Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta mapema leo ametangaza majina zaidi ya watu
anaowapendekeza kuwa mawaziri kwenye serikali yake mpya. Rais Kenyatta
amewaarifisha watu 12 wengi wao wakiwa wataalamu. Hata hivyo wanasiasa
mashuhuri kama vile Najib Balala na Charity Ngilu watapata nafasi ya
kurudi kwenye baraza la mawaziri iwapo bunge litawaidhinisha. Wawili hao
ambao wamewahi kuhudumu kama mawaziri katika serikali zilizopita
wamependekezwa kuongoza wizara za Madini na Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya miji. Hata hivyo rais wa Kenya bado hajatangaza watu watakaoongoza
wizara za Mambo ya Ndani na Leba ingawa ameahidi kutoa tangazo kuhusu
suala hilo katika siku chache zijazo. Wakili mashuhuri na balozi wa
zamani wa Kenya nchini Ufaransa, Raychelle Omamo anependekezwa kuongoza
wizara muhimu ya ulinzi. Bi. Omamo anakuwa mwanamke wa kwanza kuwahi
kushikilia wadhifa huo katika historia ya Kenya.
No comments:
Post a Comment