Bunge
Maalum la Katiba limesema kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
katika Kamati ya Uandishi wa Katiba mpya hakutaathiri upatikanaji wa
katiba mpya.
Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamadi, alisema kitendo cha kujiuzulu
kwa mwanasheria mkuu, Othman Masoud Othman, ni jambo la kawaida na
kwamba uwakilishi wa Zanzibar ndani ya chombo hicho utakuwepo.
Alisema hajapata taarifa
rasmi ya kujiuzulu kwa Othman katika kamati hiyo ambayo ipo chini ya
Uenyekiti wa Mbunge wa Bariadi Mashariki, Adrew Chenge, lakini kama
amefanya hivyo atakuwa ametimiza wajibu wake kisheria.
Hamad, alisema kwamba mwanasheria huyo hakuingia katika Kamati ya uandishi wa Katiba mpya kutokana na wadhifa wake, bali ni uteuzi wake ulifanywa na uongozi wa Bunge hilo kama wajumbe wengine.
Katibu huyo aliongeza kuwa uwakilishi wa Zanzibar katika kamati hiyo
utakuwepo kwa sababu kuna wajumbe wengine kutoka upande huo wa Muungano
wanaendelea na kazi hiyo kikamilifu.
No comments:
Post a Comment