Yupo hospitali ya Columbia Asia-
BangaloreUbalozi wa India
Dar waombwa kusaidia
Waislamu watakiwa kufanya Subra kidogo
UBALOZI wa India jijiniDar
es Salaam umeombwakuingilia kati kuharakishakupatikana
kibali chakutibiwa Sheikh IlungaHassan Kapungu ambayeamelazwa katika hospitaliya
Columbia Asia Hospital-Bangalore, India.
Kibali kinachohitajikani kwa ajili ya kufanyiwaupasuaji wa
kuwekewa figo(kidney transplantation) baada
ya Sheikh Ilunga kupatamatatizo ya figo kushindwakufanya kazi ambayokitaalamu
hutwa- ‘chronicrenal failure’.Taarifa
kutoka kwa nduguna jamaa zinafahamisha kuwaSheikh Ilunga alilazwa katikahospitali ya Columbia AsiaHospital- Bangalore, tokamwezi wa Februari
mwakahuu 2013.Hata hivyo pamoja nataratibu zote za kupata nyarakana vibali vyote
husika ikiwa ni pamoja na kile cha Serikali yaTanzania, yaani, No ObjectionCertificate (NOC ), badoSerikali ya India haijatoa Visaya Matibabu
ambayo ndiyoitawezesha hospitali kufanyamatibabu ya kuweka figo.Habari za kiutafitizinaonyesha kuwa Ubaloziwa
Tanzania (Tanzania HighCommission)
uliopo NewDelhi, umesaidia sana katika jambo hili ikiwa ni pamojana kutoa kwa haraka na kwawakati ruhusa
iliyohitajiwa naSerikali ya India.Pamoja na kuwa hospitalihusika imekuwa ikitoahuduma nyingine za afyakwa Sheikh Ilunga kwakiwango cha hali ya
juu tokaamefika hospitalini hapo, hatahivyo,
kutokana na sheria zakimataifa juu ya upandikizajiwa viungo, kama hili la figo,hairuhusiwi kufanya matibabuhayo bila ya
kibali maalumu.Hiyo ni kutokana nakuwepo kwa biashara haramuya viungo duniani
na hivyokuwekwa sheria kali ilikudhibiti
biashara hiyo.Habari kutoka hospitaliniBangalore
zinafahamishakuwa tayari taratibu zoteza
kitabibu na malipozishakamilika ikiwa
ni pamojana kuwepo mtu wa kutoafigo, ambaye ni dada yakeSheikh Ilunga ambapo vipimovya kitaalamu vinaonyeshakuwa viungo vyao vinawiana,havina
tatizo.Habari za kiuchunguzi zagazeti hili zinaonesha kuwakutokana na hitajio
la SheikhIlunga kupatiwa matibabuya
haraka kulingana na afyayake inavyobadilika
kilauchao, uongozi wa hospitali(Columbia
Asia Hospital-Bangalore) ulimweka Ilungakatika orodha ya wagonjwawa kupewa kipaumbele katikamatibabu husika
toka katikatiya mwezi uliopita wa Aprili.
Na Mwandishi Wetu
Kutokana na hali hiyo,madaktari
wake wanaomtibiakatika hospitali hiyo
waliandikataarifa maalum ikielezea haliya ugonjwa wake na hitajio
lakufanyiwa matibabu harakawakitaraji kuwa
vyombohusika vitaharakisha kutoakibali
husika. Naye mkuu wa jopo lamadaktari
wake Dr. RavindranT. Jumapili iliyopita tarehe 20Mei, 2013 alitoa taarifa yakitabibu
akionyesha umuhimuwa mgonjwa Ilunga HassanKapungu kupatiwa
matibabu(Renal replacement therapy)haraka.Hata hivyo, hadi tunakwendamitamboni jana
bado majibuya kitengo husika huko India,yaani,
Foreigners RegistrationBureau, Bangalore, walikuwa bado hawajatoa
kibali. Ndugu waliopo Indiawanasema
kuwa kilawanapofuatilia katika ofisihiyo, jibu mara zote limekuwa“
Your case is still pending.”
Ufupi wa manneo, ikiwa namaana kuwa suala lenu
badolinashughulikiwa.Katika kufuatilia sualahili,
kamati inayoshughulikiamatibabu ya Sheikh
Ilunga, juziililazimika kutuma
mjumbehadi Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, na kukutana naMkuu wa
Kitengo cha Afya(Medical Attache) ili kutafutamsaada
zaidi wa kiserikaliambapo taarifa
zinasema kuwayalifanyika mawasiliano
yaharaka katika taasisi husikakule Bangalore.Juhudi hizo zikifanyikahuko
India, habari zaidi zakiuchunguzi
zinaonyeshakuwa taasisi ya IslamicPropagation Centre yenyeMakao Makuu yake jijiniDar es Salaam imemwandikiaBalozi wa India,
ikimwombakutumia uwezo wake na kwakuzingatia
uhusiano mzuriuliopo baina ya
Tanzania naIndia, kuingilia kati suala hilina kuwasiliana na kitengocha
Foreigners RegistrationBureau,
Bangalore, kutoa kibalikinachohitajika
kuwezeshamatibabu kufanyika.
Wakati huo huo,
Waislamuwametakiwa
kuwa na subrana kuzidisha Dua kwaSheikh
Ilunga wakati juhudizikifanyika kuwasiliana
naUbalozi wa India kuhakikishakuwa anapata matibabustahiki.Wito huo umetolewakutokana na Waislamuwengi kutaka kujua haliyake, wakihoji ni kwaninimpaka sasa Sheikh Ilungahajawekewa figo wakatimtu wa kutoa sadaka yafigo
alishapatikana, fedha zamatibabu zishalipwa,
hukuwengine wakitaka kufungasafari kwenda India kumjuliahali.Kutokana na habarizilizotolewa na kiongoziwa kamati inayosimamiamatibabu ya Sheikh
Ilunga, bado kuna imani kubwakwamba kupitia kwa Baloziwa India, jijini Dar es Salaam,kibali husika kitapatikanaharaka
iwezekanavyo baadaya kufikishiwa tatizo
hilimapema wiki hii ofisinikwake.Kwa
sababu hiyo, Waislamuwametakiwa
kufanya subrawakisubiri jibu la Balozi nakama kutakuwa na tatizo
lakuhitajia mawazo na msaadawa Waislamu
wataarifiwa.Toka amalize ziara yakuzunguka nchi nzimaakitahadharisha kuwa
iwapodhulma haitakomeshwana nchi kuendeshwa kwauadilifu, inaweza
kuleta balaakatika nchi; afya ya SheikhIlinga
haikuwa nzuri hadiilipogundulika kuwa alikuwana matatizo ya kufeli figo.Katika makongamanoaliyokuwa akifanya hukuakitumia
mifano halisi, SheikhIlunga alionyesha kuwa kunamfumo usio rasmi
kikatiba nakisheria, ambao unawabaguaWaislamu
huku ukitoaupendeleo kwa Wakriosto.Akatahadharisha kuwa,hatuwezi kuzungumziakuwepo kwa amani ya
kweliya kudumu pamoja na umojawa kitaifa
bila kuangaliamadai ya Waislamu kuwakuna
ubaguzi na dhulma
chanzo:annur
No comments:
Post a Comment