Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema ndoto yake kubwa ni kuona bara la
Afrika likiungana na kuwa kitu kimoja. Rais Museveni amesema nchi za
Afrika zimeendelea kuwa masikini kutokana na kuwepo ufisadi na
kukosekana miungano thabiti ya kisiasa na uongozi bora. Amesisitiza
kuwa, Wakoloni wamefanikiwa kuendeleza ukoloni mamboleo baada ya kumaizi
kwamba Waafrika hawawezi kujichukulia maamuzi wenyewe bila ya
kusukumwa. Huku hayo yakijiri, Marais wa nchi za Afrika Mashariki
wanatarajia kukutana siku ya Jumamosi mjini Arusha, Tanzania ili
kujadili changamoto zinazoikabili Jumuiya ya EAC. Rais Uhuru Kenyatta wa
Kenya anatarajiwa kuleta mitazamo mipya na itakuwa mara yake ya kwanza
kuhudhuria mkutano wa aina hiyo tangu alipoapishwa kuwa rais Aprili 9.
No comments:
Post a Comment