Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeshindwa
kuendelea kusikiliza ushahidi katika kesi dhidi ya aliyekuwa Waziri wa
Viwanda na Biashara Iddi Simba na wenzake wawili wanaokabiliwa na
mashtaka nane likiwamo la kusababishia Shirika la Usafiri Dar es Salaam
(Uda), hasara ya zaidi ya Sh. bilioni mbili.
Mahakama hiyo ililazimika kuahirisha kesi hiyo jana hadi leo kutokana na shahidi upande wa Jamhuri kuwa mgonjwa.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Oswald Tibabyekomya uliiomba
mahakama iwape muda wa kuangalia hali ya shahidi aliyeshindwa kufika
mahakamani hapo jana kutokana na kuwa mgonjwa na kuomba kupeleka shahidi
mwingine leo.
Hakimu Ilvin Mugeta alikubali ombi hilo na kuutaka upande wa mashtaka kuwa na shahidi mwingine na ushahidi utaendelea leo.
Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi ya
UDA na Diwani wa Kata ya Sinza, Salum Mwaking'inda na Meneja Mkuu wa
kampuni hiyo, Victor Milanzi.
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka nane, ikiwemo kula
njama, kughushi, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Uda hasara
ya Shilingi bilioni mbili.
No comments:
Post a Comment