Wednesday, April 24, 2013

Waislamu wasitumbukie katika mtego wa maadui'

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu amesema Waislamu na nchi za Kiislamu zinapaswa kuchukua tahadhari ili zisitumbukie katika mtego wa mifarakano ambao umewekwa na maadui.
Dkt. Ali Akbar Velayati ameyasema hayo leo mjini Tehran alipokutana na ujumbe wa wahadhiri wa vyuo vikuu na mawakili kutoka Misri. Ameongeza kuwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mfumo wa demokrasia ya kidini na kwa hivyo wanaotaka kushiriki katika uchaguzi nchini huchunguzwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Dkt. Velayati ambaye ni mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema sababu muhimu ya kustawi Iran ni irada imara ya wananchi. Ameongeza kuwa kuhuisha thamani, utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu ni nukta muhimu zilizoimarisha Mapinduzi ya Kiislamu Iran na kuipa nguvu nchi hii. Dkt. Velayati ameelezea masikitiko yake kuwa baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati zina dhana potofu ya kwamba, kuwa uhusiano na madola ya kibebebru ndio dhamana ya kubakia tawala zao.

No comments: