Sunday, May 5, 2013

Salehi kuelekea Jordan kujadili mgogoro wa Syria

Dk Ali Akbar Salehi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anatazamiwa kufanya ziara rasmi nchini Jordan ili kuzungumza na maafisa wa ngazi ya juu wa nchi hiyo na kutafuta ufumbuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Syria. Ramin Mehmanparastm msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyasema hayo leo katika mkutano na vyombo vya habari hapa Tehran. Mehmanparast amesema kuwa Dakta Salehi karibuni hivi ataelekea nchini Jordan hasa kwa vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mwenyekiti wa hivi sasa wa harakati ya NAM na kutokana na Tehran kulipa umuhimu suala la kuendeleza mazungumzo na kustafidi na uwezo a kieneo ili kutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya kisiasa na kwa kupitia mazungumzo ya kitaifa yatakayoyashirisha makundi yote ya Wasyria.
Katika ziara yake ya siku mbili mjini Amman, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran atafuatilia juhudi za pamoja za nchi zilizo na ushawishi katika eneo hili ili kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Syria kwa kuzingatia nafasi muhimu ya Iran na Jordan katika eneo hili la Mashariki ya Kati.

No comments: