Sunday, May 5, 2013

Bozize atuhumiwa ukiukaji wa haki za binadamu CAR

Francois Bozize Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aliyelazimika kuikimbia nchi baada ya waasi wa muungano wa Seleka kuchukua hatamu za nchi, anakabiliwa na tuhuma za kukiuka haki za binadamu katika nchi hiyo.  Mahakama ya Bangui ambao ni mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati imeanza uchunguzi kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na Francois Bozize.  Arsene Sende, Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ametangaza kuwa, mahakama ya Bangui imeanzisha uchunguzi kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na Francois Bozize pamoja na watu wake wa karibu katika kipindi cha uongozi wake katika nchi hiyo. Inafaa kukumbusha hapa kuwa, waasi wa SELEKA mwanzoni mwezi uliopita waliingia kwa kishindo katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui na kuipindua serikali ya Rais Francois Bozize ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Benin. Wakati huo huo, hivi karibuni mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati alisema kuwa, hali ya kibinadamu nchini humo inasikitisha mno. Wakati huo huo taarifa zaidi kutoka nchini humo zinasema kuwa,  maeneo mengi katika nchi hiyo  ayana maji safi ya kunywa na kwamba bidhaa muhimu hazipatikani madukani.

No comments: