Mbunge huyo alihoji iwapo Serikali haioni tatizo
kuwadhulumu baadhi ya waumini muda wao na kwamba jambo hilo limekuwa
likisababisha baadhi ya watu kukimbilia kufanya ibada na huku
wakishindwa kupiga kura.
“Kitendo cha kufanya uchaguzi wa kitaifa siku za
Jumapili kinasababisha baadhi ya watu kushindwa kupiga kura jambo
linalowanyima haki yao ya kikatiba,” alisisitiza Mshama.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi, alikiri kuwa sheria za uchaguzi pamoja na kanuni zake, haziainishi siku maalumu ya iliyoteuliwa kwa ajili ya kupiga kura.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi, alikiri kuwa sheria za uchaguzi pamoja na kanuni zake, haziainishi siku maalumu ya iliyoteuliwa kwa ajili ya kupiga kura.
Lukuvi alisema kuwa uamuzi wa Serikali kuteua siku
ya Jumapili kwa ajili ya kupiga kura ulitokana na sababu kuwa ni siku
ambayo Watanzania wengi hawaendi kufanya kazi hivyo kuwa na fursa katika
zoezi la kupiga kura.
Hata hivyo alikiri kuwa kumekuwa na malalamiko
kutoka kwa watu wengi kuhusu siku ya Jumapili wakitaka ibadilishwe ili
isitumike kwa ajili ya kupiga kura lakini pia Serikali inatambua kwa
dhati kuwa ni siku maalumu kwa ajili ya waumini wa dini ya Kikristo.
Alisema suala hilo litafanyiwa kazi katika
marekebisho ya Katiba Mpya ambayo Tanzania inatarajia kuipataKatiba Mpya
kuanzia Aprili mwakani wakati uchaguzi mkuu utafanyika Oktoba 2015 .
No comments:
Post a Comment