Mangungu ameitaka Serikali kutamka kama inaweza kuivunja Tanesco au kuipa mtaji ili ijiendeshe yenyewe.
Katika swali la msingi Mangungu alihoji Serikali
kushindwa kutekeleza agizo la Rais katika kupeleka umeme maeneo ya
Banduka, Mtandago, Miteja, Sinza, Puyu, Matandu na Njenga ambayo
hayapati umeme licha ya umeme huo kupita katika maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini George
Simbachawene alisema masuala ya kuivunja Tanesco au kuiboresha
yanategemea maoni ya wadau ambayo yalikusanywa ndani na nje ya nchi
ambayo bado yanachambuliwa.
Alisema ahadi ya Rais imeanza kutekelezwa ambapo baadhi ya maeneo ya Somanga Fungu yana umeme na wateja 200 wameunganishwa.
Simbachawene alieleza kuwa Serikali inaendelea na
utekelezaji wa mradi mdogo ambapo inatarajia kuunganisha wateja wengine
50 wakati wowote.
Alisema, katika mradi huo tayari nguzo 60
zimetengwa na tayari nguzo 40 zimeshasimamishwa huku Wizara ikifungua
milango kwa wananchi kuanza kutuma maombi ya kuunganishiwa umeme.
No comments:
Post a Comment