Sunday, May 5, 2013

Libya kuwafuta kazi mabaki ya utawala wa Gadafi

Congres ya kitaifa ya Libya imesema kuwa inachunguza mpango wa kuwafuta kazi mabaki ya utawala wa zamani wa nchi hiyo uliokuwa ukiongozwa na Kanali Muammar Gadafi.  Hatua hiyo imekuja kufuatia mashinikizo ya wanamgambo wanaobeba silaha na kwa mujibu wa mpango huo, wale wote waliokuwa  katika utawala wa zamani wa Muammar Gaddafi wataondolewa katika nyadhifa wanazozishikilia hivi sasa serikalini.
Hii ni katika hali ambayo wanamgambo wanaobeba silaha huko Libya siku kadhaa zilizopita walizishambulia na kuzizingira Wizara za Mambo ya Nje na Sheria za nchi hiyo huko Tripoli ili kushinikiza takwa lao la kufutwa kazi serikalini mabaki ya kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.

No comments: