JE,
NI KWELI PASAKA NI SIKUKUUYA KUFUFUKA
KWA YESU?
Adhuhuri moja wakati nikiwa nyumbani
alikuja jamaa yangu mmoja ambaye aliniletea bakuli maalum la kuhifadhia
chakula. Ndani ya bakuli lile kulikuwa na wali na nyama ya kuku ambavyo kwa
hakika vilinitamanisha sana hasa ukizingatia nilikuwa na njaa kali. Nikaona ule
ndiyo wakati haswaa wa kujifaidia kile nilicholetewa.
Baada ya kuutwanga wali ule ndipo
nilipopatwa na shauku ya kujua Yule jamaa yangu alipata wapi ujuzi wa kupika
wali mtamu namna ile na kumtayarisha kitaalamu, kuku yule wa kienyeji. Ndipo
jamaa yangu aliponiambia kuwa chakula kile amekipika maalum kwa ajili ya
kusherehekea sikukuu ya kufufuliwa kwa Yesu Kristo maarufu kwa jina la Pasaka.
Kwa miaka mingi nimekuwa nikisikia kuhusu
siku hiyo na ndipo baada ya kuambiwa vile na jamaa yangu, nilipoamua kuandika
makala haya ili kuuelezea umma juu ya historia ya sikukuu hiyo na mwanzilishi
wake na lengo la kuwepo kwake.
Historia ya
pasaka
Pasaka ni sikukuu iliyoanza kwa nabii Mussa,
kumbuka kuwa wana wa Israel walikuwa utumwani nchini Misri chini ya utawala wa
mfalme Firauni(Farao) takribani miaka 400 walikuwa wanateswa na mfalme Farao.
Baada ya mateso ya muda mrefu mungu akamtoa
Mussa na kumfanya kwa Nabii na akaamrishwa kwenda kupambanana na Farao ili
awakomboe wana wa Israel na wawe huru.Ndipo Mussa akaenda kwa firauni na
akafanikiwa kumshinda Farao.
Baada ya Mussa kumshinda farao akaondoka na wana wa Israel (wayahudi)
akavuka nao katika bahari ya Shamu,Firauni naye alipojaribu kuvuka pamoja na
jeshi lake aliangamizwa baharini.
Baada ya mussa kuvuka salama na wana wa
Israel mungu akawapa amri ya kufurahia kutoka utumwani na ndipo sikuku hiyo ya
pasaka ilipoanzia hapo rejea katika kitabu cha kumbukumbu la torati 16:1-6)
“1
Utunzwe mwezi wa Abibu ukamfanyie pasaka Bwana mungu wako kwa kuwa ilikuwa
mwezi wa Abibu alipokutoa misri usiku Bwana Mungu wako, 2 Nawe umchinjie pasaka
Bwana Mungu wako katika kundi la kondoo na la ng’ombe mahali atakapochagua
bwana apakalishe jina lake,3 Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu ,siku
saba unakula naye mikate isiyotiwa chachu nayo ni mikate ya mateso kwa maana
ulitoka nchi ya Misri kwa haraka ili upate kukumbuka siku iliyotoka nchi ya
Misri siku zote za maisha yako, 4 Wala isionekane kwako chachu muda wa siku
saba katika mipaka yako yote wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza
jioni kisilale chochote usiku kucha hata asubuhi,5 Usimchinjie pasaka ndani ya
malango yako yote akupayo Bwana Mungu wako ,6 Ila mahali atakapochagua Bwana
mungu wako apakalishe jina lake ndipo mtakapomchinjia pasaka jioni katika
machweo ya jua kwa wakatika kama uliotoka misri”
Baada ya kuangalia maandiko kutoka katika
kitabu cha kumbukumbu la torati sasa tuangalie tena katika kitabu cha pili cha
Nabii Musa kiitwacho “KUTOKA”
Katika kitabu cha kutoka pia tunaona kuwa
asili ya sikukuu ya pasaka ilianza kwa Nabii Mussa baada ya kutoka misri na
wana wa Israel rejea Kutoka 12:42-51
“42
Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za Bwana kwasababu ya kawatoka katika nchi ya
Misri ,huu ndio usiku wa bwana ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israel
wote katika vizazi vyao, 43 Bwana akawaambia Mussa na Haruni Amri ya pasaka ni
hii, mtu mgeni asimle 44 Lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa
fedha,ukiisha kutahiri ndipo hapo atamla pasaka.45 Akaaye kwenu hali ya ugeni
na mtumishi aliyeajiliwa wasimle pasaka, 45 Akaaye kwenu hali ya ugeni na
mtumishi aliyeajiliwa wasimle pasaka, 46 Na aliwe ndani ya nyumba moja ,usiichukue
nje ya nyumba nyama yake yoyote wala msifunje mfupa wake uwao wote. 47 Na
wafanye jambo hili mkutano wa Israel wote. 48 Na mgeni atakapoketi pamoja nawe
na kupenda kumfanyia Bwana pasaka waume wake wote na watahiriwe ndipo hapo
akaribie na kufanya pasaka ,naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika
nchi lakini mtu yeyote asiyetahiriwa asimle. 49 Sheria ni hiyo moja kwa mtu
aliyezaliwa kwenu na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini. 50 Ndivyo walivyofanya
wana wa Israel wote kama Bwana alivyowaagiza Mussa na haruni ndivyo walivyofanya.
51 Ilikuwa siku ile ile moja,Bwana akawatoa wana wa Israel katika nchi ya Misri
kwa majeshi yao”(KUTOKA 12:42-51)
Kwa maelekezo hayo hapo juu kutoka katika
kitabu cha tano cha Mussa kiitwacho “KUMBUKUMBU LA TORATI” na kitabu cha pili
cha Mussa kiitwacho “KUTOKA” moja kwa moja tunaona kuwa pasaka ni sikukuu
iliyoanza wakati wa Nabii Mussa baada ya kuamriwa na Mungu wake kusheherekea
pasaka pamoja na wana wa Israel kwa kuchinja Kondoo na Ng’ombe baada ya Mussa
kufanikiwa kuwatoa wana wa Israel kutoka katika mikono ya mateso ya mfalme
Firauni(Farao),Hivyo kwa maneno hayo moja kwa moja tunaona kuwa sikukuu ya
pasaka si kufufuka bwana Yesu kama
baadhi ya wakristo wanavyodai
Jambo la kushangaza na kustaajabisha ni
kuona baadhi ya watu hususani jamii ya Wakristo wakidai kuwa pasaka ni sikukuu
ya kufufuka kwa Yesu wakati kwa mujibu wa vitabu vyao wanavyoviamini na
kuvitumia kila siku vinakanusha suala la pasaka kuwa ni sikukuu ya kufufuka
Bwana yesu.
Baada ya kuona maandiko hayo hebu
tuangalie je kweli bwana yesu alikufa na kufufua na je wanaosheherekea pasaka
kuwa ni sikukuu ya kufufuka yesu wako sahihi?
LUKA
2:41-45 “Basi wazee wake huenda
yerusalemu kila mwaka wakati wa sikuku ya pasaka.Na alipopata umri wa miaka
kumi na miwili walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuuu.Na walipokwisha
kutimiza siku wakati wa kurudi kwao,Yule mtoto yesu alibaki nyuma huko
yerusalemu na wazee wake walikuwa hawana habari.Na wakadhani ya kuwa yumo
katika msafara wakaenenda mwendo wa kutwa wakawa wakimtafuta katika jamaa zao
na wenzao.Na walipomkosa wakarejea Yerusalemu huku wakimtafuta”
Kwa maelezo hayo hapo juu tunaona kuwa
hata yeye mwenyewe yesu alikula sikukuu ya pasaka wakati akiwa mdogo na umri wake
ulikuwa ni miaka kumi na miwili akiwa na wazee wake ambao walikuwa wakienda
Yerusalemu kama ilivyokuwa desturi yao.
Swali la kujiuliza hapo je ni nani alikufa
na kufufuka ikiwa Yesu mwenyewe alikula pasaka akiwa na umri wa miaka kumi na
miwili je kusema kuwa sikukuu ya pasaka ni kufufuka kwa Yesu je huyo ni yesu
gani?
Ukweli ni kwamba kusheherekea sikukuu ya
pasaka ni kupoteza mwelekeo kwani sikukuu hiyo ya pasaka ni sikukuu ya
wayahudi.
Ushahidi unaothibitisha kuwa pasaka ni
sikukuu ya wayahudi ni YOHANA 6:4 “Na pasaka sikuku ya wayahudi ilikuwa karibu”
Nihitimishe makala hii fupi ya UKWELI
KUHUSU PASAKA kwa maneno ya kitabu kitukifi cha QUR’AN pale ambapo ALLAH S W
aliposema katika sura ya 4:157-158
“Na kwaajili ya kusema kwao sisi tumemuua
Masihi Isa mwana wa Mariamu mtume wa mungu hali hawakumuua wala hawakumsulubu
bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani Nabii Isa) Na kwa hakika wale
waliokhitalifiana katika hiyo(ya kumuua Isa)wako katika shaka nalo (jambo hilo
la kusema kauawa)wao hawana yakini juu ya jambo hili isipokuwa wanafuata dhana
tu.Na kwa yakini hawakumwua. Bali Mwenyezimungu alimnyanyua kwake na
Mwenyezimungu ni mwenye nguvu na mwenye hikima.
Kwa aya hiyo ndipo ambapo tunaona kuwa
Nabii ISSA(a.s) au YESU hakufa wala hakusulubiwa ila walifananishiwa tu hao
mayahudi waliotaka kumsulubu na kumuua bwana Yesu.
Hivyo kusheherekea sikukuu ya pasaka ni
kufuata mila za wayahudi na watu wasio na dini.
Kwa
kifupi huo ndio ukweli kuhusu pasaka na historia yake ambapo tumeona kuwa
pasaka ilianza kwa Nabii Mussa pale alipoambia na Mungu wake aende kwa
Firauni(Farao) akawaokoe wana wa Israel kutokana na mateso waliyokuwa
wanayapata kutoka kwa mfalme Firauni(Farao) lakini pia tumeona kuwa pasaka ni
sikukuu ya iliyokuwa inasheherekewa na mayahudi wa kipindi hicho.
Nakuacha na swali hili; Kusema kuwa pasaka
ni siku ya kufufuka kwa Yesu je ni Yesu gani huyo aliyekufa na kufufuka wakati
yeye mwenyewe amekula pasaka?
Makala
hii imeandaliwa na
Adinani H chorobi 0753-733217
1 comment:
Asante sana kwa elimu
kwa atakae sherehekea nn hukumu yake
Post a Comment