Sunday, May 5, 2013
Maduro: Barack Obama ni rais wa mashetani
Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amemshambulia vikali Rais Barack Obama
wa Marekani na kuwita kuwa ni rais wa mashetani. Maduro ametoa matamshi
hayo makali dhidi ya Obama baada ya rais huyo wa Marekani kuhojiwa na
kanali moja ya televisheni ya lugha ya Kihispania. Akihojiwa na kanali
ya televisheni ya Univision, Obama alikataa kusema iwapo anamtambua
Maduro kuwa ni rais halali wa Venezuela au la. Vile vile Obama ameuita
mrengo unaotawala nchini Venezuela kuwa ni wa kifashisti. Akijibu
matamshi hayo ya Obama, Rais wa Venezuela amesema kuwa, kazi yetu sisi
ni kulinda taasisi zetu, amani na demokrasia ya wananchi wa Venezuela na
tunaweza kukaa na kila mtu, hata kiongozi mkuu wa mashetani. Vile vile
Rais Maduro amemlaumu vikali rais huyo wa Marekani kwa kuwasaidia
kifedha wapinzani nchini Venezuela. Maduro amesema pia kwamba, ni Obama
mwenyewe ambaye ni kitimbakwiri cha madola ya kibeberu ndiye aliyetoa
fedha nyingi kuusaidia kifedha mrengo wake ambao lengo lake kubwa ni
kuiangamiza Venezuela. Tarehe 14 mwezi uliopita wa Aprili, Maduro
alichaguliwa na wananchi wa Venezuela kuiongoza nchini hiyo, jambo
ambalo limewahamakisha sana viongozi wa Marekani ambao wanashindwa
kuficha hamaki zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment