Sunday, May 5, 2013
Shambulio jipya la utawala haramu wa Kizayuni huko Syria
Kwa mara nyingine duru mbalimbali za habari, zikiwemo za utawala haramu
wa Kizayuni wa Israel, zimetangaza habari ya utawala huo kufanya
mashambulizi nchini Syria. Shirika la Habari la Syria (SANA) limetangaza
leo kuwa, asubuhi ya leo kulisikika sauti ya miripuko kadhaa karibu na
eneo la Alhama lililoko katika viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo
Damascus. Taarifa za awali zilizotangazwa zinaeleza kuwa, kituo cha
utafiti kilichoko katika eneo la Jamraya na ambacho pia kilishambuliwa
na utawala huo katika miezi ya hivi karibuni, ni miongoni mwa maeneo
yaliyoshambuliwa leo na ndege za utawala wa haramu wa Kizayuni wa
Israel. Kituo cha habari cha Syria pia kimetangaza habari ya kutokea
miripuko katika maeneo tofauti ya mji wa Damascus. Inasemekana kwamba,
miripuko hiyo imetokea katika kambi ya jeshi la kikosi nambari nne
iliyoko katika eneo la Mount Qasioun na katika kituo cha utafiti cha
Jamraya. Aidha duru za habari zimetangaza habari ya kusikika sauti za
milipuko katika kikosi nambari 105 cha gadi ya rais wa Syria. Wakati huo
huo, vyombo vya habari vya Syria vimetangaza kuwa, kombora la kwanza
lililotupwa na ndege za utawala katili wa Kizayuni katika eneo la
Jamraya, lilikuwa na mada za urani khafifu. Miripuko, mashambulio na
ukiukaji wa hivi sasa wa anga ya Syria, unajiri katika hali ambayo,
mwezi Januari mwaka huu, ndege za kijeshi za Israel zilikishambulia pia
kituo cha utafiti cha Jamraya katika viunga vya mji mkuu wa Syria,
Damascus. Baadhi ya duru za kisiasa zimetangaza kuwa, mashambulizi mapya
ya Israel nchini Syria, yanabainisha wazi kuwa, utawala huo unaingilia
moja kwa moja mgogoro unaoendelea nchini humo na kwamba, makundi ya
kigaidi yanayofanya mauaji ya raia huko Syria hayawezi kukanusha
mahusiano yake ya moja kwa moja na njama hizo za Israel. Chanzo kimoja
cha habari pia kimesisitiza kuwa, mashambulizi ya anga ya ndege za
Kizayuni huko Damascus na ambayo yamefanyika baada ya kushindwa makundi
ya kigaidi yanayofadhiliwa na madola ya kigeni, kukabiliana na jeshi la
Syria, ni njama zenye lengo la kuandaa mazingira ya kuyapenyeza makundi
ya kigaidi mjini humo. Ushahidi wa hayo ni kuwa, muda mchache tu tangu
ya kufanyika mashambulizi hayo ya Wazayuni, jeshi la Syria lilifanikiwa
kufelisha njama za magaidi waliokuwa na nia ya kujipenya zaidi mjini
Damascus kwa ajili ya kufanya uharibifu na jinai nyenginezo. Kwa upande
wake Tony Cartalucci, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwandishi wa
habari raia wa Thailand ameyataja mashambulizi hayo ya utawala katili wa
Kizayuni mjini Damascus kuwa yanaashiria ni namna gani Wamagharibi
walivyoshindwa na taifa hilo la Kiarabu. Amesisitiza kuwa, hatua hiyo
inaonyesha kwamba makundi ya kigaidi huko Syria ambayo yamelelewa na
Marekani, Israel na Saudi Arabia, yameshindwa kabisa kuiangusha serikali
halali ya Rais Bashar al-Assad, hivyo yanahitaji msaada wa uingiliaji
kijeshi wa Washington na washirika wake wa eneo hili. Ni wazi kwamba,
mashambulizi hayo ya ndege za Israel yamefanyika kwa msaada kamili wa
Marekani ikiwa ni katika njama na mipango iliyosukwa na Marekani
yenyewe. Hii ni katika hali ambayo, serikali halali ya Syria imetoa onyo
kali kwa utawala huo bandia na kusisitiza kuwa, jeshi la nchi hiyo
litajibu kila chokochoko za utawala wa Kizayuni katika wakati mwafaka.
Wakati huo huo, Russia nayo pia imeonya kuhusu uvamizi wowote ule wa
kijeshi wa nchi za Magharibi dhidi ya Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment