Thursday, April 25, 2013

Rais Nuseveni asema Afrika lazima iungane

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema ndoto yake kubwa ni kuona bara la Afrika likiungana na kuwa kitu kimoja. Rais Museveni amesema nchi za Afrika zimeendelea kuwa masikini kutokana na kuwepo ufisadi na kukosekana miungano thabiti ya kisiasa na uongozi bora. Amesisitiza kuwa, Wakoloni wamefanikiwa kuendeleza ukoloni mamboleo baada ya kumaizi kwamba Waafrika hawawezi kujichukulia maamuzi wenyewe bila ya kusukumwa. Huku hayo yakijiri, Marais wa nchi za Afrika Mashariki wanatarajia kukutana siku ya Jumamosi mjini Arusha, Tanzania ili kujadili changamoto zinazoikabili Jumuiya ya EAC. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anatarajiwa kuleta mitazamo mipya na itakuwa mara yake ya kwanza kuhudhuria mkutano wa aina hiyo tangu alipoapishwa kuwa rais Aprili 9.

No comments: