Waziri mkuu nchini Korea Kusini amejiuzulu kutokana
na vile serikali yake ilivyolichukulia swala lote la ferry iliozama siku
kumi na moja zilizopita.
Chung Hong Won amesema kuwa kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake.
Bwana Chung alizomwa alipozitembelea
familia za waathiriwa waliotoweka katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya
kuzama katika hali ya kutatanisha.
Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji katika
tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani waliko,wengi
wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika ziara ya
shule.
Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama.
Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo.
(bbc)
No comments:
Post a Comment