Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Ibrahim
Kilongo, aliwaaambia waandishi habari kuwa jeshi hilo limetoa ilani kwa
mbunge huyo kujisalimisha polisi haraka.
Wakati polisi wakisema hayo, Lema ameeleza kushangazwa na hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutoa amri ya kumkamata.
Alisema kibali cha kukamatwa kwake ni lazima kitoke kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Lema aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi
jijini hapa na kuwa atakamatwa ikiwa Spika Makinda atatoa kibali cha
kukamatwa kwani yeye ni mbunge halali wa Arusha Mjini.
Pia aliwapa pole wanafunzi kwa msiba wa mwanafunzi
mwenzao kisha kuwapa pole wanafunzi wengine waliokumbwa na kadhia ya
kupigwa mabomu juzi eneo la chuo wakati wakidai haki zao za msingi
ikiwamo kuhoji matukio ya vifo vya wanafunzi wenzao vinavyotokea mara
kwa mara chuoni hapo.
Hata hivyo, kamanda Kilongo alisema: “Tunamtaka
popote alipo afike mwenyewe polisi na bado tunaendelea kumtafuta popote
alipo, ni muhimu afike tufanye naye mahojiano kuhusu yaliyotokea katika
chuo cha uhasibu."
Lema anatuhumiwa kuhusika katika vurugu zilizopekea kudhalilishwa na kuzomewa kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Mara baada ya kutulizwa kwa vurugu hizo, Mulongo
aliliagiza jeshi la polisi kumkamata Mbunge huyo kwa kile kilicholezwa
kuwa ni kumhusisha na vurugu zilizotokea chuoni hapo juzi.
Katika tukio hilo lililosababisha mabomu ya machozi
kurindima kwa kwa muda chuoni hapo, Mulongo alijikuta akizomewa baada
ya kushindwa kuhutubia mamia ya wanafunzi.
Awali, Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu jijini
Arusha, Faraji Kasidi, alisema chuo hicho kimebeba jukumu la
kuusafirisha mwili wa mwanafunzi Henry Kago (22) na kuupeleka nyumbani
kwao Iringa kwa ajili ya mazishi.
No comments:
Post a Comment