Bei za vyakula katika mwezi huu wa Ramadhani zinaripotiwa
kupanda nchini Tanzania hususan katika jiji la Dar es Salaam.
Baadhi ya vyakula ambavyo hutumiwa na Waislamu kama
futari zinaonekana kupanda mno katika masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Taarifa zaidi zinasema, maeneo ya Dar es Salaam kama
Tabata Kimanga, Bima na hata Segerea yanashuhudia bidhaa za vyakula zikiwa juu
ukilinganisha na maeneo ya Kariakoo, Vingunguti na hata Magomeni.
Bidhaa kama magimbi, viazi zinadaiwa kupanda kutokana na
ugumu wa upatikanaji wake katika masoko. Baadhi ya wafanyabiashara wanasema,
kwa kipindi hiki mahitaji ni makubwa kuliko upatikanaji wa bidhaa, na kwamba,
hali hii imesababishwa na mvua kutokunyesha kwa wakati na kusababisha uhaba wa
mavuno.
Aidha katika mikoa mingine ya Tanzania pia kumeripotiwa
kupanda bei za vyakula vya mwezi wa Ramadhani kama mihogo, magimbi, viazi na
maboga.
Baadhi ya wafanyabiashara pia wamekuwa wakilangua kwa
makusudi vyakula wakifahamu kwamba, katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani
bidhaa hizo zinahitajika sana.
No comments:
Post a Comment