Sengerema
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya
Sengerema mkoani Mwanza Bw Mohamed Shaaban Mohamed, amekuwa na malumbano na viongozi wa umoja wa vijana UVCCM Bw Robert Madaha na Bw Benedicto Bujiku baada
ya mwenyekiti wa umoja huo Bw Madaha kusema hatoshi katika nafasi yake ya
ukatibu kwa viongzi wa mkoa walipokuja
kuhudhuria kwenye kikao cha kamati ya siasa wilaya sengerema kilichofanyika
march 22, mwaka huu.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti viongozi hao wa umoja wa vijana walisema kuwa hawakuwahi kuwa na malumbano
yoyote na katibu wa chama hicho Bw Mohamed isipokuwa malumbano yao yalianza march
mwaka huu baada ya viongozi wa mkoa kuwasili sengerema march mwaka huu kwa
lengo la kujadili watumishi wa chama katika mienendo yao ya kazi.
Aidha Madaha aliongeza kuwa baada ya kumaliza kikao
baadhi ya wajumbe ambao sio waadilifu walivujisha siri na kumwambia Katibu wao
kuwa hatoshi katika nafasi yake apelekwe mtu mwingine atakaeziba pengo lake
ambapo tangu hapo Mohamed alianza ktafuta visa vya kumng’oa nafasi yake ili
asiwe anahudhuria kamati ya siasa wilaya.
“Mimi Mohamed mambo yote anayoniundia ya vijana
kunipiga mawe ni kwasababu tu walikuja katibu wa CCM Mkoa akiwa na baadhi ya
viongozi wenzake kwenye kamati ya siasa ya mwezi wa tatu…… katika kujadili
masuala ya watumishi baadhi walitoka nje ili tujadili na tukajadili vizuri na
ilipofika zamu ya wengine nao walitoka wakajadiliwa ila sasa baada ya hapo kuna
mwenzetu mmoja ambaye ni diwani mwenzangu sipendi kumtaja jina alimfuata katibu
na kumwambia kuwa madaha amekuharibia kwa viongozi” alisema madaha.
Hata hivyo baada ya siku chache kupita inasadikiwa
katibu wa CCM wilaya aliwahamasisha wajumbe na wasiokuwa wajumbe wa umoja wa
vijana CCM kwenda polisi kufungua kesi
ya wizi wa pikipiki za umoja huo ambapo walifanikiwa kufika polisi na kufungua
kesi ya wizi wa pikipiki na hadi sasa inaendelea.
Aidha upotevu wa pikipiki hizo pia kuna muhusisha
katibu wake wa vijana ambapo baada ya kumuhoji katibu huo wa vijana kuhusiana
na upotevu wa piki piki hizo alidai kuwa kweli pikipiki hizo waliziuza kwa watu
watatu tofauti na bei tofauti kutokana na ubora wake na kuongeza kuwa waliziuza
kisheria kwa kufuata utaratibu wa umoja wao, ambapo kamati nzima tendaji ilikaa
kikao cha kuuza piki piki hizo na wajumbe waliohudhuria walisaini kitabu cha
mahudhulio.
“ Nashangaa
kwanini Mohamedi ananing’ang’ania mimi wakati piki piki ziliuzwa tangu mwaka
jana kabla hata hajaja alikuwepo Yule katibu mwingine Magdalena leo hii baada
ya kukorofishana na madaha tu na mimi naingizwa katika mkumbo huo yeye alisema
shida yake ni mwenyekiti wa vijana na sio mimi……. Ndugu mwandishi kinachogomba
hapo ni mimi kuwa karibu na m/kiti wangu haaya yote ni majungu ya kisiasa tu
hakuna ukweli wowote.” Alisema Bujiku.
Katibu wa chama hicho alipoulizwa kuhusu suala hilo
alichojibu shida yake ni umwenyekiti wa umoja huo na sio udiwani wa Madaha ambapo alisisitiza
kuwa mwenyekiti huyo ajiuzuru wadhifa wake, na kuongeza kuwa ili Bujiku apone
aachane na madaha na akiendelea kuwa nae pamoja ataharibikiwa.
Na
Dotto Mgaza
No comments:
Post a Comment