Maadhimisho hayo kitaifa mwaka huu yanafanyika
mkoani Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema Rais Kikwete,
anatarajiwa kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe saa
4:30 asubuhi.
Kandoro amewataka wananchi hasa wakazi wa Jiji la Mbeya na
vitongoji vyake, kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais Kikwete katika maeneo
yote atakayopita akitokea Uwanja wa Ndege wa Songwe na pia kujitokeza
kwa wingi kwenye sherehe za Mei Mosi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
(Tucta) Mkoa wa Mbeya, Alinanuswe Mwakapala, alisema maandalizi ya
sherehe hizo yapo katika hatua nzuri na kuwa anaamini kuwa kutokana na
uwapo wa Rais Kikwete kama mgeni rasmi, yatafana kuliko miaka ya nyuma.
Alisema sherehe hizo zinaandaliwa na Tucta na kwa mwaka huu
maandalizi yake yanaratibiwa na Chama cha Wafanyakazi wa Meli na Bandari
(Dowuta), huku kukiwa na kauli mbiu isemayo: ‘Katiba mpya izingatie
usawa na haki kwa tabaka la wafanyakazi’.
Mwakapa alitoa wito kwa waajiri wote kuwaruhusu na kuhakikisha
wafanyakazi wao wanashiriki kikamilifu katika sherehe hiyo ili wafikishe
madai na vilio vyao kwa waajiri.
No comments:
Post a Comment