Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, ameziagiza Mamlaka ya
Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra) pamoja na wamiliki
wa vyombo vya usafiri nchini, kuelekeza magari yao ya abiria kwenda
Uwanja wa Taifa wakati wakati wa Maadhimisho ya Miaka 49 ya Muungano
kesho.
Amesema lengo ni kuwarahisishia usafiri wananchi watakao hudhuria kilele cha maazimisho hayo yaweze kufana.
Sadiki aliitoa rai hiyo jana, wakati wa maandalizi ya kilele cha sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
“Katika kipindi cha miaka 49 nchi yetu imepata mafanikio makubwa na ya
kujivunia katika nyanja mbalimbali zikiwamo za maendeleo ya jamii,
uchumi, siasa, ulinzi na uhusiano wa kimataifa,” alisema Sadiki.
Alisema Sherehe hizo zitapambwa na gwaride, maonyesho ya ndege za kivita, silaha za kisasa pamoja na halaiki ya vitabu.
“Tunawaomba wananchi kuhuduria kwa wingi na milango ya uwanja itakuwa
wazi kuanzia saa 12:30 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana,” alisema.
Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni “Amani, utulivu na maendelea ni matokeo ya muungano wetu; tuuenzi na kuulinda’.
No comments:
Post a Comment