Bunge
Maalum la Katiba limesema kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
katika Kamati ya Uandishi wa Katiba mpya hakutaathiri upatikanaji wa
katiba mpya.
Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamadi, alisema kitendo cha kujiuzulu
kwa mwanasheria mkuu, Othman Masoud Othman, ni jambo la kawaida na
kwamba uwakilishi wa Zanzibar ndani ya chombo hicho utakuwepo.
Alisema hajapata taarifa
rasmi ya kujiuzulu kwa Othman katika kamati hiyo ambayo ipo chini ya
Uenyekiti wa Mbunge wa Bariadi Mashariki, Adrew Chenge, lakini kama
amefanya hivyo atakuwa ametimiza wajibu wake kisheria.
Hamad, alisema kwamba mwanasheria huyo hakuingia katika Kamati ya uandishi wa Katiba mpya kutokana na wadhifa wake, bali ni uteuzi wake ulifanywa na uongozi wa Bunge hilo kama wajumbe wengine.
Katibu huyo aliongeza kuwa uwakilishi wa Zanzibar katika kamati hiyo
utakuwepo kwa sababu kuna wajumbe wengine kutoka upande huo wa Muungano
wanaendelea na kazi hiyo kikamilifu.
Televisheni ya al Alam imetangaza leo kuwa, karibu Waislamu 1300
waliokuwa wamejificha katika eneo moja la pambizoni mwa mji mkuu wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, wamelazimika kulikimbia eneo hili kwa
kuhofia kushambuliwa na wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka.
Taarifa zinasema kuwa Waislamu hao leo wameonekana wakiingia kwenye
malori madogo 18 wakielekea maeneo ya kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya
Kati chini ya usimamizi wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika,
AU.
Televisheni ya al Alam imelinukuu shirika la habari la AFP likisema
kuwa, mara baada ya malori yaliyowabeba Waislamu kuondoka sehemu hiyo,
mamia ya wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka waliokuwa wanasubiri kwa
hamu mita chache tu, wamelivamia eneo hilo ili kufanya wizi na uporaji
dhidi ya mali za Waislamu hao.
Waislamu hao waliokuwa wamekimbia maeneo yao na kujificha katika eneo
hilo, hawakusalimika na ukatili wa wanamgambo hao wa Kikristo ambao
waliwazingira Waislamu hao hadi askari wa kulinda amani wa Umoja wa
Afrika walipofika na kuamua kuwahamisha katika eneo hilo.






