Wednesday, April 24, 2013

Mahakama Pakistan yakataa kumuachia huru Musharraf

Mahakama Kuu ya Pakistan imekataa kumwachia kwa dhamana Rais wa zamani wa nchi hiyo Pervez Musharraf anayekabiliwa na tuhuma za kuhusika na mauaji ya Bi Benazir Bhutto, Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan.
Musharraf anakabiliwa na kesi nyingine ambayo imemuweka kwenye kifungo cha nyumbani. Musharraf alilituhumu kundi la Taleban kuwa ndilo lililohusika na shambulio la kigaidi dhidi ya Benazir Bhutto, lakini taarifa za kiintelijensia zilizotolewa na makachero wa serikali ya Pakistan zinaeleza kuwa, Musharraf alihusika kwenye njama za kumuua Bhutto.
Umoja wa Mataifa uliituhumu serikali ya Pervez Musharraf kwa kutomdhaminia usalama wa kutosha Bi Benazir Bhutto. Musharraf amepinga vikali tuhuma hizo.

No comments: