Harakati ya waasi ya M23 imesema kuwa imesimamisha mazungumzo na
serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na Umoja wa
Mataifa kuidhinisha kikosi cha kupambana na waasi mashariki mwa Kongo.
Rene Abandi, kiongozi wa ujumbe wa M23 katika mazungumzo na serikali ya
Kinshasa yanayofanyika nchini Uganda amesema, mwenendo wa mazungumzo
hayo umeingia doa kutokana na Umoja wa Mataifa kupeleka kikosi cha
kupambana na waasi, na kwamba wana matumaini serikali ya Kongo DRC
itaelewa baadaye kwa nini vita haviwezi kutatua mgogoro wa mashariki mwa
nchi hiyo. Waasi hao pia wamesema kuwa, wanakisubiri kwa hamu kikosi
hicho na kwamba wako tayari kupambana nacho.
Hii ni katika hali ambayo, kikosi kipya cha jeshi la UN kinatarajiwa kuwasili hivi karibuni Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Hii ni katika hali ambayo, kikosi kipya cha jeshi la UN kinatarajiwa kuwasili hivi karibuni Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
No comments:
Post a Comment