Nchini Tanzania Mei nne ni siku ya kitaifa ya Albino ambapo jopo la
wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka mamlaka zote
husika kuzuia mauaji ya Albino na uchunguzi wa kina ufanyike dhidi ya
watekelezaji wa vitendo hivyo. Mmoja wa wataalamu hao Juan E. Méndez
amesema utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kikatili hauwezi
kuhalalishwa na kwamba kwa mujibu wa sheria za kimataifa ni jukumu la
serikali kuwapatia albino ulinzi dhidi ya wale wanaotaka kuwaua. Ametoa
kauli hiyo kutokana na kuwepo kwa taarifa za mauaji ya albino na viungo
vyao kutumiwa kwa imani potofu za kishirikina nchini Tanzania na katika
baadhi ya nchi barani Afrika. Mtaalamu mwingine wa Umoja wa Mataifa,
Kishore Singh ambaye anahusika na elimu amesema kuwepo kwa siku ya
kitaifa nchini Tanzania ni fursa kubwa ya kumulika tatizo hilo na kuibua
mjadala kuhusu masaibu yanayowakumba albino nchini humo.
No comments:
Post a Comment