Sunday, May 5, 2013

Wanafunzi walia na Serikali, matokeo kufutwa

Uamuzi huo wa Serikali umetokana na matokeo mabaya ya mitihani hiyo yaliyosababisha zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi kupata sifuri. Uamuzi wa Serikali ulitolewa juzi mjini Dodoma ikiwa ni wiki kadhaa tangu ilipounda Tume iliyoongozwa na Profesa Sifuni Mchome kuchunguza matokeo hayo ili kupata ufumbuzi wa kudumu.
Wanafunzi hao waliomaliza katika shule mbalimbali nchini walizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti na kueleza mengi, lakini kubwa ni matukio ya kusikitisha ya wenzao walioamua kujiua baada ya kufeli, huku wakisisitiza kuwa pengine walifaulu lakini kutokana na mabadiliko ya ghafla na uzembe katika usahihishaji ndiyo chanzo cha vifo vya wenzao.
Lameck Mathias
Binafsi naona Serikali imechelewa sana kuchukua hatua hii kwa kuwa tangu matokeo yametoka hadi sasa wapo wanafunzi waliojiunga na vyuo mbalimbali nchini, wengine kuajiriwa.
Sasa kama wanafunzi hawa ambao tayari wameshajiingiza katika ajira au vyuoni Serikali itawasaidiaje kama matokeo mapya yakionyesha kuwa wamefaulu. Katika hili lazima wahusika wawajibishwe ili siku nyingine usitokee uzembe kama huu unaowatesa wanafunzi, wazazi.
Maimuna Kessy
Imeniuma sana, wanafunzi walifanya vibaya kwa sababu Serikali iliongeza wastani wa ufaulu bila kuwataarifu wanafunzi, shule, wazazi na hata wadau mbalimbali wa elimu.
Ingekuwa vyema kama wanafunzi tungeelezwa ukweli ili tujue na kujipanga kwa ajili ya kukabiliana na ongezeko hilo. Wengi tumeanza masomo ya kurudia mitihani na tumeshalipa ada, wamewasababishia wazazi wetu hasara, sidhani kama fedha hizo zitarudishwa.
Robert Mialo
Kitendo cha zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi kufeli kimetokana na Serikali kutokuwa na umakini wa kutosha katika utoaji wa uamuzi wake.
“Inakuwaje wastani wa ufaulu upandishwe bila wanafunzi kuelezwa, sasa kama ilikuwa upate wastani wa C sasa unapata D.”
Wapo wanafunzi waliojiua baada ya kufeli mitihani yao, sijui matokeo yakionyesha wamefaulu, Serikali itawaeleza nini wazazi wao?

2 comments:

Unknown said...

my name is abubakar mohamed. Am glad that the results are canceled because it was so hard to see my friend cried because of this shameful result.I give the govt much appreciation on what they decided to do, on the day when the result was out i was so worried because in our school only 19 student was pass the examination i was think that maybe i was not on the list but thanks to the almighty i was one of them but still i was not happy because all of ma friend was not in the list. We study very hard together at noon we took potatoes only and continue learning, we go home late together still we got nothing, its hurt for really i loosed my patient back there but thanks again to the govt for looking on this. Its me ABUBAKAR MOHAMED from frelimo Iringa

Unknown said...
This comment has been removed by the author.