasi ambazo sasa zinahusisha viingilio vya sherehe, biashara, na matumizi yaliyochupa mpaka, ni utovu wa akili kwa mfananisho wowote wa imani.


Hukumu Ya Krismasi Na Mwaka Mpya

Shukrani Ziende kwa Allaah
Shaykh al-Islaam bin Taymiyah (Allaah Amrehemu) alisema kwenye fafanuzi yake katika Aayah (tafsiri ya maana):
{{Na wale ambao hawashuhudii shahada za uongo (az-zuur)…}} [Al-Furqaan 25: 72].
Ama kuhusu sherehe za mushrikiyn: wanakusanya pamoja mambo yenye kutia wasiwa.si, mahitaji ya mwili na uongo, hakuna chochote ndani yake ambacho kina faida ya kidini, na mwisho wa kutosheleza hizo shahawa, ni maumivu. Hivyo, vitendo vyao ni vya uongo, na kuvishuhudia kunamaanisha kuvifanya. Hii Aayah peke yake inawapandisha daraja na kuwapa moyo (wale ambao hawashuhudii uongo), ambayo ina maana ya kuwahimiza watu kuachana na kushiriki kwenye sherehe zao (mushrikuun) na aina nyenginezo za uongo. Tunafahamu kwamba ni vibaya kushiriki kwenye sherehe zao kwa sababu wanaitwa az-zuur (waongo). Inamaanisha kwamba ni haraam kufanya hivi kwa sababu zilizo nyingi, kwa sababu Allaah Ameiita ni az-zuur.
Allaah Anamlaumu yule anayezungumza uongo (az-zuur) hata ikiwa hamna yeyote atakaeathirika nao, kama ilivyo ndani ya Aayah ikikataza Dhwihaar (aina ya talaka ambapo mume anamwambia mkewe “Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu”), ambapo Yeye Anasema (tafsiri ya maana):
{{…Wanasema neno baya na la uongo (zuuran)…}} [Al-Mujaadalah 58: 2].
Na Allaah Anasema (tafsiri ya maana):
{{…basi jiepusheni na uchafu wa masanamu na jiepusheni na usemi wa uongo.}} [Al-Hajj 22:30].
Hivyo yule ambaye anafanya az-zuur analaumiwa kwa mtindo huu. Ndani ya Sunnah:
Anas bin Maalik (Allaah Amrehemu) amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja (Madiynah) na walikuta siku mbili ambazo kipindi cha Jaahiliyyah watacheza (na kujipumzisha).” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Allaah Amekupeni kilicho bora zaidi kuliko mambo hayo: Yawm adh-Dhuhaa (‘Iyd al-adh haa) na Yawm al-Fitr (‘Iyd al-Fitr).” [Imesimuliwa na Abuu Daawuud].
Hii inaonesha wazi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya shaka alizuia Ummah wake kusherehekea sherehe za kikafiri, na alihakikisha kuziondosha kwa njia zozote zinazowezekana.
Ukweli wa kwamba dini ya Watu wa Kitabu inakubaliwa, haina maana kwamba sherehe zao zinakubalika au ziendelezwe na Ummah, kama yalivyo matendo yao mengine ya kikafiri yasivyokubalika, na dhambi zao pia hazikubaliki. Hakika, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifikia hadi kuamrisha Ummah wake kujitofautisha nao kwenye mambo mengi ambayo ni mubaah (yanaruhusiwa) na kwa taratibu nyingi za ibada, kwa sababu tu; kwamba vinapelekea kuwa sawa nao kwenye mambo mengine pia. Hii kuweka tofauti; ni kuonesha kizuizi katika nyanja zote, kwa sababu namna utakavyokuwa tofauti na watu wa Motoni, ndivyo utakavyokuwa mchache wa kutenda matendo ya watu wa Motoni.
Ushahidi wa mwanzo ni Hadiyth ya: “Kila watu wana sherehe zao, na hii ndio sherehe yetu” ambayo ina kusudio maalum kwamba; watu wote wana sherehe zao wenyewe, kama Allaah Anavyosema (tafsiri ya maana):
{{Na kila ummah ulikuwa na Qiblah walichokielekea…}} [Al-Baqarah 2: 148]
na
{{Na kila (ummah) katika nyinyi (bin Aadam) Tumeujaalia shari'ah yake na njia yake.}} [Al-Maaidah 5: 48].
Hii inamaanisha kwamba kila taifa lina njia zake wenyewe. Hiyo laam ndani ya li-kulli (“kwa kila”, “katika nyinyi”) ina maana kwa watu maalum. Hivyo, kama Mayahudi wana sherehe na Wakristo wana sherehe, ni za kwao wenyewe, na sisi hatuna sehemu yetu ndani ya hizo sherehe, kama vile tusivyotumia Qiblah kimoja au sheria zao.
Ushahidi wa pili ni: masharti aliyoweka ‘Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kukubaliana pamoja na Swahaabah na Fuqaaha wote baada yao ni: kwa wale Watu wa Kitabu ambao wamekubali kuishi chini ya hukumu za Kiislamu (ahl adh-dhimmah) wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ndani ya Daar al-Islaam (ardhi zilizo chini ya hukumu za Kiislamu). Kama Waislamu wamekubaliana kuwazuia ahl adh-dhimmah kusherehekea wazi wazi, ni namna gani itakuwa sahihi kwa Waislamu kushereheka nao wazi wazi? Kama Muislamu atawasherehekea, jee sio zaidi ya kafiri anavyofanya wazi wazi?
Sababu iliyokuwepo ya sisi kuwazuia wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ni kwa sababu ya machafu yaliyokuwemo humo. Kwa sababu ya dhambi au alama ya dhambi. Katika kesi yoyote, Muislamu anazuiwa kutenda dhambi au kujaribu kutenda dhambi. Hata kama hakuna uadui wowote kwa Muislamu kuwa nao pamoja katika kusherehekea wazi wazi isipokuwa kafiri kupata nguvu ya kuendelea na matendo yake. Inakuwaje Muislamu anatenda hivyo? Uadui uliokuwemo (ndani ya sherehe zao) utaelezwa chini, insha Allaah.
Al-Bayhaqiy amesimulia ikiwa na isnaad swahiyh kwenye Baab karaahiyat ad-dukhuul ‘ala ahl adh-dhimmah fi kanaa’isihim wat-tashabbuh bihim yawmi nawruuzihim wa maharjaanihim (Sura kuhusu karaha ya kuingia kwenye makanisa ya ahl adh-Dhimmah (Makafiri walio katika nchi ya Kiislam)  katika kuadhimisha Mwaka wao Mpya na sherehe nyengine): Kutokana na Sufyaan ath-Thawri na kutokana na Thawr bin Yaziyd na kutokana na ‘Atwa’ bin Diynaar ambao wamesema: ‘Umar amesema: “Musijifunze lugha ya wasiokuwa Waarabu, musiingie pamoja na mushrikiyn kwenye makanisa yao katika siku za karamu zao, kwani laana (za Allaah) zinawashukia juu yao.”
‘Umar bin al-Khattwaab amesema:
“Jiepusheni na maadui wa Allaah kwenye sherehe zao.” Imesimuliwa kutokana na Abuu Usaamah ikiwa na isnaad iliyo sahihi kwamba: ‘Awn alituambia kutokana na Mughiyrah kutokana na ‘Abdullaah bin ‘Amr: “Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.” ‘Umar alikataza kujifunza lugha zao, na hata kuingia kwenye makanisa yao katika siku ya sherehe yao, jee ni vipi kwa kufanya baadhi ya mambo wanayoyafanya kwenye siku hizo, au kufanya vitu ambavyo ni sehemu ya dini yao? Je, sio kufanya baadhi ya vitu wanavyofanya kwenye sherehe zao ni (uovu) zaidi ya kuingia tu kwenye sherehe zao? Kama laana za Muumba zitaanguka juu yao kwenye siku ya sherehe yao kwa sababu ya yale wanayofanya, je, adhabu hiyo haitokuwa sawa kwa yule anayefanya yale wanayotenda wao, au sehemu ya hayo? Je, sio maneno ya: “Jiepusheni na maadui wa Allaah, kwenye sherehe zao” yana maana kwamba tusikutane nao au kushirikiana nao kwenye siku hizi? Je, ni vipi kwa mtu ambaye hakika anasherehekea sherehe zao?
‘Abdullaah bin ‘Amr amesema kwa uwazi:
“Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.”
Hii inamaanisha kwamba yule anayejikusanya nao kwenye mambo yote haya ni kafiri, au kwamba kufanya hivi ni miongoni mwa dhambi kubwa (kabaa’ir) kwamba itampelekea mmoja wao Motoni; maana ya iliyopita ni ile iliyo wazi kutokana na mpangilio wa maneno. Alitaja – Na Allaah Ndie Ajuaye Zaidi – yule anayeishi kwenye ardhi yao, kwa sababu wakati wa ‘Abdullaah bin ‘Amr na Swahaabah wengineo, walikuwa wakizuia sherehe zilizo wazi za kikafiri ndani ya ardhi za Waislamu. Na hakuna Muislamu aliyewaiga kwenye sherehe zao; hilo (la kusherehekea) pale ambapo wanapoishi kwenye ardhi za kikafiri. ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikataa hata kulitambua jina la sherehe zao ambazo zilikuwa mahsusi kwa ajili yao, je, itakuwaje kwa kushereheka nao kisawasawa? Ahmad ametaja maana ya simulizi zilizopokelewa kutokana na ‘Umar na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwenye mada hii, na wafuasi wake walijadili masuala ya sherehe.
Imaam Abul-Hassan al-‘Aamidiy alisema: mwandishi anayejulikana kwa jina la Ibn al-Baghdaadi alisema ndani ya kitabu chake Umdat al-Haadhwir wa Kifaayat al-Musaafir: “Hairuhusiwi kuingia kwenye sherehe za Wakristo na Mayahudi.” Ahmad alitamka hili kwenye simulizi ya Muhannaa, na ushahidi wake wa hilo ni Aayah (tafsiri ya maana):
{{Na wale ambao hawashuhudii shahada za uongo (az-zuur)…}} [Al-Furqaan 25: 72].
Alisema: (Hizi sherehe ni) ash-Sha’aaniyn pamoja na sherehe zao. Alisema: Waislamu wazuiliwe kuingia kwenye masinagogi (makanisa ya Kiyahudi) na makanisa (ya Wakristo).”
Kutokana na Iqtidhwa’ as-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab al-Jahiym iliyoandikwa na Shaykh al-Islaam bin Taymiyah, uk. 183.
Kuwatakia kheri ya Krismasi Makafiri na hata sikukuu nyengine za dini tofauti ni haraam kwa mujibu wa makubaliano ya wengi, kama Ibn al-Qayyim (Allaah Amrehemu) alisema kwenye Ahkaam Ahl adh-Dhimmah.
Kuwatakia kheri Makafiri katika mwenendo ambao ni kwa ajili yao ni haraam kwa makubaliano ya wengi, kama ilivyo haraam kuwatakia kheri katika sherehe zao na funga zao kwa kusema ‘Kila la kheri katika sherehe’ au ‘Nakutakia sherehe njema’, na mengineyo. Hata kama yule anayesema haya ameepushwa na ukafiri, lakini bado imekatazwa. Ni kama vile kumpa hongera mtu kwa kuuhami msalaba, au zaidi ya hivyo. Ni kama mfano wa dhambi iliyo kubwa sawa na kumpa hongera mnywaji ulevi, au kumuua mtu, au kuwa na mahusiano ya kinyama, na mengineyo. Wengi miongoni mwa wasio na heshima ya dini yao wanaangukia kwenye kosa hili; hawakai kufikiria ubaya wa vitendo vyao. Yeyote anayempa hongera mtu kwa kutovukwa na adabu au bid’ah au ukafiri amejiweka wazi na laana pamoja na ghadhabu za Allaah.”

Kuwapatia hongera makafiri kwenye sherehe za kidini ni haraam kama alivyokwenda mbali Ibn al-Qayyim kwa kufananisha na kwamba yule anayetoa salamu hizo amekubali au ameidhinisha matendo yao ya kikafiri, hata kama mtu hatovifanya mwenyewe vitu hivyo. Lakini Muislamu asikubali mienendo ya kikafiri wala kumpa hongera yeyote kwa ajili yao, kwa sababu Allaah hakubali matendo yoyote kati ya hayo, kama Alivyosema (tafsiri ya maana):

{{Mkikufuru, basi Allaah hana haja nanyi; lakini Haridhii kufuru kwa waja Wake; na kama mkishukuru; hayo Yanamridhisha kwenu.}} [Az-Zumar 39:7].

{{…Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu…}} [Al-Maaidah 5:3].

Hivyo kuwapa pongezi kunazuiwa, hata ikiwa ni mwenzio kazini au vyenginevyo. Kama wao watatutakia kheri kwa kuadhimisha sherehe zao, hatutakiwi kujibu, kwasababu hizi sio sherehe zetu, na kwasababu sio sherehe ambazo zinakubalika na Allaah. Sherehe hizi ni uzushi ndani ya dini zao, na hata zile ambazo zimetajwa huko kabla zimetenguliwa na dini ya Kiislamu, ambayo Ameileta Allaah kwa wanaadamu wetu kupitia kwa bwana Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah Anasema (tafsiri ya maana):

{{Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Aakhirah atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa)}} [Aaali-‘Imraan 3:85].

Ni haraam kwa Muislamu kukubali mialiko katika sherehe kama hizo, kwa sababu ni zaidi ya kuwatakia kheri kama inavyoonesha kushiriki katika sherehe zao. Vile vile, Waislamu wanazuiwa kuwaiga makafiri katika kuadhimisha huko kwa kushiriki kwenye tafrija parties, au kwa kubadilishana zawadi, au kutoa peremende au chakula, au kuacha kufanya kazi, n.k. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema “Yeyote anayewaiga watu ni mmoja wao.”

Shaykh al-Islaam bin Taymiyah amesema ndani ya kitabu chake Iqtidhwaa’ asw-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab Al-Jahiym:
“Kuwaiga katika baadhi ya sherehe zao inamaanisha kwamba mtu amefurahia imani zao za uongo na vitendo vyao, na anawapa matumaini kwamba wanaweza kuwa na nafasi ya kuwanyanyasa na kuwapeleka ovyo wanyonge.” Yeyote anayefanya mambo kama haya ni mtenda dhambi, ikiwa anafanya kwa ukarimu au urafiki, au kwa sababu anaona hayaa kukataa, au kwa sababu nyengine yoyote. Kwa sababu ni unafiki ndani ya Uislamu, na kwa sababu inawafanya makafiri kujisikia fakhari kwa dini yao.

Allaah Pekee ndiye tunayemuomba kuwafanya Waislamu kuwa fakhari na dini yao, kuwasaidia kuwa thaabiti katika kushikamana na dini yao, na kuwafanya kuwa washindi dhidi ya maadui zao, kwani Yeye Mwenye Nguvu ndiye Mwenye Kuweza.

Monday, September 8, 2014

JUMUIYA YA ZAKA NA SADAKA ZNZ (JUZASA) YAFANYA MKUTANO WA MAENDELEO YA JUMUIYA HIYO

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh Said Suleiman Masoud Mwenyekoti Jeusi akitoa nasaha zake kwa Wanachama na Waalikwa katika Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Shamtimba Kiembesamaki Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh Said Suleiman Masoud Mwenyekoti Jeusi akitoa nasaha zake kwa Wanachama na Waalikwa katika Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Shamtimba Kiembesamaki Zanzibar.

ZANZIBAR

Kukosekana kwa Utaratibu nzuri wa Utoaji na Usambazaji wa Zaka ni moja ya matatizo yanayopelekea Zanzibar kuendelea kuwa na Watu wanaoishi katika mazingira magumu na Umasikini uliopindukia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh Said Suleiman Masoud ameyasema hayo alipokuwa akitoa nasaha katika Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Shamtimba Kiembesamaki Zanzibar.
Amesema Zanzibar kuna watu Wenye nafasi nzuri kiuchumi lakini  wanashindwa kutoa Zaka katika utaratibu Unaofaa na hivyo kushindwa kuwafikia Walengwa wenye Mahitaji.
Amesema Watu hao wenye uwezo wangekuwa wanatoa Zaka na kusambazwa katika utaratibu unaofaa, Zanzibar ingekuwa haina Watu Masikini kutokana na Zaka hizo kuwakomboa katika kiuchumi.
Shekh Said amesema wameamua kuanzisha Jumuiya ya (JUZASA) ili kurahisisha Upatikanaji na Usambazaji wa Zaka baada ya kukosekana jambo hili kwa miaka mingi.
Ameongeza kuwa kwa muda mrefu Zanzibar kumeundwa Taasisi nyingi za Serikali na za kibinafsi kwa ajili ya kumkomboa Mwananchi na Umasikini lakini malengo yanashindwa kutimia kutokana na kukosekana Elimu ya Utoaji wa Zaka.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya JUZASA Omar Abubakar ameelezea Malengo ya Zaka kuwa ni pamoja na Kuitakasa Mali ya Mtoaji na kumkomboa Muislamu kutokana na Janga la Njaa.
Ametoa wito kwa Waisalmu kujitokeza kuwaunga Mkono sambamba na kupeleka Zaka zao katika Jumuiya yao ili Waziwasilishe kwa walengwa wanaofaa kupewa Zaka katika jamii.
Katika Mkutano huo Jumuiya hiyo imefanya Uchaguzi ambapo Mwenyekiti wake na Katibu wake wamechaguliwa tena kuiongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Jumuiya hiyo iliyopata Usajili mwaka 2011 inapokea na kusambaza Zaka kwa walengwa,ambapo malengo yake makuu ni kutekeleza vyema Suala la Zaka ili kuweza kuwasaidia Wanajimii wanaoishi katika mazingira magumu na umasikini uliokithiri.
 

MBUNGE MGIMWA APANIA KUKAMILISHA UJENZI WA MAABARA YA SAYANSI KIDAMALI SEKONDARI

KATIKA  kile  kinachoonyesha ni  kuunga mkono maagizo ya  Rais Dr Jakaya  Kikwete  katika  uanzishaji  ujenzi  wa  maabara za  sayansi  katika  shule  za sekondari  nchini ,mbunge wa  jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa ameahidi  kuchangia   kushirikiana na  shule ya sekondari Kidamali na   shule  nyingine  jimboni  humo ambazo  zitaanzisha ujenzi wa maabara.
 
Akizungumza katika harambee ya  kuchangia  ujenzi  wa maabara  katika  shule ya Sekondari Kidamali ,mbunge Mgimwa  alisema  kuwa  mbali ya kuupongeza uongozi wa  shule  hiyo kwa  kuja na  wazo la  kujenga maabara  kwa upande wake kama mbunge atakuwa  bega kwa bega na  wananchi wake  katika  ujenzi wa maabara katika  shule za  sekondari kama  ni  sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dr Kikwete .
 
” Kazi  mnayoifanya ni kubwa na inapaswa  kuungwa mkono na kila mdau  wa maendeleo katika  jimbo la Kalenga  kwani  kati ya  maagizo ya  Rais mheshimiwa Dr  Jakaya mrisho  Kikwete ni Halmashauri za  wilaya na mikoa  kuanzisha  ujenzi wa maabara za  sayansi  katika  shule zake  za  sekondari …..hivyo  mimi kama  mbunge  wenu  nimefurahishwa  sana na jitihada  hizi” alisema mbunge Mgimwa 
 
Kuwa  iwapo  shule  zote za  sekondari katika  jimbo la Kalenga zikaanza  mkakati wa ujenzi  wa  maabara  za  sayansi  ari ya  wanafunzi  kupenda masomo  ya  sayansi  itakuwa  juu zaidi na  kuwa kazi yake kama  mbunge ni  kuona anaendelea   kuunga mkono shule  zote zitakazoanzisha  ujenzi wa maabara  hizo.
 
Alisema  kuwa mbali ya  kuwa  elimu katika  jimbo lake la  Kalenga  inaendelea  vema ila bado  kuna haja ya  shule  zote za  sekondari katika jimbo  hilo  kuwa na maabara ya masomo ya  Sayansi .
 
” Maendeleo  ambayo mmeanzisha  ni makubwa  sana na  mimi kama  mbunge  najivunia  kuona  shule  inaanzisha  mpango  huu na  zaidi nampongeza  sana mkuu wa  shule ambaye amekuja na  wazo   hilo na mdau mkubwa wa maendeleo kata ya   Nzihi mkulima  George  Filiakosi aliyejitolea  kuandaa  chakula  ili  watu  wafike  kuchangia ujenzi  huo …..mimi kama  mbunge nitawachangia milioni  1  pamoja na  kujitolea  bati  zote  za  kuezekea  jengo  hilo  pindi  litakapo malizika “
 
Mbali ya  mbunge  huyo kujitolea  kwa  upande wake  mkuu  wa  shule  hiyo  Sixtus Kanyama  aliwapongeza  wadau  mbali mbali hasa   George Filiakosi kwa  kuendelea  kujitoa  kwa ajili ya  ujenzi wa maabara  hiyo huku akiwaomba  wadau  wengine  waliopo nje ya  jimbo la Kalenga  kuunga mkono  jitihada za mbunge  wao kwa kujitokeza kuchangia ujenzi huo .
 
Mkuu  huyo wa  shule alisema  kuwa  ili kukamilisha  ujenzi wa maabara   hiyo ya kisasa  jumla ya zaidi ya Tsh  milioni 200 zinahitajika na  kuwa  kwa  wale ambao  watakuwa tayari  kuunga mkono  ujenzi huo  wanaweza  kuchangia kwa kupitia  akaundi  ya shule  Kidamali sec School namba 6051100149 benki ya NMB ama kwa jina ya M- Pesa kwa namba  ya  mkuu wa shule  0752 507519
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya  wilaya ya  Iringa na  diwani  wa kata ya Nzihi Stephen Mhapa alisema  kuwa   wapo  baadhi ya  wananchi  wa kata  hiyo ambao  mbali ya  kualikwa  kufika kuchangia ujenzi huo  ila hawakuweza  kufika jambo ambalo alisema halipaswi kuendelea  kwani  kufanya  hizo ni  kurudisha  nyuma maendeleo ya ujenzi huo na maendeleo mengine kwa ujumla  wake.

Kigwangala ajitosa rasmi urais 2015

Awaponda wanaosubiri kuoteshwa .Mtoto wa Malecela amuunga mkono
 MBUNGE wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangala, amejitosa rasmi katika mbio za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwaka 2015.
Tangazo hilo la Kigwangala, linaongeza idadi ya wanaowania kiti hicho baada ya January Makamba, Bernard Membe, Edward Lowassa,William Ngeleja, Frederick Sumaye na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutangaza nia na baadhi yao kutajwa kuwa na nia ya kufanya hivyo mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari, wazazi wake, familia yake na makada wa CCM, akiwemo William Malecela (Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani John Malecela), Dk. Kigwangala alitumia muda mrefu kufafanua hotuba yake iliyokuwa na kurasa sita akielekeza kuwa, watanzania wanapaswa kubadili mipangilio ya kipaumbele na kusimiamia mambo wanayoyasema ili kujikwamua kiuchumi.
Kigwangala aliwaambia waandishi kuwa, anatangaza rasmi sasa, kuwa anatia nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015.
Alisema amefikia uamuzi huo bila kuelekezwa, kusukumwa, kushawishiwa, kupangiwa ama kupanga na mtu ama na kikundi cha watu, isipokuwa utashi utayari wake.
Bila kuwataja majina, Kigwangala aliponda njia wanazotumia wengine akisema kuwa yeye hasubiri kuoteshwa, kushauriwa au kuombwa kama wanavyofanya wagombea wengine kupitia CCM. Alisema baadhi ya wanasiasa wa CCM, wamekuwa waoga kujitosa au kutangaza nia zao bali husema kuwa wanasubiri kuoteshwa, au wengine wameombwa na watu wengine.
Alibainisha kuwa, anatangaza nia ya kugombea urais mapema ili kuwapa fursa watanzania wampime na kumtazama mwenendo na uwezo wake, akiamini kuwa ataungwa mkono si kwa rangi ya ngozi yake, si kwa jinsi yake, si kwa umri wake au kwa daraja lake kijamii, dini, ama kabila lake, bali kwa sifa na uwezo wake kama mtanzania.
Kigwangala alitumia msemo wa kilatini kusema kuwa yeye ni  baina ya wengi, mmoja! (E Pluribus unum), hivyo hawezi kuwa salama ikiwa wengine wanateseka.
Bila kutaja wazi kuwa anakosoa utendaji wa serikali ya Kikwete, Kigawangala alitoa mifano mbalimbali ikiwemo kitisho cha njaa, kucheleweshwa hukumu za mahakamani, shida za mzee mmoja wa Pemba aliyefiwa na mtoto wake, au kasoro za operesheni za wamachinga na mamantilie jijini Dar es Salaam.
Kitisho cha njaa ya familia fulani maskini kule Sakasaka, wilayani Meatu, ni kitisho changu na familia yangu, hata kama siyo familia yangu. Kucheleweshewa haki ya kuhukumiwa kwa mtuhumiwa wa mauaji ya kule Sombetini, ni kitisho kwangu pia, hata kama kesi siyo yangu,” alisema.
Aliongeza kuwa Mama Ntilie wa Sokoni Kariakoo, akifukuzwa, akapigwa virungu, akanyanganywa pesa zake, akadhalilishwa na kumwagiwa chakula chake na mgambo wa Jiji la Dar es Salaam inaniumiza na kunigusa moyoni, hata kama yeye si mama yangu,” alisema.

Waislamu watibuka kuzikwa Mahakama ya Kadhi

WAKATI Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa bin Shaaban Simba, akitarajia kutoa msimamo wake leo kuhusu hatua ya Bunge Maalumu la Katiba kuzika suala la Mahakama ya Kadhi, Waislamu kupitia Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu (Hayat), wameapa kuipigia kura ya hapana Rasimu ya Katiba pindi itakapofika kwa wananchi.
Akizungumza siku ya Jumapili, Naibu Katibu Mkuu wa Hayat na Mwenyekiti wa Jukwaa la Waislamu la Kuratibu maoni ya Katiba, Sheikh Mohamed Issa, alisema kama Bunge hilo litarudisha Rasimu ya Pili ya Mabadiliko ya Katiba kupigiwa kura na wananchi ikiwa haina kipengele cha Mahakama ya Kadhi, wataipigia rasimu hiyo kura ya hapana.
Alisema kitendo cha wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walio wengi kutogusia suala la Mahakama ya Kadhi ni mwendelezo wa kuwanyima Waislamu haki yao ya muda mrefu.
Lakini hili tumeliona toka katika Tume ya Jaji Warioba walipotuambia kwamba suala hili lisiingizwe katika maoni ya Rasimu ya Katiba hadi nchi mbili washirika kwa maana ya Zanzibar na Tanganyika zitakapokuwa na Katiba zao na waliingize suala hili katika katiba hizo,” alisema Sheikh Issa.
Alisema walihoji jambo hilo, lakini majibu yaliyotoka waliona hayakuwa na nia njema katika kuleta Kadhi katika nchi hii.
Tulipata majibu ambayo yalionyesha kabisa mwelekeo mzima juu ya Kadhi ni negative, kwahiyo toka ilipoanzia na hapa ilipofikia hatushangai,” alisema Sheikh Issa
Sheikh Issa alisema kwa sasa wataendelea kuhamasishana kwa nia ya kupiga kura ya hapana katika rasimu itakayorudishwa kwa wananchi
Mimi sielewi kwanini katika nchi hii tunaogopa Kadhi, majirani zetu wa Kenya wameingiza Kadhi kwenye Katiba yao, jambo hili tumeliomba siku nyingi na tuliambiwa tusubiri mchakato wa Katiba, lakini mchakato ndiyo huu na mambo ndiyo hayo yanayotokea,” alisema Sheikh Issa.
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Simba, alipotafutwa kuzungumzia kuhusu suala zima la Mahakama ya Kadhi, alisema angetoa tamko lake jana baada ya kukutana na viongozi wa Baraza la Maimamu (Ulamaa).
Nimekutana na Ulamaa, katika makubaliano yetu tunasubiri kukutana na wawakilishi wetu wa bungeni watupe taarifa rasmi ili tunapotoa tamko tusije tukapishana wakatulaumu kwamba hatujawashirikisha,” alisema Mufti Simba jana wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu kikao chake na Ulamaa kilichofanyika juzi.
Wakati Mufti akisema hayo, Msemaji wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania (Forum), Sheikh Rajab Katimba, alisema Waislamu kudai Mahakama ya Kadhi si jambo la huruma bali ni haki yao.
Mimi nashangaa kwanini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanakataa Kadhi wakati ilikuwa moja ya jambo waliloweka katika Ilani ya chama chao, najiuliza kwanini watu hawa hawa wakati ule waone linafaa na sasa hivi waone halifai, wanataka kutuaminisha kwamba wao ni vinyonga wanabadilika badilika au vipi, lakini wafahamu kabisa kwamba jambo hili ni haki ya Waislamu na wanachofanya ni kuukataa ukweli kwa muda tu,” alisema Sheikh Katimba.
Suala la Mahakama ya Kadhi liliibua mjadala mkali katika vikao vya Bunge Maalumu la Katiba hadi kuundiwa kamati ndogo iliyokuwa inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu.
Hata hivyo, juzi wakati kamati hiyo ikiwasilisha maoni yake, suala hilo lilionekana kuzimwa kwa sababu ambazo hazikuelezwa bayana.
Ilidaiwa baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo waliweka misimamo ya kutozungumzia suala hilo ingawa baadhi ya wajumbe wachache wa kamati namba nne na tisa waliibua licha ya kutopata mwitikio kama ilivyokuwa katika vikao vya awali.