Makumi ya watu mbalimbali wakiwemo Waislamu waishio nchini Uingereza,
wamefanya maandamano mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia wakipinga hakumu
ya kutaka kunyongwa mwanazuoni wa Saudia sheikh Nimr Baqir al-Nimr.
Maandamano hayo yamefanyika leo mjini London, Uingereza. Katika
maandamano hayo yaliyowashirikisha Waislamu wa Bahrain, Saudi Arabia,
India, Pakistan na Iraq, waandamanaji walitoa nara za kulaani utawala wa
Aal Saudi, kuwa ni muenezaji wa ugaidi duniani. Aidha waandamanaji
wamesisitiza juu ya kukomeshwa uingiliaji wa masuala ya ndani ya Bahrain
sambamba na kutaka kuachiliwa huru mwanazuoni huyo anayeendelea
kuzuiliwa katika korokoro za Aal Saudi. Aidha waandamanaji hao waliokuwa
wamebeba mabango mbalimbali, wamelaani vikali uungaji mkono wa Rais
Barack Obama wa Marekani kwa utawala wa Saudia. Katika maandamano hayo
Said al-Shahabi, Mkuu wa Kituo cha Tamaduni mjini London amesema kuwa,
maisha ya Sheikh Nimr Baqir al-Nimr yako hatarini na kwamba, Marekani na
Uingereza kwa kuziunga mkono tawala za Bahrain za Saudia zinahusika
moja kwa moja katika umwagaji damu wa raia wasio na hatia na wapigania
uhuru duniani.
No comments:
Post a Comment