Wednesday, April 24, 2013

Wakimbizi wa Rwanda wahimizwa kutoka Uganda



 24 Aprili, 2013 - Saa 09:05 GMT
Serikali za Uganda na Rwanda kwa kushirikiana na shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, zinapanga kuwarejesha nyumbani wakimbizi kutoka Rwanda katika kipindi cha miezi miwili kutoka sasa.
Hii ni kwa wale ambao wameishi ukimbizini Uganda kwa karibu miongo miwili, hata hivyo sio wote wanaridhia kurejeshwa kwao kwa hiari nyumbani.
Baadhi wanadai kuwa ingawa wao hawapaswi kurejeshwa lakini wanashanga kuona majina yao yameorodheshwa miongoni mwa wanaotaka kurejea.
Hata hivyo madai hayo yamekanushwa na maafisa wanaoshughulikia wakimbizi wa Uganda.
Mwisho wa mwezi Juni mwaka huu, ndio muda uliopewa wakimbizi kutoka Rwanda kuwa wanapoteza hifadhi ya ukimbizi ikitolewa hoja kuwa kwa sasa nchi yao ni tulivu na amani.
Serikali ya Rwanda imekuwa ikiomba shirika la wakimbizi kufuta kipengee kinachowasaidia raia wa Rwanda wanaoishi nje ya nchi hiyo kama wakimbizi.
Kipengee hicho kinawahusu wakimbizi wa Rwanda kutoka miaka ya 1950, 1970,waliokimbia mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 na pia kuzorota kwa usalama kabla ya mwaka wa 1998, na wakuu Uganda wanasema wanyarwanda wanaokumbwa na kipengee hicho wanafikia elfu nne.
Hata hivyo kuna wanaodai kuwa walitoroka Rwanda kwa usalama wao baada ya mwaka wa 1998 wanaodai kuwa majina yao yameorodheshwa katika wale wanaopaswa kurejea nyumbani.
Lakini kamishna wa wakimbizi katika ofisi ya waziri mkuu inayohusika na wakimbizi David Kazungu amepinga madai kuwa majina ya wakimbizi waliokuja baada ya 1998 pia yameorodheshwa.
''Hiyo si kweli na hakikisha kabisa kuwa huo ni uongo.Hii ni kwa sababu tunategemea habari za uhakiki mbalimbali tuliofanya na shirika la UNHCR.Hawa watu wakija husajiliwa rasmi na kila mwaka tunahakiki majina ya wakimbizi hao,'' alisema bwana Kazungu
''Lakini ikiwa umehakikiwa mara kadhaa tangu uwasili na kila mara mwaka wako wa kuwasili ni 1997 kwanini mara moja unabadili mwaka wa 1999 au 2000? Haiwezekani kuwa ulikuja mwaka wa 2000 na tukuweka katika data zetu kama aliekuja mwaka wa 1997 data zetu hazikubali hiyo,'' aliongeza kusema Kazungu
Ukiacha hayo wakimbizi wengi kutoka Rwanda wanaogopa tarehe ya Julai 31 mwaka huu.
Juni 31 ni siku imepangwa kufuta kipengee cha wakimbizi lakini utekelezaji wa hatua hiyo haumanishi kuwa ghafla bin vuu wakimbizi hawataingia tena.
Wahusika wataarifiwa ikiwa wao ni waathirika na tarehe hii ikiwa walikuja Uganda kabla ya 1998.Kisaha watachunguzwa ikiwa wana sababu sababu halali ya kutorejea nyumbani kwa hiari, na endapo jopo litaaamini hoja zako utaendelea kubaki mkimbizi na utasaidiwa vilivyo. Lakini mbali na hili maafisa wanawahimiza wakimbizi kurejea Rwanda.
Wakimbizi halisi kutoka Rwanda ambao wako katika orodha ya kurejeshwa nyumbani baada ya Juni 31 wanafikia 4,100, ingawa duru Fulani zilikuwa zimedai kuwa wanazidi elf 8.



No comments: