Mkutano wa kupambana na ufisadi wa kiidara na kifedha barani
Afrika umefanyika Kampala mji mkuu wa Uganda kwa wajumbe kusisitiza juu
ya kutokomezwa ufisadi barani humo.
Washiriki wa mkutano huo wamesisitiza juu ya kuungwa mkono sheria ya kupambana na ufisadi ambayo inapaswa kutekelezwa kikamilifu katika nchi zote za Afrika. Mathew Opoku Prempeh, Mbunge wa Bunge la Ghana amesema kwenye mkutano huo kwamba, sheria pekee si hazitoshi, kwani katika baadhi ya nchi za Kiafrika kuna sheria nyingi dhidi ya vitendo hivyo lakini ufisadi unaendelea kukithiri kwenye nchi hizo. Amesisitiza kuwa hatua za kivitendo zinapaswa kuchukuliwa kupiga vita ufisadi barani Afrika.
Washiriki wa kongamano hilo la Kampala wameafikiana kwamba serikali za bara la Afrika zitangaze utajiri wa viongozi wao wa ngazi mbalimbali.

No comments:
Post a Comment