Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema
wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama
chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya.
“Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa
kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM
bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama
chao,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema kambi rasmi ya upinzani pia imeshindwa
kulinda utaratibu mzuri wa kutetea masilahi ya umma bila jazba na hoja
zenye mashiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipokuwa ikiongozwa na
CUF, Kiongozi huyo alisema kambi ya upinzani inapaswa ijipange upya
kwa utaratibu na mikakati mizuri ya kuteta hoja za wananchi bila
kuyumbishwa na wabunge wa CCM.
“Bunge usiwe uwanja wa kuonyesha mbwembwe za chama
bali uwe uwanja wa kutetea haki za wananchi, wabunge wanapaswa
wabadilishe mitazamo ya kuona bungeni ni sehemu ya kujionyesha kisiasa
na chama chako kinafanya nini nje ya Bunge,” alisema Lipumba.
Alisema viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilika kuhusu namna ya kutoa majibu bungeni.
Profesa Lipumba alisema mawaziri wengi wanakuwa
wakitoa majibu mepesi katika maswali ya msingi yanayoulizwa na wabunge
wa upinzani.
Alisema Bunge linatumia muda na pesa za walipakodi
vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwa na ubishi usiokuwa na tija,
kutoleana matusi na wengine kuingilia hoja za wenzao bila sababu za
msingi.
Profesa Lipumba pia alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda amepoteza uwezo wa kuliongoza Bunge.
No comments:
Post a Comment