Tuesday, April 30, 2013

Mbunge aishauri Serikali kuivunjavunja Tanesco

Mbunge wa Kilwa Kaskazini kupitia CCM, Murtaza Mangungu ameshauri Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), livunjwe ili kutoa nafasi kwa mashirika mengine yatakayoweza kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mangungu ameitaka Serikali kutamka kama inaweza kuivunja Tanesco au kuipa mtaji ili ijiendeshe yenyewe.
Katika swali la msingi Mangungu alihoji Serikali kushindwa kutekeleza agizo la Rais katika kupeleka umeme maeneo ya Banduka, Mtandago, Miteja, Sinza, Puyu, Matandu na Njenga ambayo hayapati umeme licha ya umeme huo kupita katika maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene alisema masuala ya kuivunja Tanesco au kuiboresha yanategemea maoni ya wadau ambayo yalikusanywa ndani na nje ya nchi ambayo bado yanachambuliwa.
Alisema ahadi ya Rais imeanza kutekelezwa ambapo baadhi ya maeneo ya Somanga Fungu yana umeme na wateja 200 wameunganishwa.
Simbachawene alieleza kuwa Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi mdogo ambapo inatarajia kuunganisha wateja wengine 50 wakati wowote.
Alisema, katika mradi huo tayari nguzo 60 zimetengwa na tayari nguzo 40 zimeshasimamishwa huku Wizara ikifungua milango kwa wananchi kuanza kutuma maombi ya kuunganishiwa umeme.

Hati za wamiliki wa mashamba ya mkonge Muheza kufutwa

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetangaza kuwa wakati wowote itakamilisha mchakato wa kufuta hati za mashamba ya mikonge yaliyotelekezwa katika Wilaya za Muheza na Kilindi mkoani Tanga.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole-Medeye wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilindi Dastan Kitandula (CCM).
Ole Medeye alisema kuwa uamuzi wa kufuta hati miliki hizo kwa sasa uko mikononi mwa Rais baada ya kukamilika kwa hatua zote.
Katika swali hilo Kitandula alitaka kujua ni lini Serikai itafuta hati miliki kwa mashamba ya mkonge ambayo kwa muda mrefu yametelekezwa ili kuwagawia wananchi wenye uhitaji.
Awali, Herbert Mtangi (Muheza-CCM) alitaka kujua ni viwango gani stahiki ambavyo wawekezaji wa zao la katani wanatakiwa kulipa kama ushuru kwa halmashauri husika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia, alisema kuwa halmashauri zote nchini zimepewa mamlaka ya kutoza ushuru wa mazao chini ya kifungu 7 (1) (g) cha sheria ya fedha za serikali za Mitaa.
“Ushuru huu hulipwa na mununuzi na unatozwa mahali ambapo zao linazalishwa na kwa bei ya mkulima yaani bei ya zao kabla ya kuongezwa thamani,” alisema Ghasia.
Alisema wafanyabiashara wote wa zao la mkonge,wanatakiwa kulipa ushuru wa mazao ambao ni kuanzia asilimia 3 hadi 5 kwa mujibu wa sheria.
Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Maji, Dk Binilith Mahenge amemtetea bosi wake, Profesa Jumanne Maghembe kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwake za kupeleka mradi mkubwa wa maji jimboni kwake, huku wilaya zingine zikiachwa ‘yatima’.
Akijibu hoja mbalimbali za wabunge jana, Dk Mahenge alisema mradi wa Mwanga-
Same-Korogwe ni mwendelezo wa miradi mikubwa ya maji kama ule wa Chalinze.
“Yote yaliyoelezwa tutayazingatia. Ni kweli kutokana na unyeti wa suala la maji, lazima hisia zitapelekea mawazo mengi juu ya kasungura kadogo kuonekana mtu mmoja amejimegea wengine hakuna,” alisema Dk Mahenge.

Mbunge ataka Jumapili isitumiwe kwa kupiga kura

Mbunge wa Nkenge, Asumpter Mshama (CCM) ameitaka Serikali kutoa tamko la lini itaacha utaratibu wa kutumia siku ya Jumapili kwa ajili ya kupiga kura.
Mbunge huyo alihoji iwapo Serikali haioni tatizo kuwadhulumu baadhi ya waumini muda wao na kwamba jambo hilo limekuwa likisababisha baadhi ya watu kukimbilia kufanya ibada na huku wakishindwa kupiga kura.
“Kitendo cha kufanya uchaguzi wa kitaifa siku za Jumapili kinasababisha baadhi ya watu kushindwa kupiga kura jambo linalowanyima haki yao ya kikatiba,” alisisitiza Mshama.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi, alikiri kuwa sheria za uchaguzi pamoja na kanuni zake, haziainishi siku maalumu ya iliyoteuliwa kwa ajili ya kupiga kura.
Lukuvi alisema kuwa uamuzi wa Serikali kuteua siku ya Jumapili kwa ajili ya kupiga kura ulitokana na sababu kuwa ni siku ambayo Watanzania wengi hawaendi kufanya kazi hivyo kuwa na fursa katika zoezi la kupiga kura.
Hata hivyo alikiri kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa watu wengi kuhusu siku ya Jumapili wakitaka ibadilishwe ili isitumike kwa ajili ya kupiga kura lakini pia Serikali inatambua kwa dhati kuwa ni siku maalumu kwa ajili ya waumini wa dini ya Kikristo.
Alisema suala hilo litafanyiwa kazi katika marekebisho ya Katiba Mpya ambayo Tanzania inatarajia kuipataKatiba Mpya kuanzia Aprili mwakani wakati uchaguzi mkuu utafanyika Oktoba 2015 .

‘Siyo ajabu mtu wa nje kuajiriwa hapa’

Serikali imesema hakuna shida na wala sio ajabu kuajiri watu kutoka nje ya nchi hasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo ambaye alisema hakuna shida vijana kutoka Kenya kufanya kazi Tanzania katika sekta mbalimbali.
Mulugo alisema kuwa ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatoa nafasi ya watu kutoka nchi moja na kwenda nchi nyingine na kufanya kazi wakiwamo Watanzania kuwapokea wageni kutoka nje na Vijana wa Tanzania kwenda nchi nyingine.
Alikuwa akijibu swali la Christowaja Mtinda (Viti Maalumu-Chadema), ambaye alitaka kujua Tanzania ina mkakati gani wa makusudi katika kuwaandaa Vijana wake kielimu ili waweze kushindana katika soko la ajira la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbunge huyo pia alihoji ni kwa nini Serikali inatoa kipaumbele kwa Vijana wanaosoma masomo ya Sayansi pekee na kuyasahau masomo mengine yakiwamo ya masuala ya uhasibu.
Naibu Waziri alisema kuwa Serikali inatekeleza mikakati katika ngazi zote za kielimu ya kuwaandaa vijana wa kitanzania ili waweze kushindana katika soko la ajira la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alitaja baadhi ya mikakati ni kuvijengea uwezo Vyuo vya Ufundi ili viweze kuzalisha wataalamu ambao watakuwa na uwezo wa kitaaluma na kitaalamu wa kuingia kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Mulugo aliwashukuru wabunge wanaofuatilia mambo bungeni.
Aliwasihi wabunge kushirikiana na Serikali katika mipango yake ya kuboresha vyuo vya ufundi na kwamba lengo ni kuhakikisha vijana wengi wanakuwa na elimu hiyo na kuweza kujiajiri.

Chanzo:Mwananchi

MAGAZETINI LEO













Warioba: Hakuna kurudia uchaguzi mabaraza ya kata

Tume ya Mabadiliko ya Katiba, imepuuza malalamiko ya baadhi ya wananchi na vyama vya siasa kuhusu dosari zilizojitokeza kwenye uchaguzi wa mabaraza ya Katiba na imeamua kwamba inaendelea na mchakato kama kawaida.

Aidha, imesema haishughulikii vitendo vya rushwa, upandikizaji wa mamluki na mivutano ya kisiasa au kidini vilivyojitokeza kwenye chaguzi hizo kwa kuwa kuna vyombo vingine vya dola vinavyoshughulikia mambo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, alisema mchakato mzima wa kuandaa hadi kupata Katiba mpya utawahusisha wananchi na siyo matwaka ya asasi, chama au kikundi fulani.

Alisema kundi au watu ambao hajakuridhika na uchaguzi huo wanaweza kwenda kulalamika kwenye vyombo vya dola vinavyoshughulikia dosari husika.

“Tunatengeneza Katiba ya Tanzania, hatutengenezi ya vyama wala ya kikundi. Natoa wito tena kwa viongozi wa vyama vya siasa, Jumuiya na Taasisi zingine ziwaache wananchi watoe maoni yao kuhusu rasimu ya Katiba kwa uhuru,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:

“Tunaomba vikundi visikilize wananchi wanasemaje, wananchi wana ndoto zao tusije tukalazimisha ndoto zetu zikawa zao.”

AKIRI KUSIKIA MALALAMIKO YA RUSHWA
Kuhusu rushwa, Jaji Warioba alisema kwamba baadhi ya maeneo chaguzi hizo zilitawaliwa na rushwa, lakini akashauri wananchi waende kwenda kulalamika kwenye vyombo husika.

 “Hilo (la rushwa) lilikuwapo na hata kuleta mamluki kwenye uchaguzi, nilistaajabu kusikia watu wanahonga ili wachaguliwe kuingia kwenye mabaraza haya...makosa haya sisi hatushughuliki nayo, yanapaswa kuripotiwa kwenye vyombo husika,” alisema.

Alisema dosari nyingine ni baadhi ya wananchi kuendelea na misimamo na tofauti zao za kisiasa kwa kudhani kwamba Mabaraza ya Katiba ni jukwaa la kutetea maslahi na misimamo ya vyama vya siasa kuhusu Katiba mpya.

Hata hivyo, alisema pamoja na dosari zilizojitokeza, chaguzi zimekamilika kwa asilimia 99.8 Tanzania Bara na asilimia 96.4 Zanzibar.

Jaji Warioba alisema jumla ya kata 3,331 kati ya 3,339 na Shehia 323 kati 335, zimekamilisha vizuri mchakato wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa.

Alisema tume yake inafanya kazi iliyopewa kwa weledi mkubwa na kwamba ilitumia busara kuwashirikisha wananchi kwenye uundaji wa mabaraza ya Katiba japokuwa sheria inairuhusu tume kufanyakazi hiyo yenyewe.

Alifafanua kuwa sheria ya Mabadiliko ya Katiba sura ya 83 inaeleza kwamba kutakuwa na aina mbili za mabaraza; moja ambalo litaundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume yake na lingine ni la hiari litakaloundwa na asasi, taasisi au makundi ya watu wenye malengo yanayofanana.

Alisema aina ya pili ya mabaraza hayo yatajiunda, kujisimamia na kujiendesha yenyewe kisha kuwasilisha maoni yao kuhusu rasimu ya Katiba kwa tarehe ambazo zitapangwa na Tume.

Alisema kwenye uundwaji wa aina ya kwanza ya mabaraza, Tume iliona busara kuwashirikisha wananchi hivyo ikatoa mwongozo wa kuchagua wajumbe kwa kutumia utaratibu uliowekwa na sheria ya Serikali za Mitaa sura 287 na 288 kupitia mikutano kwa ajili ya jambo maalum la Kata.

Alisema inashangaza kunaibuka malalamiko kwamba mabaraza hayo ni ya kisiasa wakati utaratibu huo umekuwa ukitumika kuchagua kamati za kusimamia mambo mbalimbali ya kata kama elimu, afya, miradi na maendeleo.

Kuhusu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kususia mchakato huo kama utaratibu hautasitishwa, Jaji Warioba alisema hataki kujiingiza kwenye malumbano ya kisiasa kwa kuwa watakaokubali au kukataa katiba ni wananchi.

Alisema: “Kama tusipoondokana na hii ya kujiweka vipande vipande hatutafikia mwafaka.”
Jaji Warioba ambaye alifuatana na Makamu wake, Jaji Augustino Ramadhan, alisema tayari Tume imeanza kupokea majina ya watu wote waliochaguliwa kuwa wajumbe pamoja na majina ya madiwani wote, mkurugenzi wa baraza la manispaa, makatibu wa mabaraza ya miji na halmshauri za wilaya.

Alisema mchakato wa uwasilishaji wa majina itakamilika leo na kwamba kwenye kata na shehia ambazo uchaguzi ulivurugika, Tume inaendelea kuwasiliana na watu wa maeneo hayo ili kurudia uchaguzi.

Aliongeza kuwa kata ambazo hazijafanya uchaguzi ni tatu ambazo ni za mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Kagera.

MAAMUZI MAGUMU
Alisema hivi sasa Tume inaandaa rasimu ya katiba na kwamba inatekeleza kazi hiyo kwa weledi mkubwa.

“Hali halisi inayojitokeza ni kwamba Tume italazimika kufanya maamuzi magumu, wananchi zaidi ya 300,000 na makundi maalum zaidi ya 160 yametoa maoni yao. Katika mambo mengi ya msingi maoni yanakinzana na katika hali hiyo, lazima Tume ichague moja kati ya maoni hayo na kuyaacha mengine,” alisema.

Alisema Tume yake itafanya maamuzi magumu kwa manufaa ya nchi kwa kuingiza kwenye Katiba hoja ambazo zitalisaidia Taifa.

“Kwa msingi huo, tume inawashauri wananchi nao wawe tayari kufanya maamuzi magumu, kama kila mmoja akitaka wazo lake likubalike haitawezekana kufikia mwafaka. Kila mmoja awe tayari kusikiliza mawazo ya wengine. Ni lazima wote tuwe tayari kufanya maamuzi magumu,” alisema Jaji Warioba.

Alitoa mfano kwamba baadhi ya maoni yanayokinzana ni wengine wanataka kuvunja Muungano wakati wengine wakitaka uendelee na wengine wanataka Muungano wa mkataba.

Alisema baadhi ya wananchi wanataka serikali nne yaani ya Pemba, ya Unguja, ya Tanganyika na Jamhuri ya Muungano, wengine wanataka moja, mbili na wengine tatu.

“Katika hali hii ni lazima tume ichague moja na kuyaacha mengine na tuko tayari kujieleza kwanini tulichukua hili tukaache lile,” alisema.

Alitoa wito kwa vyama vya siasa, jumuiya, taasisi au makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kutumia fursa ya kisheria kuunda mabaraza ya katiba na kutoa maoni yao kuhusu rasimu.

Maelezo hayo ya Jaji Warioba yamelenga kupuuza maoni yaliyotolewa na Chadema bungeni baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, kusema kwamba chama hicho kitasusia mchakato wa katiba unaoendelea kwa kuwa inaonekana kwamba mabadiliko yaliyokusudiwa yanaelekea kuilinda CCM na Serikali yake na kuendeleza baraka za “Status Quo”.

Alisema ushahidi wa mwanzo unaonyesha kwamba utaratibu wa kupata mabaraza ya katiba ni mabaraza ya CCM na siyo mabaraza ya Watanzania kutokana na wajumbe hao kuchaguliwa na kamati ya maendeleo ya kata na kwamba umelenga kuwagawa wananchi.

Polisi watoana kafara Liwale

Vurugu za kuchomeana nyumba zilizowakumba wakazi wa Wilaya ya Liwale, zimemtoa kafara aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo (OCD), Lucian Ngoromela, habari zikisema kuwa ameng’olewa na kurudishwa makao makuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi.

Mbali na hatua hiyo, kuna madai kuwa huenda akahojiwa ili aeleze kwa nini athari za tukio hilo zimekuwa kubwa kiasi hicho.

Hatua ya kumuondoa OCD Ngoromela Liwale imechukuliwa baada ya kubainika kuwa siku ya tukio (usiku wa kuamkia Aprili 24, mwaka huu), simu yake ya mkononi haikupatikana hadi kesho yake, kitendo ambacho kinadaiwa kilitoa mwanya kwa wahalifu kuchoma nyumba 20 ikiwamo ofisi ya serikali iliyokuwa ikitumiwa na Mbunge wa Liwale, Faith Mitambo (CCM).

Mbali na nyumba hizo, katika tukio hilo pia maduka 11 yalivunjwa na mali kuporwa huku trekta ndogo tano aina ya Powertiller zikiteketezwa kwa moto.

Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE lililokuwa limepiga kambi mjini humo, unaonyesha kuwa hatua ya kumng’oa OCD Ngoromela inalenga kurudisha imani ya wananchi wa wilaya hiyo kwa Jeshi la Polisi.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kikao cha pamoja kati ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, George Mwakajinga; Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Abdallah Ulega; Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Ephreim Mbaga na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mungulu.

Uchunguzi umeonyesha kuwa, wavamizi walianza kuchoma nyumba ya mbunge iliyopo kijiji cha Kingolowira Kata ya Nangando saa 2:30 usiku na waliendelea hadi alfajiri ya Aprili 24 bila hatua zozote kuchukuliwa na Jeshi la Polisi.

Habari zinasema kuwa wachomaji hao walikuwa wakisikika wakisema ‘tukimaliza kuchoma nyumba hii twende katika nyumba ya fulani’ na kwamba walifanya hivyo.

Uchunguzi unaonyesha kuwa kukosekana kwa mawasiliano kulisababisha polisi kurundikana kituo cha polisi ili kulinda fedha zilizowasilishwa hapo na viongozi wa vyama vya ushirika baada ya wakulima wa korosho kukataa kupokea malipo ya nyongeza ya Sh. 200 badala ya Sh. 600 yaliyoahidiwa kutolewa awali.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Abdallah Ulega, alipoulizwa na NIPASHE kuhusu taarifa za uhamisho wa ghafla wa OCD Ngoromela, alithibitisha na kusisitiza kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kwa nia njema ikiwamo kutafuta amani ya kudumu wilayani humo.

Mapema akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa mji wa Liwale, Ulega alisema pamoja na kasoro mbalimbali zilizobainika katika mfumo wa stakabadhi ghalani, pia uasi umechangiwa na baadhi ya viongozi wa serikali kushindwa kuwajibika kwa wakati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mwakajinga, alithibitisha kwa kuwa OCD Ngoromela, amehamishiwa makao makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi.

Jaji Manento: Polisi wanabambikia kesi raia

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji mstaafu Amiri Manento, amelituhumu Jeshi la Polisi nchini kuwa linawabambikiza kesi wananchi na kutumia nguvu nyingi kupita kiasi zinazosababisha vifo vya raia wasiokuwa na kosa.

Alisema jeshi hilo limeshindwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu katika utendaji wa kazi wa kila siku na kwamba hatua hiyo inayochangia kuwapo kwa matukio ya mauaji ya raia katika maeneo mbalimbali nchini.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye Jukwaa la Asasi za Kiraia zinazopinga adhabu ya kifo na kusisitiza kuwa polisi wanakiuka maadili katika utendaji wao wa kazi. Alisema  polisi wanaokiuka maadili ya kazi, lakini hawajawahi kuchukuliwa hatua zinazostahili na kwamba hali hiyo imekuwapo kwa kipindi kirefu.

Jaji Manento alilitaka jeshi hilo kufanya kazi kwa kufuata sheria za nchi na kwamba yeye na tume yake kazi yao ni kuhubiri amani na kwamba hawana mamlaka kisheria ya kukamata mtu yeyote.

Kuhusu Tanzania kufuta adhabu ya kifo, Jaji Manento alisema jambo hilo linahitaji muda na kwamba haiwezekani likafanyika kwa mara moja na kumalizika.

“Huwezi kuamka asubuhi na kusema umefuta adhabu ya kifo, badala yake uwe ni mchakato wa muda mrefu ambao mwisho wake utasaidia kuifuta na kuondokana nayo,” alisema.

Akizungumzia mauaji yanayofanywa na wananchi dhidi ya wenzao, Jaji Manento alisema tatizo hilo linatokana na watu kutokuwa na kazi maalum za kufanya na kwamba vijijini zinapofanyika shughuli za kilimo takwimu za mauji zipo chini ikilinganishwa na mijini.

Aliitaka jamii kujisikia vibaya mtu mmoja anapopoteza maisha kwa namna yoyote ile na kwamba ikifikia hapo inaweza kupunguza mauaji yanayofanywa na raia wenye hasira.

Kuhusu jamii kubadilika na kutii sheria, Jaji Manento alisema tume yake kwa kipindi kirefu imekuwa ikizunguka nchi nzima kutoa elimu ya namna hiyo ingawa bado vitendo viovu vinaendelea kufanyika maeneo mbalimbali nchini.

Mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia, alisema adhabu ya kifo imeendelea kutolewa nchini licha ya kuwa tangu mwaka 1994, marais hawajawahi kutia saini ili waliohukumiwa wanyongwe.

Alisema hukumu ya kifo ni miongoni mwa sheria mbaya zinazotakiwa kufutwa kwa kuwa haitoi fundisho kwa mhusika badala yake inaongeza maumivu. Aliongeza kuwa umefika wakati serikali kuwa na adhabu mbadala badala ya kifo kwa kuwa tangu imeanza kutolewa tatizo halijaweza kumalizika katika jamii na kwamba matukio ya mauaji yameendelea.

Mmoja wa mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo na Mahakama Kuu na kuachiwa huru na Mahakama ya Rufaa, Michael Lembeli, alisema alikamatwa na polisi akiwa kidato cha nne mwaka 1994 na kubambikwa kesi ya mauaji. Alisema siku aliyokamatwa polisi walifika nyumbani kwao wakimsaka mpangaji wao waliyedai kamba aliiba mito ya makochi na baada ya kumkosa wakamkamata yeye, lakini cha kushangaza alipofika kituoni aliambiwa ameua ofisa wa Jeshi.

Alisema licha ya kubambikiwa kesi hiyo, lakini pia alipigwa na kulazimishwa kukubali kuandika maelezo polisi kwamba ameua ili aachiwe huru. Alisema baada ya kuyaandika, yalitumika mahakamani kama ushahidi na hivyo kumfanya atiwe hatiani na kuhumiwa kifo na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Bajeti ya maji yawa moto

Wakati serikali ikijikusanya huko na huko ili kuongeza bajeti ya  Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 kutoka Sh. bilioni 398.4 zilizokuwa zimetengwa awali hadi Sh. bilioni 582.8, jana pia ilijikuta ikifurushwa kwenda kujipanga vema baada utoaji wa taarifa ya nyongeza hiyo kudaiwa kukiuka kanuni.

Hali hiyo ilitokea baada serikali kupitia kauli ya Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kueleza jinsi nyongeza ya fedha hizo ilivyopatikana, lakini wabunge wakapinga utaratibu uliotumika.

Wabunge hao ni pamoja na Tundu Lissu (Singida Mashariki-Chadema) na John Mnyika (Ubungo-Chadema), ambaye alisema kwa jinsi mawaziri hao walivyotoa kauli za serikali, ni sawa na kuwauzia wabunge mbuzi kwenye gunia.

Walisema utaratibu wa mawaziri hao ulikiuka kanuni za Bunge namba 49 (3), 57 (2) na 100 (1) na kutaka kiti cha Spika kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kuahirisha mjadala wa bajeti hiyo.

Kwa mujibu wa wabunge hao, kanuni hizo zinamtaka waziri kutoa nakala kwa wabunge kuhusu kauli ya serikali anayoitoa bungeni, jambo ambalo halikufanywa na mawaziri hao hata kwa Spika pia.

Akitoa Mwongozo wake, Spika Makinda, pamoja na mambo mengine, alisitisha mjadala wa bajeti hiyo jana asubuhi hadi katika kikao cha jana jioni ili kuipa serikali nafasi ya kwenda kujipanga vizuri.

Kabla ya kuahirisha kikao hicho, Makinda alisema kwa taarifa alizonazo ni kuwa fedha zilizoongezwa zimetoka katika mafungu ya posho katika wizara ambazo zimeshawasilisha bajeti yake.

Kutokana na udhaifu huo, Spika aliahirisha kikao cha Bunge asubuhi hadi jana jioni ili serikali ikatimize wajibu wake kwa mujibu wa kanuni.

Awali, serikali ilisema kuwa iliamua kuongeza fedha hizo ili kukabiliana na tatizo kubwa la upatikanaji wa maji nchini, hususan maeneo ya vijijini, lililolalamikiwa na wabunge.

Nyongeza hiyo inafuatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, ambayo ilipendekeza kuongezwa Sh. bilioni 184.5 katika bajeti hiyo ili kukidhi mahitaji makubwa ya maji nchini.

Aidha, matumizi ya kawaida bajeti yake imeongezwa kutoka Sh. bilioni 18.9 hadi Sh. bilioni 29.6 huku fedha za matumizi mengine zikipungua kutoka Sh. bilioni 16 hadi Sh. bilioni tano.

Kadhalika, serikali imeonya kuwachukulia hatua kali maofisa wote wa wilaya watakaokwamisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini, ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi.

 Hata hivyo, wakati hayo yakijiri, baadhi ya wabunge kutoka upinzani wameonyesha wasiwasi wao kuhusu nyongeza hiyo kwa maelezo kwamba, kanuni za Bunge katika kutoa kauli hiyo ya serikali bungeni zilikiukwa.

Wakati Waziri Mgimwa akieleza nyongeza hiyo, Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, alitoa onyo hilo dhidi ya watumishi wa umma wanaosimamia sekta ya maji.

Waziri Mgimwa alisema serikali imelitazama tatizo lililokuwa likiikabili bajeti hiyo, kuangalia kwa umakini hoja za wabunge na kutazama umuhimu wa maji kwa wananchi.

Kutokana na hilo, alisema serikali imeona iungane na hoja za wabunge kwamba, tatizo la maji walipe kipaumbele zaidi.

Alisema jambo la pili, ni kwamba, katika kutoa kipaumbele zaidi kwa upande wa maji, serikali imelifanyia kazi suala hilo kiundani na kuangalia namna ya kupata fedha za ziada kwa kutazama mafungu mengine.

“Tumetazama kiundani na kuona mafungu mbalimbali ya posho, ambayo hayataathiri sana utendaji wa serikali yakipunguzwa, basi tuyapunguze mafungu hayo tuongeze fedha katika Mfuko wa Maji,” alisema Waziri Mgimwa.

 Jambo la tatu, alisema katika kuitekeleza kazi hiyo, wizara yake itawasilisha katika kipindi cha kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Matumizi ili maeneo ambayo yatapunguzwa, yalete afueni kwa ajili ya bajeti ya maji yatakayoguswa.

Alisema jambo la nne, katika kutekeleza kazi hiyo, uchambuzi huo wa ndani atauwasilisha kwenye kamati husika ili wajumbe wake waone maeneo ambayo watayagusa ili kusaidia kuongeza mafungu ya maji.

Kwa mujibu wa Waziri Mgimwa, wamezingatia vifungu vilivyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Maji na Mifugo, na kwamba, kiwango hicho ndicho walichokizingatia katika kuongeza bajeti ya Wizara ya Maji.

Baada ya kueleza hayo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alimtaka Waziri Mgimwa, kutaja kiwango cha fedha kilichoongezwa kwenye bajeti ya Wizara ya Maji.

Waziri Mgimwa alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo, baada ya kueleza kwa undani, alipendekeza ziongezwe Sh. bilioni 184.5 na kwamba, kiwango hicho ndicho kilichopendekezwa pia na wabunge wakati wakiijadili bajeti hiyo bungeni.

Waziri Maghembe alisema fedha za utekelezaji wa miradi ya maji zimeshapelekwa vijijini, utekelezaji wake utakamilika ifikapo mwaka 2019 na kwamba, asilimia 62 ya watu watapata maji nchini kote.

Alisema ifikapo Septemba, mwaka huu, watakagua wilaya na kwamba watachukua hatua, ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi maofisa watakaoshindwa kutekeleza miradi ya maji.

Hata hivyo, alisema utekelezaji wa miradi ya maji si kazi ya ushabiki wa kisiasa, bali ni ya ujenzi wa miundombinu, hivyo haiwezekani kuandamana kwenda Wizara ya Maji kupewa glasi ya maji kwa siku moja.

Kuhusu teknolojia ya matumizi ya maji ya bahari kwa Dar es Salaam, alisema kumekuwa na maendeleo ya kuondoa chumvi kwenye maji hayo na kwamba, utafiti wake unaendelea.

Alisema ameunda kamati ya wataalamu itakayoongozwa na Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Ardhi (Aru), Profesa Idrisa Mshoro, kufuatilia thamani ya miradi ya maji ili kudhibiti matumizi ya fedha nyingi za miradi hiyo na kwamba, serikali italipa visima vitakavyotoa maji na siyo ‘vikavu’.

KESI YA MAUAJI PADRE MUSHI Z'bar: Mahakama yatupa ombi la mshtakiwa

Mahakama Kuu ya Zanzibar imetupilia mbali ombi la mtuhumiwa wa mauaji ya Padre Evarist Mushi, la kupinga kukamatwa na kushikiliwa kwa zaidi ya saa 24 bila ya kupelekwa mahakamani, kutokana na ombi hilo kufunguliwa kinyume na sheria za Zanzibar.

Mtuhumiwa Omar Mussa Makame (35), alifungua ombi hilo mahakamani kupitia jopo la mawakili wanaomtetea Abdallah Rajab Abdallah na Abdallah Juma Mohamed.

Mawakili hao walikuwa wakipinga kitendo cha Jeshi la Polisi Zanzibar kumkamata mtuhumiwa huyo Machi 17, mwaka huu na kufikishwa mahakamani Aprili 5, mwaka huu.

Akisoma hukumu baada ya kusikiliza ombi hilo, Jaji wa Mahakama Kuu, Mkusa Isaack Sepetu, alisema ombi hilo lilifunguliwa kinyume na kifungu cha nne Sura ya 28 cha Sheria ya Zanzibar.

Aidha, Jaji Mkusa alisema maombi hayo yameonekana kuwa na tarehe mbili tofauti, ikiwamo mwezi Machi na Aprili na hivyo kuipa wakati mgumu mahakama kufahamu ni tarehe ipi ambayo hati ya kiapo ilifunguliwa kabla ya kusikilizwa na kutolewa uamuzi wake.

“Kutokana na kasoro hizo za kisheria, maombi hayo hayakuwa na nguvu za kisheria, kujadiliwa na kutolewa maamuzi na kwa msingi huo,  Mahakama imeyatupa,” alisema Jaji Mkusa.

Hata hivyo, wakati hukumu hiyo inasomwa, mawakili wote wanaomtetea mshtakiwa huyo hawakuwapo na wakati Jaji Mkusa, akijitayarisha kupanga tarehe ya kutajwa kesi ya msingi, wakili kutoka kampuni ya A.J.M Shaban Juma Shaban, alifika ghafla katika ukumbi wa mahakama na kuitaka mahakama kurejea hatua ya mwenendo wa kesi ilipofikia.

Jaji Mkusa aliwataka mawakili hao kuwa makini wanapotekeleza majukumu yao, kwa vile kampuni hiyo ina mawakili wengi na hakukuwa na sababu za msingi za kutofika wakili hata mmoja wakati wakifahamu kesi ya msingi itatajwa pamoja na kutolewa hukumu ya ombi la mteja wao.

“Natoa nafasi kwa upande wa Mwendesha Mashitaka, kurudia maelezo aliyoyatoa mahakamani kuhusu kesi ya msingi, lakini tabia hiyo iwe mwanzo na mwisho,” alisema Jaji Mkusa.

Aidha, Jaji Mkusa aliwataka mawakili hao kutorudia hoja wanazoziwasilisha mahakamani na kutolewa uamuzi ili kuepusha mahakama hiyo kuwa kama gurudumu la kujadili mambo ambayo yameshajadiliwa na kutolewa uamuzi wake.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili Shabani kutaka mahakama hiyo imwachie huru mtuhumiwa huyo kama upelelezi bado haujakamilika pamoja na kutaka Mmhakama iwape muda maalum wa kuhakikisha upelelezi unakamilika, hoja ambazo zimewahi kuwasilishwa na Wakili Abdallah Juma Mohamed Aprili 19, mwaka huu.

Awali, Mwendesha Mashitaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Abdallah Issa Mgongo, aliieleza mahakama hiyo kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Mgongo alisema uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hivyo kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine ya kusikilizwa kwa shauri hilo, lakini wakati akitoa maelezo hayo mawakili wa mtuhumiwa hawakupo katika ukumbi wa mahakama hiyo.

Jaji Mkusa aliiahirisha kesi hiyo hadi Mei 9 mwaka huu na kuwataka wahusika wote kuhakikisha wanafika kwa wakati ili kuepusha usumbufu wowote kama ulivyojitokeza jana.
CHANZO: NIPASHE

Kikwete kuanza ziara ya mkoani Mbeya leo

Rais Jakaya Kikwete, leo anaanza ziara ya siku mbili mkoani Mbeya ambapo pia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi.
 
Maadhimisho hayo kitaifa mwaka huu yanafanyika 
mkoani Mbeya.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema Rais Kikwete, anatarajiwa kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe saa 4:30 asubuhi.
 
Kandoro amewataka wananchi hasa wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake, kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais Kikwete katika maeneo yote atakayopita akitokea Uwanja wa Ndege wa Songwe na pia kujitokeza kwa wingi kwenye sherehe za Mei Mosi.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Mkoa wa Mbeya, Alinanuswe Mwakapala, alisema maandalizi ya sherehe hizo yapo katika hatua nzuri na kuwa anaamini kuwa kutokana na uwapo wa Rais Kikwete kama mgeni rasmi, yatafana kuliko miaka ya nyuma.
 
Alisema sherehe hizo zinaandaliwa na Tucta na kwa mwaka huu maandalizi yake yanaratibiwa na Chama cha Wafanyakazi wa Meli na Bandari (Dowuta), huku kukiwa na kauli mbiu isemayo: ‘Katiba mpya izingatie usawa na haki kwa tabaka la wafanyakazi’.
 
Mwakapa alitoa wito kwa waajiri wote kuwaruhusu na kuhakikisha wafanyakazi wao wanashiriki kikamilifu katika sherehe hiyo ili wafikishe madai na vilio vyao kwa waajiri.

Shahidi akwamisha kesi ya akina Iddi Simba

Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu, jijini Dar es Salaam imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi katika kesi dhidi ya  aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Iddi Simba na wenzake wawili wanaokabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kusababishia Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), hasara ya zaidi ya Sh. bilioni mbili.

Mahakama hiyo ililazimika kuahirisha kesi hiyo jana hadi leo kutokana na  shahidi upande wa Jamhuri kuwa mgonjwa.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Oswald Tibabyekomya uliiomba mahakama iwape muda wa kuangalia hali ya shahidi aliyeshindwa kufika mahakamani hapo jana kutokana na kuwa mgonjwa na kuomba kupeleka shahidi mwingine leo.

Hakimu Ilvin Mugeta alikubali ombi hilo na kuutaka upande wa mashtaka kuwa na shahidi mwingine na ushahidi utaendelea leo.

Watuhumiwa wengine  katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi ya UDA na Diwani wa  Kata ya Sinza, Salum Mwaking'inda na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Victor Milanzi.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka nane, ikiwemo kula njama, kughushi, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Uda hasara ya Shilingi bilioni mbili.

Lipumba: Rasilimali zinatumika kifisadi

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema rasilimali za nchi zikitumika vizuri na kuwepo mipango bora, zitasaidia kuondoa umaskini wa Watanzania.
Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui.
Prof. Lipumba alisema sera mbovu za serikali ya CCM ndizo zinamfanya Mtanzania aendelee kuwa maskini wa kutupwa na kwamba hali ilivyo sasa chama hicho tawala kinawapeleka pabaya Watanzania.
“Wananchi ndugu zangu hali ilivyo sasa serikali ya CCM ndiyo iliyotufikisha hapa...tunahitaji kufanya maamuzi magumu vinginevyo tutaendelea kuwa kama tulivyo, tunahitaji pia kuwa na serikali makini na siyo hii ya sasa ambayo haina huruma na wannchi wake,” alisema.
Prof. aliongeza kuwa hali ilivyo sasa ndani ya serikali ya CCM ni rushwa, wizi ubadhirifu na matusi na kwamba hakuna linalofanyika ili kumkomboa Mtanzania na hali ngumu ya maisha.
Alisema kuwa waathirika wakubwa wa umaskini huo ni wajawazito, watoto na wazee.
Kuhusu elimu, Prof. Lipumba alisema kwa kiwango kikubwa elimu nchini imeporomoka na asilimia 60 ya vijana wanaofanya mitihani ya darasa la saba wanafeli na kwamba ipo haja serikali ikawezekeza kwenye sekta hiyo kama inataka maendeleo.
Aligusia pia Reli ya Kati na kudai serikali ya CCM imeiua kwani mkoa wa Tabora uchumi wake ulitegemea reli hiyo ikiwemo ajira ambapo katika kipindi cha mwaka 2002 tani milioni 1.4 zilisafishwa kwa reli lakini kwa sasa tani 130,000 ndizo zinasafishwa.
Aidha alisema hata barabara ambazo Rais Jakaya Kikwete ameweka mawe ya msingi ana uhakika haziwezi kukamilika kwa wakati na kwamba itafika mwaka 2015, zitakuwa bado na gharama zitazidi kuongezeka kulingana na mikataba ilivyo.
Prof. Lipumba aliongeza kuwa tumbaku ni zao la kwanza linalochangia pato la taifa kwa fedha za kigeni lakini mkulima wa zao hilo yuko hoi kutokana na serikali kuweka mipango ya kinyonyaji kwake.
Alisema ifikie mahali serikali ya CCM iweke utaratibu mzuri kwenye mazao kama karanga, alizeti na mpunga kuwa mazao ya biashara tofauti na ilivyo sasa.
Alifafanua kuwa yuko mbioni kuanzisha asasi mkoani Tabora ambayo itakuwa ikisimamia maendeleo ya mkoa kwenye sekta ya kilimo, biashara, elimu na viwanda na ana imani itatoa dira na muelekeo mzuri wa maendeleo ya mkoa huu aliodai umeaachwa kama kisiwa.

Nauli mpya ya mabasi yawagawa madereva

Madereva wa Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam, wamepatwa na wakati mgumu tangu serikali itangaze kuongezwa nauli kwa vyombo hivyo.

Hali hiyo inatokana na mgawanyiko uliopo kati ya madereva hao ambao baadhi yao wanaendelea kutumia nauli za zamani kwa lengo la kuwapata abiria na kuwafanya wanaotumia nauli mpya kukimbiwa abiria wao.

Akizungumza jana, Mohamed Shebe, ambaye ni dereva wa basi linalofanya safari zake kati ya  Dar es Salaam na Dodoma, linalomilikiwa na kampuni ya Gairo Coach, alisema hali hiyo inatokana na madereva hao kutokuwa na msimamo kama waliokuwa nao wale wa daladala.

Kwa mujibu wake, nauli mpya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa mabasi ya kawaida ni Sh.16,700 kutoka 14,000, lakini baadhi ya madereva wako tayari kupunguza nauli hiyo kati ya Sh. 9,000 na Sh. 10,000.

Aliongeza kuwa kwa upande wa mabasi yaendayo Morogoro, badala ya kutumia nauli mpya ya Sh.13,000 baadhi ya madereva hulazimika kutumia nauli ya zamani ya kati ya Sh. 6,000 na Sh.6,500 ili kupata abiria wengi.

Alisema wanalazimika kutumia viwango vya nauli vya zamani kwa lengo la kuwavuta abiria.

Kwa upande wake, Ibrahim Juma, kondakta wa basi la Simba Mtoto, linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Tanga, alisema  baadhi ya abiria wanakubaliana na mabadiliko hayo lakini takriban asilimia 15 wanaosafiri na usafiri huo hulipa nauli ya zamani ya Sh.11,000 badala ya sasa ya Sh.13,000 ya sasa.

Kwa mujibu wa Juma, changamoto hiyo inatokana na wananchi kuwa na hali ngumu ya maisha inayowasabisha kutomudu kiasi hicho cha nauli mpya.

Juma aliongeza kuwa mbali na nauli hizo kuongezwa, bado wana wasiwasi iwapo kutawanufaisha kwani bado hawajajua mkutano wa Bunge la Bajeti mwaka huu litaamua nni kuhusu kupanda au kushuka kwa gharama za mafuta.

Serikali ilipandisha nauli za usafiri wa vyombo hivyo mwezi uliopita kufuatia maombi ya wamiliki wa vyombo vya habari kudai gharama za uendeshaji zimepanda.
 

Netanyahu: Iran bado haijavuka mstari mwekundu

Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa, miradi ya nyuklia ya Iran bado haijavuka mstari mwekundu.
Akizungumza na wanachama wa chama cha Likud, Netanyahu amedai kuwa, Iran bado inaendeleza miradi yake ya nyuklia japokuwa bado haijavuka mstari mwekundu, lakini inaukaribia  mstari huo. Waziri Mkuu wa Israel aliendelea kukariri maneno yake dhidi ya Iran na kusisitiza kuwa, Israel haiko tayari kutoa mwanya kwa Iran kuvuka mstari huo mwekundu.
Hata hivyo Meir Dagan mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Israel MOSSAD amekosoa vikali matamshi hayo ya Netanyahu na kusema kuwa, vitisho vya mara kwa mara vinavyotolewa na Waziri Mkuu wa Israel vya kutaka kuishambulia kijeshi Iran, vimepelekea  kuporomoka haiba na itibari ya utawala wa Israel ulimwenguni.

17 wauwa katika mapigano kaskazini mwa Nigeria

Kwa akali watu 17 wameuawa katika mapigano makali yaliyojiri kati ya askari jeshi wa serikali ya Nigeria na makundi yanayobeba silaha katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Luteni Kanali A.G Laka amethibitisha kutokea mapigano hayo katika eneo la Bama, lililoko katika jimbo la Borno. Luteni Kanali Laka amesema kuwa, kwenye mapigano hayo maafisa saba wa polisi na askari wengine kumi waliuawa.
Hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusina na shambulio hilo, lakini inashukiwa kwamba kundi la Boko Haram ndilo lililotekeleza shambulio hilo. Kundi la Boko Haram limekuwa likitekeleza operesheni  dhidi ya majengo ya serikali kama mashule, mahospitali na miundombinu mbalimbali katika eneo la kaskazini mwa Nigeria tangu mwaka 2009.

Mkutano: Ufisadi upigwe vita barani Afrika

Mkutano wa kupambana na ufisadi wa kiidara na kifedha barani Afrika umefanyika Kampala mji mkuu wa Uganda kwa wajumbe kusisitiza juu ya kutokomezwa ufisadi barani humo.
Washiriki wa mkutano huo wamesisitiza juu ya kuungwa mkono sheria ya kupambana na ufisadi ambayo inapaswa kutekelezwa kikamilifu katika nchi zote za Afrika. Mathew Opoku Prempeh, Mbunge wa Bunge la Ghana amesema kwenye mkutano huo kwamba, sheria pekee si hazitoshi, kwani katika baadhi ya nchi za Kiafrika kuna sheria nyingi dhidi ya vitendo hivyo lakini ufisadi unaendelea kukithiri kwenye nchi  hizo. Amesisitiza kuwa hatua za kivitendo zinapaswa kuchukuliwa kupiga vita ufisadi barani Afrika.
Washiriki wa kongamano hilo la Kampala wameafikiana kwamba serikali za bara la Afrika zitangaze utajiri wa viongozi wao wa ngazi mbalimbali.

Mwili wa Kilonzo kupasuliwa leo

Mwili wa aliyekuwa Seneta wa Kaunti ya Makueni nchini Kenya Mutula Kilonzo unatarajiwa kufanyiwa upasuaji leo baada ya shughuli hiyo kuakhirishwa jana.
Shughuli hiyo inafanyika ili kubaini sababu halisi ya kifo cha ghafla cha waziri huyo wa zamani wa elimu wa Kenya kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa nyumbani kwake.
Familia ya Kilonzo imemwajiri mwanapatholojia wa Uingereza kushiriki katika timu inayochunguza kifo cha mwanasiasa huyo aliyewahi kushika myadhifa mbalimbali za uwaziri katika serikali ya Kenya.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma wa Kenya Keriako Tobiko ameteua jopo la waendesha mashtaka kusaidia polisi katika uchunguzi wa kifo cha Mutula Kilonzo.

Friday, April 26, 2013

Lipumba 'aisigina' Chadema bungeni

Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa  na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza jijini Dar es Salaam  jana,  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya.
“Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni  na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema kambi rasmi ya upinzani pia imeshindwa kulinda utaratibu mzuri wa kutetea masilahi ya umma bila jazba na hoja zenye mashiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipokuwa ikiongozwa na CUF, Kiongozi huyo   alisema kambi ya upinzani inapaswa ijipange upya kwa utaratibu na mikakati mizuri ya kuteta hoja za wananchi bila kuyumbishwa na wabunge wa CCM.
“Bunge usiwe uwanja wa kuonyesha mbwembwe za chama bali uwe uwanja wa kutetea haki za wananchi, wabunge wanapaswa wabadilishe mitazamo ya kuona bungeni ni sehemu ya kujionyesha kisiasa na chama chako kinafanya nini nje ya Bunge,” alisema Lipumba.
Alisema  viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilika kuhusu namna ya kutoa majibu bungeni.
Profesa Lipumba alisema   mawaziri wengi wanakuwa wakitoa majibu mepesi katika maswali ya msingi yanayoulizwa na wabunge wa upinzani.
Alisema Bunge linatumia muda na pesa za walipakodi vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwa na ubishi usiokuwa  na tija, kutoleana matusi na wengine kuingilia hoja za wenzao bila sababu  za msingi.
Profesa Lipumba pia alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda amepoteza uwezo wa kuliongoza Bunge.

Wizara yashtushwa baa zinazojengwa maeneo ya shule

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeziagiza bodi na kamati za shule nchini kupitia upya mikataba iliyoingiwa kati ya shule na wafanyabiashara waliojenga maduka, baa zikamo nyumba za kulala wageni kwenye uzio wa shule.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Elimu, Kassim Majaliwa, alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One Sterio.

Majaliwa alisema kuruhusu ujenzi wa baa, maduka na nyumba za kulala wageni kwenye uzio wa shule kunaleta athari kwa wanafunzi kimasomo, hivyo kamati za shule na bodi ziangalie upya mikataba hiyo ikiwezekana isitishwe.

Alisema serikali imeshatoa waraka kwa wakurugenzi wa halmashauri kusimamia suala hilo na kwamba mkurugenzi atakayeshindwa kufanya hivyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Tumeshatoa waraka kwa wakurugenzi wasimamie suala la upitiaji wa mikataba hiyo na kwa mkurugenzi atakayeshindwa kufanya hivyo itabidi tumchukulie hatua kama atakuwa ameshindwa kuwajibisha viongozi wa shule husika,” alisema Majaliwa.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tatizo la baadhi ya viongozi wa shule kwa kushirikiana na bodi na kamati za shule kuingia mikataba na wafanyabiashara  ambao wanajenga maduka na baa katika uzio wa shule kwa lengo la kujipatia fedha bila kujali athari wanazoweza kupata wanafunzi.

Waziri Maghembe hoi

                                                     Bajeti yake yaondolewa bungeni
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiteta na Waziri wa Maji, Profesa Jumann Maghembe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma,Aprili 25,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesitisha mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Jumanne Maghembe, Jumatano wiki hii kutokana na karibu ya wabunge wote waliopata fursa ya kuchangia juzi na jana kutoiunga mkono.
 Kutokana na hali hiyo, Spika Makinda ameipa serikali siku tano, kuanzia jana kuhakikisha inapeleka bungeni majibu ya uhakika kuhusiana na tatizo la ufinyu wa bajeti hiyo lililosababisha wabunge kuipinga. Uamuzi wa Spika Makinda umechukuliwa saa chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kusema anaweza kuliomba Bunge
kupata fursa ya kuangalia namna serikali itakavyoweza kuboresha baadhi ya maeneo katika bajeti hiyo kutokana na maoni na ushauri uliotolewa na wabunge.
Pinda alisema hayo wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, bungeni jana.
 Katika swali lake la msingi, Mbowe, ambaye ni Mbunge wa Hai, alisema wabunge walio wengi wamelalamika kuwa hazikukokotolewa fedha za kutosha katika kukabiliana na tatizo la maji nchini.
 Hivyo, akahoji kwanini serikali isiondoe bajeti hiyo na kwenda kuifumua upya ili kutafuta fedha kwa ajili ya kuwezesha Watanzania kupata maji?
 Wabunge hao, ambao wengi wao ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walipinga bajeti hiyo, wakisema ni finyu, ambayo haiwezi kukidhi mahitaji makubwa na ya muda mrefu ya maji yaliyoko nchini kote, hususan maeneo ya vijijini.
 Katika bajeti hiyo, Waziri Maghembe ameliomba Bunge liidhinishe Sh. 398,395,874,000 kwa ajili ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka huo wa fedha.
 Mjadala huo ulitarajiwa kuhitimishwa jana jioni. Hata hivyo, kutokana na wabunge hao kuendelea kutoiunga mkono katika kikao cha Bunge cha jana asubuhi, Spika Makinda, aliamua kusitisha mjadala kuendelea, akisema amefikia uamuzi huo baada ya kuona bajeti hiyo ikipingwa na wabunge wengi.
Aliiagiza Kamati ya Bajeti, Wizara na Maji na Hazina, kukutana ili kuangalia namna watakavyolipatia ufumbuzi tatizo la ufinyu wa bajeti hiyo linalolalamikiwa na wabunge.
 Pia aliitaka serikali kuhakikisha inapeleka majibu ya uhakika bungeni Jumatatu ijayo.
 Miongoni mwa wabunge waliochangia mjadala huo na kupinga ni  Gosbert Blandes (Karagwe-CCM) akipinga kutotekelezwa kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kupeleka maji Karagwe.
 Alisema anasikitishwa kuona Sh. bilioni 30 zimetengwa kwa ajili ya upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Mwanga anakotoka Waziri Maghembe, lakini ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kupeleka maji katika Wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera, ambayo haihitaji fedha nyingi, hadi sasa haijatekelezwa.
Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, alisema tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama limesababisha watoto katika baadhi ya Kata za jimboni mwake; kama Ndeisinyai na Shambalai, kupinda miguu.
 Kutokana na hali hiyo, alishauri fedha za posho zilizotengwa kwa ajili ya vinywaji katika wizara hiyo ziondolewe na kupelekwa kusaidia katika miradi ya maji.
Mbunge wa Mwibara (CCM), Alphaxard Lugola, alisema bajeti ya wizara hiyo ni sawa na mchezo wa karata tatu, ambao Watanzania wanaliwa kwa kutumia karata ya rangi nyekundu, hivyo haoni sababu ya kuiunga mkono, kwani imesheheni miradi isiyotekelezeka.
 Alisema kuna upendeleo unaofanywa na serikali kwa mawaziri katika masuala ya maendeleo, hivyo akaomba pia wabunge nao wapewe upendeleo huo.
 Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Clara Mwituka, alisema kama kuna upendeleo, ambao mawaziri wanafanyiana, basi anaomba pia ufanywe katika Jimbo la Newala linalowakilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, kwani kuna tatizo kubwa la ukosefu wa maji.
 “Kuna maeneo hakuna maji hata ya kunawa uso,” alisema Mwituka.
 Mbunge wa Longido (CCM), Michael Lekule Laizer, alisema kutokana na tatizo la ukosefu wa maji, katika Wilaya ya Longido imefikia hatua baadhi ya familia wanapotaka kuoga wanapeana zamu.
 “Leo baba akioga kesho mama,” alisema Laizer na kuonya kuwa kama itafika mwaka 2015 maji yakaendelea kukosekana hajui nini kitakachotokea. Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambari Nywangwine, alisema haungi mkono bajeti hiyo kwa sababu jimboni kwake wananchi hawaogi kabisa kutokana na kutokuwa na maji.
 Alisema ni aibu  kwa nchi kama Tanzania, ambayo imesheheni mito na maziwa, lakini bado inakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa maji, hivyo akamtaka Pinda kuhakikisha usiku wa kuamkia jana anatafuta fedha ili kupatia ufumbuzi.
Nywangwine alisema ni aibu kuona nchini Kenya maji yanamwagika na Tanzania ikiambulia aibu ya kuyakosa.
  Alisema maji yanayopatikana na kutumiwa na wananchi ni yale yanayofanana na ugoro au juisi, huku wakiwa wamesheheni maziwa na mito, lakini hayawanufaishi hata kidogo.
 Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby, alisema kama ambavyo mwaka jana hakuunga mkono bajeti ya wizara hiyo, mwaka huu pia hataiunga mkono na kwamba, atapeleka hoja binafsi bungeni kuhakikisha wataalamu wote katika Wizara ya Maji wanaondoka.
 “Kuna watu walithubutu wakafanikiwa kama Mheshimiwa Lowassa katika mradi wa Ziwa Victoria. Hivi kweli tunajali kuwa maji ni uhai?” alihoji Shabiby.
 Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrodi Mkono, alisema haungi mkono bajeti hiyo kwa kuwa ni muda mrefu sasa amekuwa akisimama bungeni na kupiga kelele kuhusu tatizo la maji katika maeneo mengi jimboni kwake, lakini hakuna linalotekelezwa.
 “Waasisi wa taifa waliweka msingi wa kupata maji. Ahadi ya tangu mwaka 1974 haijatekelezwa na kila siku nasimama. Kwanini niunge mkono hoja?  Sioni sababu. Miaka 12 wananchi wangu wanalia kwa maji. Kwa nini niunge mkono hoja hii? Sioni sababu,” alisema Mkono.
 Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, alisema anaungana na wabunge waliokataa kuunga mkono bajeti hiyo, kutokana na fedha zilizotengwa kutokidhi mahitaji ya upatikanaji wa maji.
 Alisema licha ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2005-2010 na 2010-2015 kuwaahidi Watanzania kuwa ifikapo 2010 asilimia 65 vijijini na asilimia 90 mijini watakuwa na maji safi na salama, hakuna lolote lililotekelezwa.
 Hivyo, akasema haamini kabisa kama ahadi iliyotolewa na Pinda, bungeni jana itatekelezwa.
 Alisema licha ya Rais Kikwete kuahidi tatizo la maji kwamba, litakuwa historia, hakuna lolote lililotekelezwa, hivyo akasema iwapo ufumbuzi hautapatikana, wananchi wa Dar es Salaam wataendelea kuandamana kwenda ofisini kwa Waziri Maghembe.
 Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Rose Kamili Sukum, ambaye naye alikataa kuunga mkono bajeti hiyo, alisema hawezi kusema maji yasipelekwe katika Wilaya ya Mwanga wala Same, lakini akasema utaratibu wa kuyapeleka katika wilaya hizo haukuwa sahihi, kwani fedha zilizopelekwa huko ni nyingi, hivyo akataka zigawanywe na kupelekwa katika maeneo mengine, ambako tatizo la maji pia lipo.
 Alisema kwenye hotuba ya Waziri Maghembe aliahidi kukamilika kwa visima vitano katika kila kijiji, lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika.
 Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari, alisema atamshangaa mbunge atakayeunga mkono bajeti hiyo na kuwaomba wananchi kutomrudisha bungeni.
 Alisema Waziri Maghembe amelidanganya Bunge kwa kusema kuna Kijiji cha Kasanumba kilichopelekewa maji wakati hakipo, hivyo akawaomba wabunge wa CCM kuikataa bajeti hiyo.
 Mbunge wa Manyoni Mashariki (CCM), John Chiligati, alisema anakubaliana na wabunge wengine kuhusu tatizo la maji kwamba, ni kubwa sana nchini, hivyo akashauri ufadhili wa Benki ya Dunia (WB) kutotegemewa sana.
 Mbunge wa Mbeya Vijijini (CCM), Mchungaji Luckson Mwanjale, alisema tatizo la maji ni kubwa na kwamba hakuna mbunge anayeweza kusema jimboni kwake ni salama.
 Dk. Christina Ishengoma (Viti Maalum-CCM) alisema maji safi na salama bado ni changamoto kubwa sana, hasa vijijini, hivyo akaishauri serikali ijipange kutatua tatizo hilo.
 Mbunge wa Nyang’hwale (CCM), Hussein Amar, alisema tatizo la maji limesababisha kifo jimboni kwake kufuatia ugomvi uliozuka baina ya wanawake wawili walipokuwa wakiyagombea.
 Alisema tatizo hilo pia limesababisha kukithiri kwa mimba, ndoa kuvunjika na wanafunzi kushindwa mitihani.
 Amar alisema kwa muda mrefu amekuwa akipigia kelele tatizo la maji bila ufumbuzi, na kwamba jimbo lake lina matatizo makubwa ya maji, huku maji yakiwa yamewazunguka, hivyo akasema haoni sababu ya kuunga mkono bajeti hiyo.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Stella Manyanya, alisema hawezi kuwa kinyume cha wabunge waliopiga kelele kuhusu tatizo la maji.
Alisema hata ukiongea na wananchi nini kipaumbele chao, wanaume watakuambia elimu, lakini wanawake watakuambia maji na afya na kuwa katika maeneo ya vijijini, hata katika zahanati, ambako kinamama wanakojifungulia, hakuna maji safi na salama.
Mbunge wa Manyoni Magharibi (CCM), John Lwanji, alisema Tanzania imepata misaada mingi kutoka kwa wafadhili katika eneo la maji, lakini tatizo hilo bado ni sugu.
 Lwanji alisema tangu mwaka 1961 tatizo la upatikanaji wa maji bado limekuwa sugu, hivyo akasema haungi mkono bajeti hiyo.
 Mbunge wa Solwa (CCM), Ahmed Ali Salum, alisema haungi mkono bajeti hiyo na kushauri kuvunjwa kwa vyombo vyote vinavyosimamia maji na kuunda chombo kimoja, mkoani Shinyanga.

 WAZIRI MKUU ASINYWE MAJI YA CHUPA
Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde, alisema kuanzia sasa katika ziara zote za viongozi wakuu wa serikali; akiwamo Waziri Mkuu, wasiandaliwe maji ya kunywa ya chupa, bali yale yanayotumiwa na wananchi wa kawaida na kusema haungi mkono bajeti hiyo.
 Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse, alisema miradi ya maji inayofadhiliwa na WB iko hoi na haiwezi kuwasaidia Watanzania, kwani sehemu yake kubwa imekuwa ikiliwa na baadhi ya wakandarasi, ambao alisema wanapaswa kuogopwa kama ukoma.
 AnnaMaryStella Mallac (Viti Maalum-Chadema), alisema anashangazwa kuona kufikia leo miaka 50 ya Uhuru, kinamama wanachota maji kwa kutumia kichwa, kwa kuinama na kutumia maji yanayofanana na togwa.
 Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka miwili, wabunge kukataa kuunga mkono bajeti za serikali zinazowasilishwa bungeni.
 Mara ya kwanza, wabunge waliikataa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, William Ngeleja, mwaka juzi, kwa maelezo kwamba, serikali ilikosa umakini katika kuiandaa.
 Wiki mbili baadaye, wabunge waliikataa pia bajeti ya Wizara ya Uchukuzi iliyowasilishwa na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Omar Nundu, kwa maelezo kwamba, ilikuwa ni ndogo isiyokidhi mahitaji ya kukarabati miundombinu ya reli, ambayo hutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.

Kibali cha kunikamata kitatoka kwa Spika: Lema

Jeshi  la Polisi linamsaka Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa tuhuma za kuhusika katika vurugu zilizotokea juzi katika chuo cha Uhasibu Mkoani Arusha (IAA) na kusababisha chuo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Ibrahim Kilongo, aliwaaambia waandishi habari kuwa jeshi hilo limetoa ilani kwa mbunge huyo kujisalimisha polisi haraka.
Wakati polisi wakisema hayo, Lema ameeleza kushangazwa na hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutoa amri ya kumkamata.
Alisema kibali cha kukamatwa kwake ni lazima kitoke kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Lema aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi jijini hapa na kuwa  atakamatwa ikiwa Spika Makinda atatoa kibali cha kukamatwa kwani yeye ni mbunge halali wa Arusha Mjini.
Pia aliwapa pole wanafunzi kwa msiba wa mwanafunzi mwenzao kisha kuwapa pole wanafunzi wengine waliokumbwa na kadhia ya kupigwa mabomu juzi eneo la chuo wakati wakidai haki zao za msingi ikiwamo kuhoji matukio ya vifo vya wanafunzi wenzao vinavyotokea mara kwa mara chuoni hapo.
Hata hivyo, kamanda Kilongo alisema: “Tunamtaka popote alipo afike mwenyewe  polisi na bado tunaendelea kumtafuta popote alipo, ni muhimu afike tufanye naye mahojiano kuhusu yaliyotokea katika chuo cha uhasibu."
Lema anatuhumiwa kuhusika katika vurugu zilizopekea kudhalilishwa na kuzomewa kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Mara baada ya kutulizwa kwa vurugu hizo, Mulongo aliliagiza jeshi la polisi kumkamata Mbunge huyo kwa kile kilicholezwa kuwa ni kumhusisha na vurugu zilizotokea chuoni hapo juzi.
Katika tukio hilo lililosababisha mabomu ya machozi kurindima kwa kwa muda chuoni hapo, Mulongo alijikuta akizomewa baada ya kushindwa kuhutubia mamia ya wanafunzi.
Awali, Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu jijini Arusha, Faraji Kasidi, alisema chuo hicho kimebeba jukumu la kuusafirisha mwili wa mwanafunzi Henry Kago (22) na kuupeleka nyumbani kwao Iringa kwa ajili ya mazishi.

Machinjio ya Ukonga yafungwa kwa uchafu

Mamilioni ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam huenda wakakabiliwa na uhaba wa kitoweo kufuatia hatua ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (Nemc) kuyafunga machinjio ya Ukonga.
Nemc imeyafunga machinjio hayo yaliyoko eneo la Ukonga Mazizini katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, baada ya kubaini kuwa yanaendesha shughuli zake katika mazingira machafu yanayohatarisha afya za walaji wa nyama.
Machinjio hayo ambayo ng’ombe kati ya 350 hadi 500 huchinjiwa hapo, yamefungwa baada ya maofisa wa Nemc wakiongozwa na Afisa Mwandamizi Mkuu wa baraza hilo, Lucy Lugusha, kufanya ziara ya ukaguzi wa kushtukiza katika eneo hilo.
Maofisa hao walifika katika machinjio hayo jana majira ya asubuhi  na kumkuta Afisa Mfawidhi wa Machinjio ya Ukonga, Pradisius Mbita, ambaye pia ni mtumishi wa Manispaa ya Ilala akiwa katika ofisi za wamiliki wa machinjio hayo.
Kabla ya kuanza ukaguzi, Mbita aliulizwa na maofisa wa Nemc kuna mahusiano gani kati ya Manispaa ya Ilala na machinjio hayo na kueleza kuwa manispaa imekuwa ikikusanya ushuru tu na kwamba kuna watumishi ambao wameteuliwa rasmi kufanya kazi katika machinjio hayo.
Mbita alisema watumishi wa manispaa ambao wanafanya kazi katika machinjio hayo yaliyoanzishwa tangu mwaka 1972, ni pamoja na yeye mwenyewe (Mbita) kama mkaguzi wa nyama, afisa afya, mhasibu na mlinzi.
Alipoulizwa kama machinjio hayo yana leseni, Mbita alisema manispaa haina uhakika kama kuna leseni yoyote iliyokatwa kwa ajili ya kuendesha machinjio hayo.
Baada ya maofisa hao wa Nemc kuendelea kumhoji Mbita, alijitetea kuwa masuala mengine ni ya ndani zaidi, hivyo ni bora akamwita mmoja wa wamiliki wa machinjio hayo ayajibu.
Baada ya nusu saa, mmoja wamiliki wa machinjio hayo, Philemon Bereko, aliwasili eneo hilo na kueleza kuwa machinjio hayo yanamilikiwa na watu watatu ambao ni Philemon Bilia, Anthony Bilia na yeye mwenyewe (Bereko).
Bereko ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wachinja Nyama, alisema kama ilivyo kwa Nemc, nao wamekuwa wakipata malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu mazingira machafu ya machinjio hayo.
Alisema Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala alishawahi kufika katika machinjio hayo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi na aliahidi kuwa halmashauri itatoa fedha zinazotokana na ushuru unaotozwa katika machinjio hayo kwa ajili ya kusaidia kuboresha mazingira.
Bereko alisema tangu Mkurugenzi wa Manispaa alipondolewa, ahadi hiyo imekwama kutekelezwa badala yake halmashauri hiyo imekuwa ikiendelea kukusanya ushuru wake wa Sh. 2,500 kwa kila ng’ombe mmoja anayechinjwa katika machinjio hayo.
“Halmashauri wameweka hadi mhasibu wao hapa, kila ng’ombe anayechinjwa ushuru unaotozwa ni Sh. 2,000 na Sh. 500 ni za mkaguzi wa nyama ambaye anatoka halmashauri, mazingira haya wanayaona na mvua ikinyesha hali inakuwa mbaya sana,” alisema Bereko.
Hata hivyo, alipoulizwa inakuwaje machinjio hayo yaendeshwe na watu binafsi halafu halmashauri ichangie kuyaboresha, alisema hayo ni katika makubaliano yao na kwamba kinachomsikitisha ni hatua ya halmashauri kuweka mhasibu katika machinjio hayo wakati katika maeneo mengine hakuna utaratibu kama huo.
Baada ya kikao hicho, maofisa wa Nemc walianza ukaguzi wa machinjio hayo na kujionea hali ya kutisha ya uchafu wa mazingira katika eneo hilo ambayo yanahatarisha usalama kwa mlaji wa nyama inayochinjwa.
Miongoni mwa mambo yaliyobainika ni mamia ya tani za kinyesi cha ng’ombe ambacho kimerundikana, mifereji ya kupitishia maji yaliyochanganyika na damu kutitirika katika mtaro wa maji unaounganishwa katika mto ambao unaingiza maji kwenye Bahari ya Hindi na kupita kando kando ya makazi ya watu.
Pia mazizi ya kuhifadhi ng’ombe kabla hazijachinjwa yamejaa maji machafu yaliyochanganyika na kinyesi kiasi kwamba ng’ombe akiwa humo huzama miguu.
Maofisa wa Nemc walipofika eneo la machinjio na kufanya ukaguzi saa 5:45 asubuhi, hapakuwapo na nyama, lakini nzi na funza walionekana kutokana kukithiri kwa uchafu.
Baada ya kujionea hali hiyo, Afisa Mwandamizi Mkuu wa Nemc, Lugusha, alitoa agizo la kusitisha shughuli za uchinjaji nyama katika machinjio hayo hadi hapo mazingira ya usafi yatakapoboreshwa.
“Mchana wa leo (jana), tutakuletea barua rasmi ya kukutaka usitishe shughuli za kuchinja nyama katika machinjio haya na nakala tutapeleka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,” alisema Lugusha.
Hata hivyo, Bereko alijitetea kwamba apewe muda wa mwezi mmoja au wiki moja arekebishe mazingira hayo, lakini ombi lake lilikataliwa na maofisa wa Nemc ambao walimweleza kuwa aanze kazi ya kuboresha mazingira na akimaliza ndipo ataruhusiwa kuendelea na uchinjaji.

HISTORIA YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Historia, sababu na Hati za
Muungano
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja 27/05/2009

HISTORIA YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja). Tanganyika ilikuwa ni mwendelezo wa koloni la Ujerumani, utawala wa Waingereza kwa Mamlaka ya Umoja wa Mataifa, Himaya ya Umoja wa Mataifa chini ya utawala wa Uingereza na mwisho Taifa huru kuanzia mwaka 1961 ndani ya nchi za Jumuiya ya Madola.
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkataba huu wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar.
Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam na kubadilishana Hati za Muungano. Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 4 kwamba: “Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano)
2 Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadae mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964. Watanganyika kama ilivyokuwa kwa wananchi wa nchi nyingine za kiafrika, hawakukubaliana hata kidogo na utawala wa kikoloni. Tangu mwanzo waliwapinga na kupigana na wavamizi wa kikoloni, upinzani mkubwa ukionyeshwa na Wasambaa wakiongozwa na Kimweri dhidi ya Wajerumani, Wahehe wakiongozwa na Mkwawa kupigana vichungu na virefu dhidi ya Wajerumani na wakati wa vita vya Maji Maji chini ya uongozi wa Kinjekitile, Mputa na Kibasila. Kukosekana kwa umoja kati ya wapigania uhuru hawa wa mwanzo na uimara wa majeshi ya wakoloni na silaha bora za moto kulidhoofisha mapambano haya ya uhuru na kusababisha hasara kubwa na kupoteza maisha ya watu.
Kama ilivyokuwa kwenye makoloni mengi ya Kiafrika, hisia za Utaifa ziliendelea kuimarika katika Tanganyika baada ya mwaka 1945.
Alama za utaifa zilishaanza kuonekana punde baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kwa kuanzishwa kwa vyama mbalimbali vya Waafrika kwa upande wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa upande wa Tanganyika, African Association ilianzishwa mwaka 1929 kama kikundi cha mijadala baina ya wasomi na ilipofika mwaka 1948 chama hiki kikawa Tanganyika African Association (TAA).
Baada ya vita ya Pili ya Dunia, wanachama wa Tanganyika African Association
3 (TAA) waliendeleza wimbi la utaifa.
Mwaka 1953 chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere, TAA ilitambuliwa kama chama cha siasa na kuelekea moja kwa moja kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954 iliyotumika kama chombo cha kisiasa cha watu katika kutoa vilio vyao vya kudai uhuru. Kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954, ulikuwa ndio mwanzo wa mbio za kupigania uhuru. Baada ya miaka saba ya mapambano ya kisiasa, Tanganyika ilikuwa huru chini ya chama cha TANU,kilichoimarishwa na vyama vya wafanyakazi na vya ushirika.
Kwa upande wa Zanzibar, chimbuko la Jumuiya ya Waafrika ilikuwa ni vilabu vya mpira wa miguu vilivyoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1930.
Ilipofika mwaka 1934, Jumuiya ya Waafrika ilianzishwa rasmi na kupewa jina la African Association (AA).
Baada ya vita ya pili ya dunia kama ilivyokuwa katika sehemu nyingine za dunia, kulikumbwa na uhaba mkubwa wa chakula, ubaguzi na mgawanyiko baina ya jamii.
Kutokana na matatizo hayo ya ubaguzi, kulianzishwa Jumuiya ya Washirazi (Shirazi Association) katika Visiwa vya Unguja na Pemba lengo likiwa ni kudai kupatiwa haki mbalimbali za kijamii na kulinda utambulisho wao. Kuundwa kwa chama cha ZNP (Zanzibar Nationalist Party) mwaka 1957, kulifanya viongozi wa Jumuiya ya Waafrika (African Association) na wale wa Shirazi Association waone umuhimu wa kushirikiana. Waligundua kuwa Serikali ya kikoloni na chama cha ZNP walishirikiana kuendeleza dhuluma dhidi ya Waafrika.
Viongozi hao waliona ulazima wa kuungana kuwa kitu kimoja kupigania uhuru. Hivyo, katika kutekeleza azma hiyo, Viongozi wa Jumuiya hizo walikutana na kukubaliana kuunganisha Shirazi Association na African Association mwaka 19574 na kuunda chama kilichoitwa Afro- Shirazi Union ambacho baadae kiliitwa Afro-Shirazi Party chini ya uongozi wa Sheikh Abeid Amani Karume.
Mwalimu Nyerere alishiriki katika mkutano huu. Ilikuwa tarehe 05 Desemba, 1957 hapo mtaa wa Mwembekisonge Unguja.
Kati ya mwaka 1957 mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza na mwishoni mwa mwaka 1963, kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964, Zanzibar ilitawaliwa na vuguvugu na mivutano mikali ya kisiasa.
Mapambano haya ya kisiasa yalikuwa kati ya Chama cha Afro-Shirazi kilichoungwa mkono na Waafrika na kile cha Zanzibar Nationalist Party kilichoungwa mkono na Wakoloni, Sultani pamoja na jamii ya Waarabu.
Chama cha ZNP baada ya kushindwa uchaguzi, kilianzisha kampeni za kushawishi wenye mashamba na mabepari wengine wenye kumiliki njia kuu za uchumi, kuwafukuza kazi au kutowaajiri wafuasi wa ASP.
Halikadhalika, Chama cha ZNP kiliwatafutia kazi na kuwabakisha mashambani Waafrika wote waliokubali kukiungamkono.  Wakati wa mvutano huo wa kisiasa kati ya ASP na ZNP  ikipambamoto, kulijitokeza tofauti miongoni mwa viongozi wa ASP.
Tofauti hizo zilichangiwa na uroho wa madaraka, ubinafsi na kutokuwa na msimamo imara miongoni mwa baadhi ya viongozi wachama hicho.
Halikadhalika Serikali ya Sultani nayo ilichochea migogoro hiyo ili ijinufaishe kisiasa. Migogoro hiyo ilipelekea kujitoa kwa baadhi ya Viongozi wa ASP ambao walifanya mkutano na baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa ASP huko Pemba Novemba, 1959 na kukubaliana kuanzisha Chama kipya cha siasa cha Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP) na Sheikh Muhammed Shamte
kuwa Mwenyekiti.
Wakati vyama vya ASP, ZNP na ZPPP vikiwa katika malumbano makali ya kisiasa, Serikali ya Kikoloni ilifanya 5 matayarisho ya uchaguzi wa pili. Uchaguzi ulifanyika tarehe 16 Januari, 1961 na siku moja kabla ya uchaguzi huo Serikali ilitangaza kuwa chama kitakachoshinda kitaunda Serikali na Wizara zote zitakuwa chini yake.
Katika uchaguzi huo ASP ilishinda kwa kupata viti 10, ZNP kilipata viti 9 na chama cha ZPPP kilipata viti 3.
Kutokana na kuenea kwa chuki za kisiasa miongoni mwa Wazanzibari, Vyama vikuu vya kisiasa vilifikia muafaka wa kumaliza hali hiyo.
Hatahivyo, ASP haikufikisha zaidi ya nusu ya kura na hivyo haikuweza kuunda Serikali.
Hivyo njia pekee iliyobakia ilikuwa ni kuishauri ZPPP ichanganye viti vyake na chama kimoja kati ya ASP na ZNP.
ZPPP na ZNP viliungana. Hatahivyo, iliamuliwa kuwa iundwe Serikali ya muda na kusubiri uchaguzi mwingine uliopangwa kufanyika mwezi Juni, 1961. Waingereza walitoa uhuru kwa Serikali ya Mseto ya ZNP/ ZPPP ya Waziri Mkuu Muhammed Shamte.
Chini ya ushauri wa Waingereza, Shamte aliwatenga ndani ya Serikali yake baadhi ya viongozi wa ZNP wenye msimamo wa Kikomunisti wakiongozwa na Abdulrahaman Babu, na hivyo kutokea kutofautiana kwa baadhi ya viongozi wa ZNP na Serikali ya ZNP/ZPPP.
Baada ya kutengwa na Serikali hiyo walijitoa ZNP na kuanzisha Chama cha Umma. Chama hicho kilivunjwa mara tu baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na hapo viongozi na wafuasi wake walijiunga na Serikali ya ASP chini ya uongozi wa Abeid Karume.
Zanzibar ilikuwa na wakati mgumu katika kupigania uhuru. Waingereza walijikita zaidi kwa madhumuni ya kibiashara na kwa nia ya kukomesha biashara ya utumwa. Hii ilikuwa ni kwasababu, walitaka nguvukazi rahisi ambayo ilikuwa inapotea kwa kufanywa 6 watumwa kwa uzalishaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vyao Ulaya, halikadhalika kutokana na Mapinduzi ya Viwanda Ulaya yalisababisha Waingereza kuja kutafuta soko kwa ajili ya bidhaa zao.

Waingereza walifikia makubaliano na Sultani mwaka 1822 ili kukomesha biashara ya utumwa, lakini ilichukua zaidi ya miaka 50 hadi utumwa kutokomezwa. Makubaliano ya Waingereza na Wajerumani ya mwaka 1890 yalifanya Zanzibar kuwa koloni la Waingereza ambao walimshirikisha Sultani katika utawala wao.
Waingereza waliainzisha ubaguzi wa rangi Zanzibar kwa Wazungu na Waarabu kupendelewa kuwa tabaka la juu na Waafrika la chini. Waingereza walifanya Zanzibar kuwa ni koloni la Waarabu na ilipofika Desemba 1963, Sultani alipewa mamlaka kamili ya kutawala Zanzibar.
Tarehe 12 Januari 1964, aliyekuwa Sultani wa Zanzibar, Jamshid bin Abdulla, aling’olewa madarakani katika Mapinduzi yaliyokuwa yameandaliwa kwa usiri, ustadi na ujasiri mkubwa wa Wanamapinduzi wa Afro-Shirazi Party (ASP) na Jamhuri ikatangazwa.

Muundo wa Muungano wa Tanzania kama ulivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, una vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji ambavyo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ambavyo ni Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma ambavyo ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 7 inashughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoshughulikia mambo yote yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Zanzibar.

Muungano wa Tanzania ni tukio la nadharia iliyotafsiriwa katika vitendo, kwani kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ni hatua ya watu walio wakweli. Ni ushahidi unaojitosheleza kuwa wananchi wa Tanganyika na wa Zanzibar wakiongozwa na viongozi wao wa mapambano ya kudai uhuru, walitoa kauli zilizokuwa zikimaanisha walichofikiri na kuazimia na wala siyo kwa sababu ya kusombwa na jazba za kisiasa.

SABABU ZA KUWEPO KWA MUUNGANO
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na
sababu zifuatazo:-
1. Kuwepo kwa mahusiano ya karibu kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile udugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususan baina ya TANU na ASP.
2. Moyo wa kuwa na Muungano wa Afrika hususan kwa kuanzia na Shirikisho la Afrika Mashariki. Hata kabla ya uhuru wa Tanganyika, Mwalimu Nyerere pamoja na viongozi wengine 8 waliokuwa wakipigania utaifa katika ukanda wa Afrika Mashariki walikuwa na matarajio ya kuwa na Muungano wa Afrika.

Mwalimu Nyerere binafsi alipendelea uwepo Muungano wa Afrika kwa kuanzia na Mashirikisho ya kikanda.
Baada ya kushauriana na viongozi mbalimbali wa iliyokuwa Jumuiya ya Wapigania Uhuru wa Afrika Mashariki na Kati (Pan- African Freedom Movement for East and Central Africa - PAFMECA) Mwalimu Nyerere alitoa tamko wakati wa mkutano wa nchi huru za Afrika uliofanyika Addis Ababa mwaka 1960 kwamba;
“Wengi wetu tunakubaliana bila kikwazo kwamba Shirikisho la Afrika Mashariki litakuwa ni jambo zuri.
Tumesema na ni kweli kwamba mipaka inayotenganisha nchi zetu imewekwa na mabeberu na sio sisi wenyewe na kwamba tusikubali itumike dhidi ya umoja wetu…lazima tuzisumbue ofisi za wakoloni kwa nia si ya kudai uhuru wa Tanganyika, kisha Kenya, na Uganda halafu Zanzibar lakini kwa nia ya kutaka uhuru wa Afrika Mashariki kama Muungano mmoja wa Kisiasa”.(imeripotiwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard, Novemba 1964) Mapinduzi ya Zanzibar mnamo mwezi Januari, 1964 yalifanyika wakati Mwalimu Nyerere akiwa ameshachoshwa na kukatishwa tamaa na mazungumzo ya Shirikisho la Afrika Mashariki.
Mapinduzi haya yaliiweka madarakani Serikali ya chama cha ASP kilichokuwa na mahusiano ya karibu na TANU kwa upande wa Tanganyika. Kwa uhakika zaidi, upo mchanganyiko wa sababu mbalimbali za Muungano huu kama vile historia za nchi hizi mbili, ukaribu 9 wa nchi hizi mbili,muingiliano wa kijamii, ushirikiano wa kibiashara, ushirikiano madhubuti na wa muda mrefu wa kisiasa baina ya TANU na ASP, ushirikiano na urafiki wa muda mrefu kati ya watu, viongozi, na wakati wa harakati za utaifa uliopelekea uhuru wa nchi hizo mbili, sababu za kiusalama n.k.

HATI YA MAKUBALIANO YA MUUNGANO
Msingi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za mwaka 1964. Hati za Muungano zilitiwa saini na waasisi wa Muungano tarehe 22 Aprili, 1964, na hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mapatano ya Muungano yaliunganisha mataifa mawili yaani Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar na kuweka Taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa misingi ya Katiba na misingi inayotambulika Kimataifa. Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lilibadilishwa baadae na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya Muungano, Mwalimu J. K. Nyerere alikuwa Rais wa kwanza na Sheikh Abeid Amani Karume, alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tarehe 26 Aprili, 1964 Bunge la Tanganyika lilipitisha Sheria za Muungano. Halikadhalika Sheria hizi zilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar. Sheria hizi za Muungano zilithibitisha Hati za Muungano, zilitaja Rais na Makamu wa Rais, zilitaja Muundo wa Muungano na Katiba ya Muungano. Mnamo tarehe 27 Aprili 1964, 10 waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba (7) wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ni: Sheikh Abeid Amani Karume, Bw. Kassim Abdala Hanga, Bw.
Abdulrahaman Mohamed Babu, Sheikh Hassan Nassor Moyo, Sheikh Aboud Jumbe, Sheikh Hasnu Makame na Sheikh Idris Abdul Wakil. Wote hawa walifanya Mawaziri wa Serikali ya
Muungano.
Kati ya Viongozi hawa wawili wako hai hadi sasa. Nao ni Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo. Kabla ya siku ya Muungano, kulikuwa na Katiba mbili; Katiba ya Tanganyika ya mwaka 1962 na upande wa Zanzibar kulikuwa na Amri za Katiba (Constitution decrees). Katiba ya Tanganyika baada ya kufanyiwa marekebisho iliendelea kutumika kama Katiba ya Muungano wakati ule wa mpito, kuanzia tulipoungana hadi ilipopitishwa Katiba ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano na Sheria za Muungano. Aidha, marekebisho hayo yalimtaja Rais wa Zanzibar kuwa ni Makamu wa kwanza wa Rais, akiwa ni msaidizi wa Rais kwa masuala yote ya kiutawala kwa upande wa Zanzibar, na Waziri Mkuu kuwa ni Makamu wa Pili wa Rais ambaye atamsaidia Rais kwa masuala yahusuyo upande wa Tanganyika na kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni.

Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliainisha mambo kumi na moja (11) ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano chini ya usimamizi wa Serikali ya Muungano.
Mambo hayo ni; 11
· Katiba na Serikali ya Muungano
· Mambo ya Nchi za Nje
· Ulinzi
· Polisi
· Mamlaka juu ya mambo yanohusika na hali ya hatari
· Uraia
· Uhamiaji
· Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje
· Utumishi katka Serikali ya Jamhuri ya Muungano
· Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
· Bandari mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

Katiba ya muda ya mwaka 1965 ilianiainisha utawala wa Serikali ya mfumo wa chama kimoja, TANU kwa Bara na ASP kwa Zanzibar. Katiba hii, ilizingatia misingi ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Katiba ya muda ya mwaka 1965 iliainisha Serikali mbili, Uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge la Muungano na uongozi wa Serikali ya Zanzibar.
Serikali ya Muungano ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano na mambo yote yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
12
KUONGEZEKA KWA MAMBO YA MUUNGANO
Mambo ya Muungano yaliongezeka kutoka kumi na moja (11) hadi ishirini na mbili (22) kutokana na mahitaji ya ndani ya wananchi yaliyolenga kuunganika kwa mambo mengi zaidi pamoja na mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea kutokea ulimwenguni baada ya Muungano.

Mwaka 1965, jambo la kumi na mbili linalohusu Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yoyote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni liliongezeka chini ya Katiba ya muda ya mwaka 1965. Sababu kubwa ilikuwa ni kuwa na sarafu ya pamoja ya Tanzania baada ya Muungano, na kurahisisha usimamizi wa fedha za kigeni na mabenki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967, mambo matatu ya Muungano yaliongezwa, ambayo ni; Leseni za viwanda na takwimu; elimu ya juu; na usafiri na usafirishaji wa anga.

Mwaka 1968, mambo ya maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na ama ya petrol na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliongezwa kwenye orodha ya
mambo ya Muungano.
13
Aidha mambo ya Muungano yaliendelea kuongezeka hadi kufikia 21 kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977.
Mambo yote yaliyokuwa ya upande wa Tanganyika na Zanzibar yaliyokuwa yakisimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, yalikabidhiwa kwa Serikali ya Muungano.

Mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa siasa nchini suala la ishirini na mbili la uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo liliongezwa kwenye orodha ya mambo ya Muungano.
14