Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel
amesema kuwa, miradi ya nyuklia ya Iran bado haijavuka mstari mwekundu.
Akizungumza na wanachama wa chama cha Likud, Netanyahu amedai kuwa, Iran bado inaendeleza miradi yake ya nyuklia japokuwa bado haijavuka mstari mwekundu, lakini inaukaribia mstari huo. Waziri Mkuu wa Israel aliendelea kukariri maneno yake dhidi ya Iran na kusisitiza kuwa, Israel haiko tayari kutoa mwanya kwa Iran kuvuka mstari huo mwekundu.
Hata hivyo Meir Dagan mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Israel MOSSAD amekosoa vikali matamshi hayo ya Netanyahu na kusema kuwa, vitisho vya mara kwa mara vinavyotolewa na Waziri Mkuu wa Israel vya kutaka kuishambulia kijeshi Iran, vimepelekea kuporomoka haiba na itibari ya utawala wa Israel ulimwenguni.

No comments:
Post a Comment