Mahakama moja nchini Misri imewahukumu wafuasi 11 wa
aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi kifungo cha kati ya miaka
mitano hadi minane jela kwa kufanya maandamano.
Washtakiwa hao walikamatwa kufuatia msururu wa
ghasia zilizozuka baada ya kundolewa madarakani kwa Mohammed Morsi mwaka
uliopita.
Mnamo mwezi Machi, zaidi ya wafuasi 500 wa Mohammed Morsi walihukumiwa kifo katika mahakama hiyo hiyo.
kesi hiyo inajiri wakati ambapo kuna msako dhidi ya waislamu wenye itikadi kali wanaomuunga mkono Mohammed Morsi.
No comments:
Post a Comment