Wananchi mkoani Mwanza, wametakiwa kudumisha Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ili kuwaenzi waasisi wa taifa hili hayati Amani Karume na Mwl Julias
kambarage Nyerere kwa kutenda mema waliyoyafanya.
Kauli hiyo ilitolewa na mgeni rasmi mkuu wa wilaya
ya Ilemela Amina Masenza ambaye alikuwa akimwaakilisha mkuu waa mkoa wa Mwanza
Eng Evarist Ndikillo alipokuwa akiwahutubia mamia ya watu kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya
muungano ambayo kimkoa yalifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Sengerema kata ya
Nyampulukano wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Bi Masenza alisema kuwa wananchi wote kwa ujumla
wanatakiwa kudumisha muungano wa Tanganyika
na Zanzibar kwa amani na utulivu na
kuwaepuka wanasiasa wenye uchu wa madaraka na wapotoshaji ambao wanataka
kuvuruga amani ya nchi ya Tanzania kwa
maslahi yao binafsi .
“Kuna kila sababu ya kuwakumbuka viongozi wetu hawa
wawili Karume na Nyerere kwani leo hii
tunaadhimishaa miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa wao
kutuonganisha, tumekuwa tukifanya biashara kwa pamoja na kuoleana” alisema Bi
Masenza
Aidha aliongeza kuwa wananchi waliowengi walizoea
serikali mbili ambapo muungano utakapovunjika wananchi wengine hawana pa
kukimbilia.
Pia katika hotuba yake alikemea ubaguzi wa rangi na
ukabila na kuwaasa wana Mwanza kudumisha muungano na kuonyesha mbegu bora
walizopanda ambapo changamoto za muungano ni fursa na sio kuvuruga amani ya
nchi.
“ Hatma ya muungano wetu ipo mikononi mwetu……
tuimarishe muungano wetu..” alisema Bi Masenza.
Na
Dotto Mgaza- Sengerema
No comments:
Post a Comment